June 11, 2018

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA AWAPA ONYO KALI WANA CCM KILOLO ATAKA MBUNGE MWAMOTO NA MADIWANI WASIINGILIWE ....

Mwenyekiti  wa  CCM  mkoa wa  Iringa Albart Chalamila  akizungumza na wajumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM wilaya ya  Kilolo  leo 
Viongozi  wa  CCM  wilaya na mkoa  wa Iringa  wakiimba  wimbo wa  chama kabla ya  kuanza  kikao cha Halmashauri  kuu wilaya  leo 
Mwenyekiti wa CCM  mkoa  Albart Chalamila  kulia  akishuhudia  wana CCM  Kilolo wakimpokea kwa shangwe  leo 
Wajumbe  wa Halmashauri  kuu ya   CCM kilolo  wakidua 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila  akisisitiza jambo 
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  akieleza changamoto za usafiri Kilolo 
Mbunge wa  Kilolo  Venance  Mwamoto  akitoa kero za  wana Kilolo na mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika  jimbo  hilo mbele ya mwenyekiti wa CCM mkoa 
Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila  akipokelewa kwa heshima  kubwa  Kilolo 
Mwenyekiti wa CCM mkoa  akivishwa  skafu baada ya  kupokelewa  Kilolo leo 
Viongozi wa  CCM mkoa wa Iringa wakiongozana na  mwenyekiti wa CCM mkoa Albart Chalamila  na katibu wa CCM mkoa Christopher Mgala  kukagua  gwaride la  UVCCM 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akiwataka  makatibu  kufanya  usajili wa  wanachama 
Baadhi ya  wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM Kilolo  wakiwa katika  kikao  leo 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele akitoa  salam zake kwa  wana CCM 
Mbunge wa  Kilolo  Venance Mwamoto  kulia  akimkabidhi  zawadi ya  mbuzi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila kwa niaba ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya  CCM Kilolo 
Mwenyekiti wa CCM  mkoa wa Iringa Albart Chalamila  akiwa amebeba  mbuzi  aliyopewa  zawadi  na  wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM Kilolo leo 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Albart Chalamila  kulia  akimkabidhi  cheti  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  kutokana na  kuwa karibu wa CCM 
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akipongezwa na mwenyekiti wa  wilaya ya  Kilolo Kilian Myenzi mara  baada ya kukabidhiwa  cheti  cha pongezi na  mwenyekiti wa CCM mkoa 
Mwenyekiti wa  CCM  Kilolo  Kilian Myenzi  akimkaribisha mwenyekiti wa  CCM  mkoa wa Iringa 
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila amewaonya  wanachama wa chama  hicho  wilaya ya  Kilolo   kuepuka  kuanza kampeni za  udiwani na ubunge kabla ya  wakati .

Kuwa  CCM hakitamfumbia  macho wanachama  yeyote  ambaye atajihusisha na mbio  za udiwani ama ubunge katika jimbo hilo la Kilolo ambalo mbunge wake ni Venance Mwamoto .

“Huku nyuma kulikuwepo na baadhi ya wana CCM waliokuwa wakijinasibu kwamba wao ndio wenye chama na wana uwezo wa kuamua lolote bila maamuzi ya vikao vya chama kwa muda mrefu wana CCM hao walionekana watu wenye nguvu kuliko chama, nataka kuwaambia CCM ya sasa sio ya wakati ule, tunawasubiri wapiti kwenye reli, tuwashughulikie,” 

Chalamila  alitoa onyo hilo kali kwa  wana CCM kupitia wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM wilaya wakati wa  kikao  cha halmashauri kuu ya CCM ya wilayani hapo  leo .

Katika  kikao   hicho  ambacho ni mwendelezo wa vikao kama hivyo katika wilaya mbali mbali za  mkoa wa Iringa kikao cha kazi kwa ajili ya kuelezea mwelekeo wake wa usimamizi wa shughuli za chama katika kipindi cha uongozi wake tangu ashike wadhifa huo mwishoni mwa mwaka jana.

Alisema  kuwa tayari  amekwisha  jipanga yeye kwa  kushirikiana na vyombo  mbali mbali  za  kiusalama ndani ya  chama  kuweka  mtego wa  kuwabaini wanachama  walioanza kampeni na wasilalamike  watakapochukuliwa hatua kali .


" Tayari  nimeanza  kufanya uchunguzi kwa  wale  ambao  wanajipitisha katika kata na  jimbo la Kilolo kwa  ajili ya uchaguzi mkuu ujao narudia  tena  wakibainika  wanachama  hao  nitawapokonya kadi na kuwasimamisha  kujihusisha na  shughuli  yeyote  ya  chama "

Mbali ya  kutowataja majina wanachama hao  Chalamila aliwataka wana CCM hao kujitafakari na kama  wana ndoto  za  kuja kugombea wasitegemee tena kwani pindi  watakapobainika  watafukuzwa  chama .


Kwani  alisema baadhi ya  wana CCM  wanaoshiriki kuhatarisha amani ndani ya chama hicho ni wale waliopewa dhamana ya kuwa wajumbe wa vikao vikubwa vya chama  na kuwataka  kuachana na tabia   hiyo .

“Nasema Mwacheni  mbunge  Venance Mwamoto na madiwani wote wa Kilolo wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi kwa amani na utulivu  ili mbunge na madiwani  wamalize  miaka yao mitano bila kuingiliwa na mtu "


 Chalamila alisema makundi ndani ya  chama hayana nafasi na  kuwa visasi na mioyo ya kinyongo miongoni mwa wana CCM wakati na baada ya chaguzi za chama na jumuiya zake jambo ambalo limekuwa likisabisha mpasuko wa muda mrefu ndani ya chama hivyo ni lazima yaachwe na  wasioacha  watawajibika .Aliwataka wenye taarifa za wanachama wenye mienendo mibaya na inayotishia uhai wa chama waziwasilishe kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba ya chama ili ziweze kufanyiwa kazi.

Kuhusu  mwelekeo wake  katika uongozi wake kuwa ni kuendesha chama kwa kuzingatia msingi wa siasa safi zisizo na majungu ili kulinda taswira ya mkoa wa Iringa ulioharibiwa na siasa za majungu hasa  kipindi cha nyuma kabla yake .
Aidha  amewataka  wana CCM kujiandaa kwa uchaguzi wa mwakani wa Serikali za Mitaa  na  kuwa ni  uchaguzi muhimu unaosaidia kutathimini utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kuzingatia vipaumbele vyake na ndio unatoa dira ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2020.

Hata  hivyo  mwenyekiti  huyo  alimpongeza mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Asia  Abdalah na  viongozi wa CCM wilaya  hiyo kwa  kufanya kazi kama  timu  moja na  kuwa  toka ameanza  ziara  yake  Kilolo ni wilaya ya pekee  kukutana na  mkuu wa  wilaya na mbunge wa jimbo .

Katika hatua  nyingine  mwenyekiti huyo wa  mkoa amewataka   wajumbe wa Halmashauri  kuu ya  CCM wilaya na  viongozi  kuendelea  kutoa  elimu kwa wananchi  kuacha kuuza  ovyo ardhi huku  akipongeza uamuzi wa mkuu wa wilaya ya  Kilolo  kuzuia uuzaji kiholela  ardhi  yenye ukubwa wa  zaidi ya  ekari 4500.

Kwa upande wake  katibu wa CCM mkoa wa Iringa Christopher Mgalla aliwataka  watendaji wa CCM ngazi zote  kuhakikisha  wanasajili  wanachama kupitia mfumo rafiki  utakaokwenda sanjari na  sayansi na Teknolojia  ili  kuwezesha  mwenyekiti wa chama Taifa  kuongea na mwanachama  yeyote pindi anapohitaji akiwa Ikulu .

Hivyo  alisema  suala la uhai wa chama ni  vizuri  kwenda sambamba na  ulipaji wa ada  na usajili wa wanachama  wote .


Huku mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele aliwataka  wana  CCM hasa  wajumbe wa Halmashauri  kuu  kuendelea  kufanya kazi ya  kukijenga  chama badala ya  kukiingiza  chama katika makundi ambayo  yamekuwa  yakihatarisha  uhai wa chama .

Alisema  ndani ya CCM wanachama  wote  wanawajibu wa  kukijenga chama na  kuwa ni lazima katiba na  kanuni za  chama  kuzingatiwa  katika  uendeshaji wa chama .


Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  akieleza  utekelezaji wa ilani ya  CCM katika  wilaya  hiyo alisema  anaipongeza  serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt  John  Magufuli kwa kuendelea  kuharakisha maendeleo ya  Kilolo  hasa kwa  kuahidi  kushughulikia  changamoto ya  barabara ya Iringa - Kilolo .

Kuwa  kero  hiyo ya  barabara  hadi 2025   wanategemea  Kilolo  kuwa na lami  na  hivyo wananchi  wataondokana na kero   hiyo .

 Wakati  mbunge wa  jimbo la  Kilolo Venance Mwamoto pamoja  na  kumpongeza  mwenyekiti  huyo kwa  ziara  yake Kilolo  bado  alisema  ziara ya Rais ndani ya  wilaya ya  Kilolo  imeleta  matunda  kwa  wilaya  hiyo na kuwa tayari  serikali imetoa  pesa  za  miradi ya maji Ilula  na  kero ya maji  inaendelea  kufanyiwa kazi .

Pia  alisema ujenzi wa Hospitali ya  kisasa  ya  wilaya ya  Kilolo kilikuwa ni  sehemu ya  kilio  kwa wananchi wa Kilolo  ila  sasa ujenzi huo unaendelea  na  serikali ya Dkt Magufuli  imeahidi  ujenzi huo kumalizika haraka  zaidi .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE