June 3, 2018

MATUKIO KATIKA PICHA MAPACHA WALIOUNGANA ENZI ZA UHAI WAO

Mbunge  Venance  Mwamoto  akiwa na mapacha Maria  na  Consolata Mwakikuti  enzi za  uhai  wao 

Aliyekuwa katibu tawala wa  mkoa wa Iringa Getrude  Mpaka  akiwapa  zawadi mapacha hao 
mapacha wakiwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na viongozi wa benk ya NMB Kilolo pamoja na wanafunzi wenzao waliofanya mtihani wa kidato cha sita ..


Dc Kilolo na mlezi wa Maria na Consolata 
Image result for mapacha  Iringa
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akiwa amekaa na  mapacha walioungana  Maria  na  Consolata  Mwakikuti enzi  za  uhai  wao ,kulia ni mkurugenzi wa Halmashauri ya  Kilolo  Aloyce Kwezi  na kushoto  mbunge wa  Kilolo Venance  Mwamoto.

......................................................................................................................................................
MAPACHA  Maria na  Consolata  Mwakikuti  ni mapacha  ambao  wameacha simanzi kubwa si  tu wilayani  Kilolo mkoani Iringa  waliko soma  elimu yao ya  sekondari ama wilani Makete  walikozaliwa ila ni Tanzania  kwa  ujumla .

Mapacha hao  walizaliwa  wilani Makete  miaka  20  iliyopita  na mara  baada ya  kuzaliwa mama yao  alifariki  dunia na baadae baba  yao  maisha yao waliishi kwa  msaada  wa  shirika la Masisita  la Maria  Consolata ambao  ndio  walikuwa  wakiwalea hadi kifo  chao.

Serikali  ya  awamu ya  nne  chini ya  Rais Jakaya  Kikwete  ilikuwa  mstari wa  mbele katika  kuwasaidia  watoto hao   jitihada  hizo  ziliendelea  na serikali ya awamu ya tano  chini ya  Rais Dkt John Magufuli  ambae ni mmoja kati ya viongozi  waliokuwa  wa kwanza  kutuma  salam za  Rambi rambi kwa  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza .

Mazishi ya  watoto  hao yamepangwa  kufanyika Tosamaganga  wilaya ya  Iringa kati ya  jumanne na jumatano huku  wanafunzi wa  chuo cha Ruaha  na  wananchi wa Iringa  wataaga miili ya  Mapacha hao kati ya  kesho  .

Uongozi wa  Hospitali ya  Rufaa ya mkoa wa Iringa  pamoja na  kuthibitisha  kifo cha  mapacha  hao  umeeleza  sababu ya  kifo chao kuwa ni kutokana tatizo la njia ya  hewa .

Tayari  serikali ya  mkoa wa Iringa  kupitia mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  umewataka  wananchi  kujitokeza kwa  wingi  kutoa heshima  zao za  mwisho huku ukitaka  familia yake  kujitokeza  kushiriki mazishi hayo .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE