May 6, 2018

KUMEKUCHA IRINGA , TAYARI MKANDARASI WA UJENZI WA UKUMBI WA BILIONI 8.8 AKAMATWA


ZIKIWA  zimepita  siku siku tatu toka  Rais    Dkt  John Magufuli kuagiza    aliyekuwa  mkuu wa  chuo  kikuu  cha  Mkwawa mkoani  Iringa  Prof  Pak  Mushi   na  mkandarasi  wa kampuni ya  M& N  ambaye  alihusika  na  ujenzi  wa ukumbi wa  bilioni  8.8  katika  chuo  cha  elimu Mkwawa (MUCE ) kukamatwa  na kufikishwa mahakamani  kutokana na  ufisadi  tayari jeshi la  polisi mkoa wa Iringa linamshikilia  mkandarasi  aliyehusika na  ujenzi huo .

Kwa  mujibu wa kamanda  wa  polisi mkoa  wa Iringa  Juma Bwire  mkandarasi wa kampuni ya M&N ya  mkoaani ya  Iringa amekamatwa na  yupo  chini ya  ulinzi  wa  vyombo vya  usalama  mkoani hapa akiendelea  kuhojiwa  .

Kamanda  Bwire  alimweleza mwandishi wa habari hizi jana kuwa jeshi  la polisi la  taasisi ya kuzuia  Rushwa nchini (Takukuru) baada ya  agizo la Rais  kutaka  watuhumiwa hao kukamatwa walifanya  utekelezaji  wa haraka na  sasa mkandarasi  huyo  tayari amekamatwa .

" Tumemkamata  mkandarasi wa M&N ambae ni bwana  Mshana  na  kwa  sasa  anaendelea  kushikiliwa kwa mahojiano ya  Takukuru na baada ya  hapo atafikishwa mahakamani na  wengine  tunaendelea  kuwasaka "

Alisema kamanda  Bwire  kuwa hawapo  tayari  kufanya  subira katika  utekelezaji  wa agizo la Rais  na  kuwa watahakikisha  wote  wanakamatwa .

Akiwa mkoani  Iringa Rais Dkt  John Magufuli aliagiza  kukamatwa kwa  mkandarasi  aliyehusika na  ujenzi wa ukumbi  huo wa bilioni 8.8  pamoja na  aliyekuwa mkuu wa  chuo cha Mkwawa Prof  Mushi na  wote  waliohusika katika   mchakato  wa  utoaji wa  pesa  hizo bila kuzingatia  taratibu 

"Ujenzi huu wa  kifisadi na  ndio  lazima  tuwe  tunafika mahali  tuelezani ukweli  tu  haiwezekani  ukumbi huu Mkwawa  ujengwe  kwa bilioni  8.8  wakati   mabweni  yote ya chuo  kikuu  cha  Dar es Salaam  kinachochukua  wanafunzi 4000 yamemejengwa kwa shilingi  bilioni 10 “

Kuwa kuna Prof Mushi  aliyesimamia mradi huo bado  huyo  mtaa wakati  amefanya  ufisadi  huo  hivyo  atafutwe na  kupelekwa mahakamani  na  sio  kuwa maprofesa  hawatakiwi kwenda Mahakamani .

Huku  mkandarasi wa kwanza  aliyepewa  kazi  hiyo alilipwa  pesa  za kwanza  kinyume  na utaratibu wa  ukandarasi  kwani  mkandarasi hawezi  kulipwa  pesa kabla ya  kukabidhi  satifiketi ya kazi yake .

“  Sasa nilitegemea   kwenye  chuo hicho cha wasomi kikawa  kikaweza  kusimamia  vizuri  matumizi sahihi ya  fedha  wanafunzi  wanateseka kwa  kukosa sehemu ya  kukaa kutokana na watu  waliokuwa  wakiwaongoza na mimi  najua hamuwezi  kushangilia kwa kuwa mnawaogopa  sasa naomba mshangilie  maana  wote  watakamatwa  ifike  sehemu  sisi  watanzania  tuwe na uchungu wa kodi zao “

Hivyo  aliagiza chuo  kikuu cha  Dar es Salaam  (MUSE)  kuchukua  hatua ya  kusaka wote  waliohusika  na  kuwafikisha mahakamani   na kuiigiza  wizara ya  elimu  kufuatilia  vizuri mradi  huo .

Rais  Dkt Magufuli  alisema hawezi kutekeleza  ombi la mkuu wa chuo   hicho  cha Mkwawa  Profesa Estar Ndungumalo  la kuomba  mabweni  hawezi  kulitekeleza  kwani  ufisadi  uliofanyika hapo ni mkubwa na kuwa iwapo  watashughulikia  kuwasaka  wahusika  ataangalia  kutekeleza  ombi  hilo .

Aidha  Rais  Dkt Magufuli  ameliagiza  jeshi la polisi nchini ,taasisi ya  kuzuia  Rushwa nchini (Takukuru ) na vyombo  vingine kuwakamata  wote  waliohusika na  ufisadi  huo .

“ Mkimaliza  hilo  tatizo  mkuu wa  chuo cha MUSE  njoo  uniambie  nitakuja na mkakati wa kujenga  mabweni hapa Mkwawa mimi sina  tatizo “

Hata  hivyo  Rais  Dkt  Magufuli  amemwagiza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kufikisha  ujumbe kwa meneja wa TANROADS  Iringa ili  kutengeneza  barabara ya  lami katika barabara  ya  chuo  hicho  cha Mkwawa .

Kuhusu  maombi ya wanafunzi  juu ya kupewa mikopo  wote  alisema  haiwezekani kwa  serikali kuwapa  mikopo  wanafunzi  wote kwani  serikali imekuwa ikitoa  mikopo kutokana na hitaji la watumishi katika   kada  husika  kama  sasa hitaji ni  wahandisi na walimu .
 Akijibu  swali la wanafunzi kuhusu  ombi lao la kutaka  kuanzishwa kwa masomo ya ujasiliamali  alisema kuwa  jibu  la swali  hilo lipo  chini ya uwezo wa  mkuu wa chuo  hicho na  si lake kama  wanaona  linafaa wafanye .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE