May 11, 2018

WAZIRI LUKUVI KUTATUA MGOGORO WENYE ZAIDI YA MIAKA 40 DAR KESHO JUMAMOSI

Image result for lukuviWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anataraji kufanya Ziara Wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam siku ya jumamosi tarehe 12 Mei, 2018 saa 3 asubuhi.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri anataraji kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Boko – Kinondoni ili kutatua mgogoro wa Ardhi unaotambulika kama eneo la Somji.
Mgogoro huu ulioanza miaka ya 1970 ni wa muda mrefu unaohusu eneo lenye ukubwa wa hekari 357.5 baina ya wananchi na mtu anayedai kuwa ni mmiliki wa eneo hilo.
Waziri Lukuvi akiambatana na uongozi wa manispaa ya Kinondoni wanataraji kufika eneo hilo na kuutolea maamuzi mgogoro huo wa muda mrefu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE