May 15, 2018

Waziri Dkt Mwakyembe azindua Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri alipowasili katika Chuo cha Michezo Malya jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza kuzindua Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho
Mkuu wa Chuo cha Michezo Malya Bw. Richard Mganga (kulia) akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipowasili katika chuo hicho kuzindua Bodi ya Ushauri ya chuo hicho jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Eng. Mtemi Msafiri (aliyesimama) akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya Chuo cha Michezo Malya jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. Wapili kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Dkt. Richard Masika
Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (aliyesimama) akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya Chuo cha Michezo Malya jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Dkt. Richard Masika
: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Malya Mhandisi Dkt. Richard Masika na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Eng. Mtemi Msafiri
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wakifuatili hotuba ya Waziri Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya Mhandisi Dkt. Richard Masika (katikati) akizungumza baada ya bodi yake kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo
: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya baada ya kuzindua bodi hiyo jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Eng. Mtemi Msafiri na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya Mhandisi
Dkt. Richard Masika
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Michezo Malya baada ya kuzindua Bodi ya Ushauri ya chuo hicho jana katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza
Baadhi ya wanachuo cha Michezo Malya wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) baada ya kuzindua bodi ya ushauri ya chuo hicho na kukutana na wanachuo jana katika wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
 ....................................................................................................
 
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 15/05/2018
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa Bodi ya ushauri wa Chuo cha Michezo Malya kutumia kila aina ya ubunifu kuzigeuza changamoto zilizopo katika chuo hicho kuwa fursa ili kukipa chuo sura na nafasi yake stahiki kuwawezesha wahitimu kutambulika ndani na nje ya nchi.
Rai hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri jana katika Chuo cha Michezo Malya katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kusema kuwa Chuo cha Michezo Malya ni chuo cha pekee nchini hivyo hakina budi kuzalisha wataalamu wa kutosha wa kufundisha michezo katika shule, vyuo mbalimbali  na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Mwenyekiti na wajumbe wa bodi hii ni changamoto ya kwanza inayowakabili kuhakikisha kuwa taasisi hii yenye wajibu adhimu katika maendeleo ya michezo nchini mnaitangaza na kuiongezea thamani upya ili taasisi hii iweze sio tu kujulikana na watanzania bali vile vile ihudumie vijana wengi wenye ari kubwa ya kupata ujuzi katika michezo kutoka nchi mbalimbali” amesema Mhe. Mwakyembe
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Michezo Malya Mhandisi Dkt. Richard Masika amesma kuwa Bodi imedhamiria kufanya kazi kwa weledi, ubunifu uadilifu na bidii katika kushauri na kusimamia Chuo cha Michezo Malya ili kitekeleze ipasavyo maudhui na madhumuni ya kuanzishwa kwake.
Aidha Mhandisi Dkt. Masika amesema kuwa Chuo cha Michezo Malya ni dhana muhimu katika michezo kwa taifa letu kwani kinahitaji kuwa na wataalamu wa michezo wanaokidhi viwango vya taifa na vya kimataifa hivyo chuo kizingatie kuwa na wakufunzi mahiri, mitaala bora na mafunzo yenye ithibati
Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo ametoa rai  kwa wafanyakazi wa chuo cha Malya pamoja na wanachuo kuwapa ushirikiano bodi hiyo mpya ya ushauri ili baada ya miaka michache Chuo cha Michezo Malya kiweze kuvune mafanikio chanya yatakayokidhi mahitaji ya wakufunzi wa michezo ndani na nje ya nchi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Eng. Mtemi Msafiri amewaomba Wajumbe wa bodi kuangalia namna ambavyo watawaunganisha wataalamu wanaopatikana kutoka katika Chuo cha Michezo Malya na wadau hususani Wizara ya Elimu na Tamisemi kwani wadau wote wanaotoka katika chuo hicho nia yao ni moja ya kukuza michezo nchini.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE