May 29, 2018

WANANCHI WA HALMASHAURI MJI MAFINGA WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 954.5 MIRADI YA KIMAENDELEO

Viongozi  mbali  mbali wa Halmashauri ya  mji Mafinga  wakisubiri  kupokea  Mwenge 
Mmoja kati ya  wakimbiza  Mwenge  akikaribishwa na  mkurugenzi wa mji Mafinga Saada Mwaruka 
Vitanda  kwa  ajili ya  bweni la  wanafunzi Mnyigumba  
Wananchi  mtaa wa Tanganyika  Mafinga  wakishika  mwenge 
Tanki la maji la  mtaa wa  Tanganyika  
Wanawake  wakisubiri  kuzinduliwa  kwa mradi wa maji 
Kiongozi wa  mbio za  Mwenge  Kitaifa  Chalresy  Kabeho  akikagua  tanki la maji 
Kiongozi wa  mbio za  mwenge  Kitaifa Chalresy  Kabeho  akitoa maagizo katika  mradi wa maji mtaa wa Tanganyika
Mhandisi  wa  maji  akijibu maswali kwa  kiongozi wa mwenge 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya  mji Mafinga Saada Mwaruka  akiwa  na mwenge  wa Uhuru 
Mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi Wiliam  Jamhuri  akiwa na mwenge wa  uhuru 
Mkuu  wa  wilaya  ya  Mufindi Wiliam  Jamhuri (kushoto)  akimkabidhi mwenge  wa  Uhuru  mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  mara baada ya  mwenge  kumaliza  mbio  zake  katika  mkoa  wa  Iringa kwa  kuzindua  miradi ya  kimaendeleo  8  katika Halmashauri ya  mji Mafinga
......................................................................
Na  MatukiodaimaBlog


WANANCHI  wa Halmashauri ya Mji  Mafinga wilayani  Mufindi  mkoani  Iringa wamechanga   kiasi cha  shilingi 954,545,000 kwa  ajili ya  kukamilisha  miradi ya  kimaendeleo iliyozinduliwa  na  mbio  za  mwenge  wa  uhuru mwaka  huu .

Akisoma  risala  ya  utii kwa  Rais  Dkt John Magufuli mbele  ya  kiongozi  wa  mbio  za  mwenge  Kitaifa Chalresy  Kabeho ,mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi  Wiliam  Jamhuri  katika  viwanja  vya Mashujaa mjini Mafinga  alisema  kuwa  wananchi hao  wameungana na  serikali katika  kutekeleza  miradi  hiyo  8  iliyogharimu  kiasi  cha shilingi bilioni 1,781,296,053.

 Mkuu  huyo wa wilaya  aliitaja  miradi hiyo  kuwa ni  pamoja na mradi  wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya  sekondari Mnyigumba  lililojengwa  kwa  kiasi  cha  shilingi milioni 81,910,000 wakati  mchango wa  wananchi  ni shilingi  milioni 14,810,000 ,wahisani  walichangia  shilingi milioni 38 ,serikali  kuu  ikichangia  shilingi milioni 2  na  Halmashauri  ya  mji Mafinga  ilichangia  shilingi milioni 27,100,000.

Miradi  mingine ni hifadhi ya mazingira   ambao wananchi  wamechangia milioni 560 , mradi  wa tanki la maji  lita 500,000 mtaa wa  Tanganyika ambao serikali  kuu  imechangia  shilingi milioni 407,658,553, mradi  wa  kilimo cha  Parachichi  mtaa wa  Ndoleza ambao ni mradi wa mtu  binafsi  uliotumia  kiasi  cha  shili ngi milioni 30.8 ,mradi wa  ujenzi wa madarasa mawili shule ya  sekondari ya  Ihongole  ambao  wananchi walichangia milioni 2.8 na  Halmashauri  ikichangia  shilingi  milioni 19,841,900 matengenezo  ya  barabara  kilimita 15  kati ya Changarawe na Matanana  uliotumia  kiasi cha  shilingi milioni 331,633,100 mradi  ambao  hata  hivyo  haukufunguliwa na mwenge  kutokana na kujengwa  chini ya  kiwango.

Pamoja na miradi  hiyo pia  alisema  miradi mingine ni Zahanati ya Nipende  mtaa wa Amani  iliyojengwa kwa  shilingi milioni 346 ,Klabu ya kuzuia na kupambana na  Rushwa katika shule ya  sekondari JJ Mungai uliotumia  kiasi cha  shilingi 200,000. hivyo  alisema  kwa  ujumla  wake  wahisani  wameshiriki  pia  kuchangia  miradi  hiyo kwa  kutoa  pesa  kiasi cha  shilingi milioni 38 huku  Halmashauri ya Mji  Mafinga katika  miradi  yote  imechangia  shilingi milioni 47.2 na Serikali  kuu  imechangia shilingi  milioni 741 .4

Hata  hivyo  alisema hali ya  miradi  iliyofunguliwa na mbio za Mwenge  mwaka 2017 miradi  yote 14 iliyogharimu kiasi  cha  shilingi  bilioni 3,7 inaendelea  vizuri .

Jamhuri  alisema  kuwa  Halmashauri ya  mji  Mafinga  ilitarajia  kukusanya  jumla ya  shilingi 42,208,000 kiasi  ambacho  kilikusanywa ni  shilingi 25,083,300 sawa na  asilimia 59.4 ya  makisio  na kati  ya  fedha  hizo shilingi 14,435,600 sawa na  asilimia 57.55 zilitumika  kukamilisha  miradi  ya  kimaendeleo na  shilingi 10,647,700 zilitumika  kwa shughuli  za  ukimbizaji  Mwenge kwa  mwaka huu na  kuwa  tayari  Halmashauri  hiyo  imekusanya  shilingi 45,973,500

Aidha  alisema  kuwa Halmashauri   hiyo  imeendelea  kuelimisha  wananchi juu ya  dhana ya elimu  bila malipo utoaji wa elimu ya  msingi  bila  malipo kwa  shule zote  37 za  serikali pamoja na  kufanya  mikutano na vikao   kwa kamati  za  shule viongozi wa kata na  mitaa kwa  kuwashirikisha  pia  wazazi  pamoja na wananchi  wote .

Kuwa  wamekuwa  wakifanya  hivyo  kuwaelekeza  wajibu  wao  wa  kuwanunulia  sare  za  shule na  michezo pamoja  na  vifaa vya  kujifunzia ikiwa ni  pamoja na kuweka  utaratibu  wa utoaji  wa  chakula  cha mchana kwa kuzitumia kamati  za  shule na  sio  walimu .

Aidha  alisema  kuwa Halmashauri   hiyo  imeendelea na mkakati  wa  ufuatiliaji na usimamizi wa mifumo ya  ithibati  na  uthibiti  wa  ubora  wa  elimu  ambapo  kwa  kipindi  cha julai mwaka  2017 hadi machi 2018 jumla  ya  shule 18 kati ya  36 zimekaguliwa pia shule  za  sekondari zimefanyiwa  uthibiti  wa  ubora .

Kwa  upande  wake  kiongozi  wa  mbio  za  Mwenge  Kitaifa Kabeho  alisema  kuwa  ni lazima  wananchi kuendelea  kuchangia  miradi  ya  kimaendeleo pamoja  na  kutimiza  majukumu yao kwa  kuwanunulia  sare  watoto na  kuchangia  chakula  cha mchana  shuleni .

Alisema  serikali  ya  awamu ya  tano  inayoongozwa na Rais  Dkt  Magufuli  ni  serikali  yenye  mapenzi  mema na  wananchi  wake na  hivyo  hatua ya  kufuta michango  mbali mbali mashuleni  na kufuta  ada  ni  kutaka  watoto  wote  kusoma   hivyo ni lazima  wazazi  kwa  nafasi zao  kuendelea  kuchangia  mahitaji  muhimu  kwa  watoto  wao kama sare na chakula na  kama  kuna  mchango  wa maendeleo ya  shule  michango   hiyo  ikusanywe bila  kuwahusissha  walimu .

Pia  kiongozi  huyo  alisema  mwenge  wa  Mwaka  huu  haufungui  miradi  isiyo na  ubora  na  kuwa  miradi  inayofunguliwa ni ile  iliyojengwa kwa  ubora  na ndio  sababu ya   agoma kuzindua mradi wa barabara katika halmashauri ya Mji Mafinga baada ya kujengwa chini ya kiwango.

Kiongozi huyo aligoma kuzindua barabara hiyo inayojengwa kati ya Changarawe -matanana na Kisada yenye urefu wa kilomita 15 iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya shilingi milioni  331.6 na kampuni ya Gilco (2000)company Ltd chini ya usimamizi wa Mhandisi wa Tarura halmashauri ya mji Mafinga.

Akitoa maagizo  kwa  mkuu wa wilaya ya  Mufindi  Wiliam Jamhuri ,kiongozi huyo wa  mbio za Mwenge  alimtaka  mkuu wa  wilaya kusimamia  matengenezo mapya ya  barabara   hiyo na yakikamilika basi  aizindue yeye  na  sio  mwenge kama  ilivyopagwa na  baada ya  kuzindua atoa taarifa  kwake .

pamoja na kuukataa mradi  huo  pia kiongozi  huyo alitoa  muda  wa  wiki mbili   kwa  Taasisi ya  kuzuia na kupambana na  Rushwa ( TAKUKURU ) kuchunguza  mradi wa  barabara ya  kiwango cha lami ya  Samora  ,Mashine tatu  Mkwawa  katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa   yenye  urefu wa Kilomita  3.4 iliyojengwa kwa  kiasi cha  zaidi ya shilingi Bilioni 5.3  huku akitilia  shaka mradi wa maji Halmashauri Mji Mafinga .

 kiongozi  huyo  aliiagiza  vyombo  vinavyohusika ikiwemo Takukuru  ndani ya  wiki mbili   kuanzia jana  kutuma  taarifa ya  uchunguzi wa pesa zilizolipwea kwa mkrandarasi  wa  barabara   hiyo pamoja na vielelezo  vyote .

Kwani alisema  pamoja na mradi  huo  kujengwa kwa kiwango  kinachofaa  ila ana hofu ya  pesa zilizoptumika katika  ujenzi  huo  hivyo lazima uchunguzwe na taarifa  azipate kwa  muda  huo na kama wapo  waliohusika na matumizi mabaya ya pesa  basi  waweze   kuwajibika.

Kuhusu Halmashauri ya mji Mafinga  pamoja na kupongeza  miradi  mbali mbali mbali ya kimaendeleo miradi 8 yenye  thamani  ya  shilingi bilioni 1.7 bado  kiongozi   huyo  alitaka  mradi  wa ujenzi  wa  darasa  shule ya  sekondari  Ihongole kufanyiwa  marekebisho  ya  haraka  huku  mradi wa ujenzi wa  tenk la maji  mtaa Tanganyika lililojengwa kwa shilingi milioni  407,658,553 kupatiwa vielelezo vya malipo ,vipimo  vya  udongo na  vingine.

"  Sijaukataa mradi  wenu  nimeukubali na umejengwa  vizuri ila nataka  tu nijiridhishe  na matumizi ya  pesa  zilizotumika na kama  kuna mtu amehusika  kula  pesa  basi  hatua  kali  zichukuliwe dhidi yake”
Alisema  kuwa  suala la  ujenzi  wa  miradi linapaswa  kuzingatia  ubora  na  matumizi   sahihi ya  pesa  na  kuwa  wakimbiza  mwenge wa  safari hii  wamejidhatiti kwa kuwa  na  wataalam wa miradi  na watalamu  wa  tathimini ya  miradi na ndio  sababu  wamekuja na  kila aina ya  vifaa vya kukagulia  miradi  hiyo kama sululu  na vifaa vingine .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE