May 25, 2018

WANANCHI HALMASHAURI YA IRINGA WACHANGIA TSH MILIONI 169 MIRADI 9 YA KIMAENDELEO ,KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA KUENDELEA KUTUNZA MIRADI


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika mwenge wa Uhuru
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Masunya akiwa na mwenge wa uhuru
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William Kushoto akimkabidhi mwenge Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katika kijiji cha Muwimbi
Vijana wa alaiki waliopamba mwenge Iringa vijijini


Watumishi Iringa wakiulaki Mwenge
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Stevin Mhapa akiwa amesika mwenge

WANANCHI wa Halmashauri ya Iringa mkoani Iringa wamechanga jumla ya siblingi 169,098,400 kwa ajili ya kukamilisha miradi  9 ya kimaendeleo.

Akitoa taarifa  wakati wa uzinduzi na ufunguzi wa miradi hii leo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ,mkurugenzi wa Halmashauri ya  Iringa Robert Masunya  alisema kuwa pamoja wananchi hao kuchangia pesa hizo serikali kuu imechangia  kiasi cha shilingi 844,383,900.

Wakati Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imechangia 36,173,219  huku wahisani wamechangia shilingi 14,200,000 na kufanya jumla ya michango yote kufikia shilingi 1,063,855,519.

Masunya alisema kuwa miradi iliyochangiwa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati kijiji cha Muwimbi ambayo wananchi wamechangia shilingi 44,803,900.

Huku Halmashauri ikichangia shilingi 5,827,100 ,wahisani shilingi 12,500,000 ,ukarabati wa barabara ya Masumbo -Kiponzero ambayo imekarabatiwa kwa pesa za serikali kuu kwa kiasi cha shilingi 277,611,900 na ujenzi wa shule ya sekondari Tanangozi iliyojengwa kwa shilingi 58,774,500  ambayo wananchi wamechangia shilingi 49,244,500 na serikali kuu imetoa shilingi 9,530,000.

Aidha alitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na mradi ujenzi wa Zahanati ya Mlangali iliyojengwa kwa shilingi 59,486,119 pesa ambazo zimetokana na wahisani kiasi cha shilingi 1,200,000 ,Halmashauri imechangia shilingi 21,786,119 na wananchi shilingi 36,500,000.

Pia alisema wananchi wa Halmashauri ya Iringa wamechangia shilingi 4,435,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja ya walimu na matundu 5 ya vyoo katika shule ya sekondari Kiwere na serikali kuu imechangia mradi huo shilingi 65,500,000 na kufanya pesa zote kufikia 69,935,000 .

Alitaja miradi mingine iliyofunguliwa na mwenge kuwa ni pamoja na shamba la korosho  kwa taasisi za Halmashauri kwenye shule ya sekondari Ismani ambalo limegharimu kiasi cha shilingi23,137,000 kwa wananchi kuchangia shilingi 17,395,000 na serikali kuu ikichangia 5,742,000.

Hata hivyo alisema mbio hizo za mwenge zimeweza kuzindua mradi wa maji kijiji cha Kising'a mradi wenye thamani ya shilingi 346,080,000  pesa zilizotokana na michango ya wananchi ikiwa ni 6,720,000 ,Halmashauri shilingi 3,360,000 na serikali kuu ni shilingi 336,000,000.

Alipongeza pia wananchi kwa kuchangia shilingi 10,000,000 kati ya shilingi  165,000,000 zilizotumika kwenye ujenzi wa bweni la wasichana shule ya sekondari Ismani ambapo Halmashauri ilichangia shilingi 5,000,000 na serikali kuu ikichangia shilingi 150,000,000.


Aidha Masunya  alisema kwa mwaka huu 2018 mbio za mwenge wa Uhuru katika miradi yote 9 wananchi wamechangia jumla ya shilingi 169,098,400 na Halmashauri imechangia shilingi 36,173,219 ,serikali kuu imechangia shilingi 844,383,900 huku wahisani wakichangia shilingi 14,200,000.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa ,kabeho alitaka wananchi kuendelea kushiriki kuchangia miradi yote ya kielimu ambayo itawalazimu kufanya hivyo.

Alisema pamoja na kushiriki kuchangia miradi walimu wakuu hawaruhusiwi kufukuza watoto shule kwa michango ambayo wazazi na wananchi wamekubaliana nao kupitia kamati za maendeleo za kata .

Alisema jukumu la mzazi kuhakikisha ananunua sare za wanafunzi pamoja na kuchangia Chakula shuleni ila michango yote na ada serikali ya awamu ya tano imeifuta mashuleni

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE