May 17, 2018

MAOFISA UGANI MIKOA 9 TAZANIA KUTUMIA SIMU JANJA KUFIKISHA TAFITI KWA WAKULIMA

Add caption

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  katikati  waliokaa pamoja na mkuu wa  wilaya ya  Iringa   Richard Kasesela  kulia kwake  wakiwa na watafiti wa udongo kutoka  mikoa mbali mbali  nchini  leo katika  Hotel ya Iringa Sun Set
Watafiti  wakiwa katika warsha  hiyo leo 


Watafiti  wakimsikiliza mkuu wa  mkoa wa Iringa 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina |Masenza  akifungua  warsha  ya  watafiti wa udongo 

WATAFITI  wa udongo kusini mwa  jangwa la Sahara kuja na mbinu mpya ya kuwawezesha maofisa ugani  kutumia simu janja (smartpohone ) kwa ajili ya kuwafikishia matokeo ya utafiti wakulima ili kutumia mbolea, mbegu na kuweza kukadiria mimea sahihi kwa eneo yao .


  Hatua   hiyo  imekuja ili kurahisisha ufikishaji wa matokeo ya utafiti na kubadilishana taarifa zinazomuwezesha mkulima kulima kisasa na kupata tija.

Akifungua   warsha  ya siku  moja ya wadau wa  kuongeza  tija ya  zao la mahindi na utafiti wa  udongo  kusini mwa jangwa  la  sahara (Africa)iliyofanyika   katika  ukumbi wa Hotel ya  Sun Set Gangilonga mjini Iringa   Leo  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema hatua  hiyo ni  kubwa na itaongeza  uzalishaji kwa  wakulima.
 
“Napenda kuwapongeza kwa kuweza kutekeleza sera ya kilimo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao na hususani zao la mahindi kwa kutumia teknolojia za matumizi sahihi ya mbolea, mbegu bora na idadi ya mimea kwa eneo ili kuongeza uzalishaji na kufikia azma ya uchumi wa kati wa viwanda. Nimetaarifiwa kuwa umefanyika utafiti wa awali juu ya matumizi”

Masenza alisema  kuwa Tanzania ni nchi inayotegemea kilimo na  mkoa  wa Iringa ni miongoni mwa mikoa inayotegemewa asilimia 85 ni wakulima wadogo wadogo wanaotumia jembe la mkono na teknolojia duni.

“Nimetaarifiwa kuwa mradi mmoja wapo unaoitwa ‘Taking Maize Agronomy to Scale in Africa’ (TAMASA) unatekelezwa katika mikoa 9 ambayo ni Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Aidha, mradi huu unatekelezwa katika wilaya 25 kuwa  ni jambo la faraja sana katika nchi  katika awamu hii ya tano ya serikali inayoongozwa na Rais,  Dkt. John Magufuli ambaye  anataka  kuona uboreshaji  bora  na  wenye  tija katika  kilimo kwa  wakulima nchini .

“katika kufikia kilimo chenye tija. Tuzingatie idadi sahihi ya mimea katika eneo kama Swala la afya ya udongo na mbegu bora ni muhimu wanavyoshauri wataalam”

Mkuu  huyo wa mkoa  alisema  kuwa mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa inayotegemewa na taifa (ghala la taifa kwa chakula) katika uzalishaji wa mahindi.
Hivyo alisema ujio wa technolojia hizi ni muhimu sana katika mkoa .

“ Ni mategemeo yangu kuwa matokeo ya utafiti huu wa matumizi sahihi ya mbolea na mbegu bora utawafikia wakulima wengi zaidi nchini ili waweze kulima na kupata tija hii  ndiyo dhamira ya Serikali yetu ambayo imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha utaalamu wa kilimo cha kisasa unawafikia wakulima wengi nchini na  itapendeza  mkoa  wa Iringa uwe  kitovu cha  tafiti mbali mbali”

Alisema kuwa Suala la mabadiliko ya tabia ya nchi limekuwa kikwazo katika uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Hivyo mbinu sahihi zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni muhimu. Zaidi .

 “Nimetaarifiwa kuwa utafiti huu umezingatia kuongeza tija katika kilimo cha mahindi, wakati huohuo bila kuathiri mazingira”.
“Napenda kutoa shukrani zangu kwa makampuni na taasisi zote za kitaifa na kimataifa zilizoshiriki kuandaa nyenzo hizi ikiwemo  Serikali ya Tanzania kupitia Vituo vya utafiti vya (Ironga, Seliani, Uyole na Chuo Kikuu cha Sokoine), YARA, CIMMYT, Shirika la utafiti wa Ngano na Mahindi (CIMMYT), Utafititi wa mabadiliko ya tabia ya nchi na usalama wa chakula (CCAFS), Global yield Cap Atlas, Ushirika wa  kimataifa wa mbolea (ifa), Mfuko Bill na Melinda Gates”
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE