May 9, 2018

TAARIFA TOKA TFF LEO JUMATANO MEI 9

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 9, 2018

Msimu wa Ligi wa 2017/2018 kwa mujibu wa Kalenda ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) unamalizika Mei 31, 2018.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambao ndiyo waendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) tunatoa pongezi kwa timu ambazo zimefanikiwa kupanda daraja.

Kwa upande wa FDL zilizopanda kwenda VPL msimu wa 2018/2019 kulingana na msimamo wa mwisho wa Ligi hiyo ni; Kundi A ni JKT Tanzania FC ya Dar es Salaam na African Lyon ya Dar es Salaam.

Kundi B ni Kinondoni Municipal Council FC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga wakati Kundi C ni Biashara United FC ya Musoma na Alliance Schools FC ya Mwanza.

Kwa upande wa SDL zilizopanda kwenda FDL msimu wa 2018/2019 ni timu nne zilizoongoza makundi pamoja na washindwa bora (best looser) watatu. Kundi A ni Reha FC ya Dar es Salaam, Kundi B ni Arusha FC ya Arusha, Green Warriors ya Dar es Salaam, na Mashujaa FC ya Kigoma.

Washindwa bora ni Namungo FC ya Lindi,  Pepsi FC ya Dar es Salaam, na Boma FC ya Kyela, Mbeya.

IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA   

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE