May 3, 2018

SILVERLENDS HONGERENI KWA UWEKEZAJI LAKINI TULIPENI KODI YETU - RAIS DKT MAGUFULI

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa leoRais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT Bw. Geoffrey Kirenga alipowasili katika kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa kabla ya kukizindua rasmi katikati ni  mbunge wa Kalenga  Geofrey  Mgimwa 


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa,kulia  kwake ni mke wa Rais Janet  Magufuli na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi 
 

                                    Rais Dkt Magufuli akitazama  vifaranga  vya  kuku  vya  siku  mmoja  

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Msenza alipowasili eneo la Ihema kuzindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na kulia kwa Rais ni Mama Janeth Magufuli
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Balozi wa Denmark nchini Mhe. Camilla Christensen na viongozi wengine wakizindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga eneo la Ihema mkoani Iringa leo Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Balozi wa Denmark nchini Mhe. Camilla Christensen na viongozi wengine wakizindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga eneo la Ihema mkoani Iringa kutoka  kushoto ni mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Rose  Tweve, MNEC Iringa  Salim Asas , waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi, mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza, mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati,mbunge wa Kalenga Geofrey Mgimwa  na mawaziri  pamoja na mbunge wa Mafinga Cosato Chumi  wa tatu  kulia kwa Rais picha na Matukiodaima na Ikulu


...............................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog 
 
RAIS  Dkt  John  Magufuli ameipongeza   kiwanda  cha Silverlends Tanzania  LTD  ya  mkoani  Iringa ambayo  inazalisha  vyakula  vya  mifugo  na  kuku kwa  kutoa  ajira kwa  watanzania 938 katika kampuni  hiyo na  kuitaka kuanza  kulipa   kodi  inayotokana na  faida  inayopatikana katika  uwekezaji  wake.

Alisema  kuwa makampuni  mengi yamekuwa  yakija  kuwekeza nchini na baada ya  miaka  mitano  ya   uwekezaji utayasikia  yanadai  kuwa  hayajapata  faida  na  yanaweza  kuendelea na  uwekezaji hata   miaka  10  bila  kulipa kodi  inayotokana na faida  kwa  madai  yamepata  hasara.

"  Sasa kama kampuni  miaka 10  linapata  hasara na bado   linaendelea  kuwekeza  nchini  na  kampuni haifungwi  kama  yanapata  hasara  kwanini hafungi huu ni ujanja  ambao  unatumiwa na  baadhi ya wawekezaji kukwepa  kulipa  kodi  itokanayo na faida  wanayoipata  nataka  faida  mnayoipata  hapa  tulipeni  kodi  yetu "

Rais Dkt  Magufuli  aliyasema hayo  leo  wakati  akiwahutubia  wananchi wa  kijiji cha Ihemi wilaya ya  Iringa wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha  Silverlends Tanzania  LTD  pamoja  na  ufunguzi wa barabara  ya Iyovi  ,Iringa na  Mafinga  yenye  urefu  wa  kilomita 218.6 iliyojengwa  kwa mkopo kutoka  nchi  ya  Denmark  kwa zaidi  ya shilingi bilioni 283.715.

Alisema  kuwa  serikali imejipanga  kuhamasisha  uwekezaji wa  viwanda  vyenye  tija  vitakavyowezesha  watanzania  wengi kunufaika na  viwanda  hivyo  ambavyo pia  vitatumia  Teknolojia  rahisi  kwa watanzania  pamoja na kununua malighafi  zinazozalishwa na  watanzania .

Hivyo  alisema  amependezwa na uwekezaji wa  Slivalends  na   jinsi ajira  zilivyotolewa kwa  wingi kwa  wananchi  wanaozunguka  kampuni  hiyo  na  kuwa kasi  hiyo  ya uwekezaji ni nzuri  na  serikali yake  inaunga  mkono  na inapongeza uwekezaji  huo ambao umekuwa na  tija kubwa .

Rais  Dkt  Magufuli  alisema  kwa  ajili ya  kuwavutia  wawekezaji  wengi  zaidi kufika  kuwekeza  nchini  ni vema  makampuni ya  uwekezaji nchini  kuhakikisha  wanatangaza faida wanazopata  kwa  uwekezaji  ili  kuvutia  wengine  kuja  kuwekeza  kuliko  kuendelea  kudai kuwa  wamepata  hasara  jambo  ambalo   halitawavutia wengine  kuja  kuwekeza .

Alisema  serikali ya  awamu ya tano  imeweka  mkakati  wa  kujenga  miundo  mbinu ya reli  ,anga  na barabara  ili kuwavutia  wawekezaji  wengi zaidi na  kuwaondolea  vikwazo  vya  usafirishaji bidhaa  zao  wanazozalisha .

Kwani  alisema  suala la uboreshaji wa  miundo  mbinu  linahitajika  katika  safari ya kuelekea  uwekezaji  wa viwanda na  kuwa serikali imejipanga kuboresha  mazingira  mazuri ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuendelea  kusogeza  umeme  na miundo  mbinu  bora .

Hata   hivyo  Rais  Dkt  Magufuli alipongeza  jitihada  kubwa zinazofanywa na uongozi wa  mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa  mkoa huo  Amina Masenza kwa  kuendelea  kusimamia  na  kuhamasisha  uanzishwaji  wa viwanda na  kuufanya mkoa  wa Iringa  kuwa na  viwanda 2663.

Kuhusu  ushirikiano kati ya wananchi na kampuni   ya  Silverlends Tanzania  LTD  ,Rais Dkt  Magufuli  alipongeza kuona kuna ushirikiano mzuri na kuwepo kwa mkakati wa  kuendelea  kushirikiana na  wananchi katika  uzalishaji .

Aidha  alisema jambo la  kujivunia na kupongeza Slvalends  ni  kuona  asilimia 80 ya  malighafi   inayotumika  kiwandani  hapo  inazalishwa hapo  hapo .

"  Wakati  tunaingia madarakani mwaka 2015  moja ya  ahadi  yetu  ilikuwa ni kujenga  uchumi  wa viwanda kwa  kuanzisha viwanda  vyenye kuajiri  watanzania na  vitakavyonunua  malighafi  zinazozalishwa  humu nchini  pia viwe na  Teknolojia  rahisi kwa watanzania "


Awali  mwakilishi wa  Silverlends Beny Mosha  alisema  kuwa  kiwanda  hicho  cha kutengeneza vyakula  vya mifugo na   uzalishaji wa  vifaranga  vya kuku  kimewekeza kiasi cha  shilingi bilioni 15.6 na  kimeweza  kutoa ajira kwa wafanyakazi 938 kati yao  wafanyakazi 15 pekee ni wageni ambao hata  hivyo jitihada za  kuwafundisha  wazawa  kupata  ujuzi wa  nafasi  hizo zinafanyika  ili nafasi zao  zichukuliwe na  wazawa .

Kuwa kiwanda kina uwezo wa  kuzalisha tani 40,000 za  chakula  cha  mifugo kwa  saa moja  na  lengo  likiwa ni  kuja kuzalisha tani 47,000 kwa mwaka  na  kuwa  kwa upande wa vifaranga  vya  kuku  wanavyozalisha huuzwa katika nchi mbali mbali kama Uganda , Nigeria na  Kenya .

Pia  alisema  wametoa  mafunzo ya ufugaji kuku kwa  wananchi ambao ni  wafugaji wadogo kwa wafugaji 895 toka  walipoanzisha ufugaji  wa  kuku katika kiwanda  hicho .

Katika hatua  nyingine Rais Dkt Magufuli  amemuomba  naibu  balozi  wa Denmark nchini Camilla Christensen  kusaidia ujenzi wa barabara  ya  mchepuko  kutoka Ipogolo  hadi  chuo cha  Iringa  yenye urefu wa Kilomita 11 ili kupunguza msongamano wa  magari hasa malori  katika mji wa Iringa ambao umepitiwa na barabara ya Afrika  kusini na Cairo .

Rais  Dkt  Magufuli  alisema serikali yake  ipo tayari hata kama itakopeshwa  leo  ili  barabara  hiyo iwezekujengwa ama naibu balozi  huyo anaweza  kujitolea  kujenga kwa msaada maana kama  nchi  yake  imeweza  kujenga  barabara  ya Iyovi , Iringa na Mafinga  yenye  urefu wa Kilomita 218.6  haitaweza  kushindwa  kujenga kipande  hicho cha  kuchepusha malori yasiingie  katikati ya mji wa Iringa .

Aidha  aliwataka  wananchi kuendelea  kutunza barabara  na  kuepuka  kuharibu ama  kutoa alama  za barabarani huku akiwataka madereva  kuzingatia  sheria  za  usalama barabarani na kuepuka  kumwaga  oili ovyo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE