May 10, 2018

SERIKALI MKOA WA IRINGA YAPONGEZA VYOMBO VYA HABARI

Mmiliki  wa  mtandao  wa matukio  daima Francis  Godwin (mzee  wa matukio) akipokea  cheti cha  pongezi  kwa kazi kubwa  ya  kutangaza mkoa  wa Iringa  wakati wa Mei  mosi  toka kwa  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Mwandishi wa Mtanzania  mkoa  wa  Iringa  Raymond  Minja  akipokea cheti  cha  shukrani ya  ushiriki  mzuri  wa sherehe za  Mei  Mosi toka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Mwakilishi  wa Nipashe mkoa wa Iringa  George  Tarimo  akipokea  cheti
Mwakilishi wa UHURU Iringa  Ester Malibiche  akipokea  cheti
Mwakilishi  wa TV  ONE Mohamed  Nyaulingo akipokea  cheti
Mwakilishi wa Tanzania  Daima Denis  Mlowe  akipewa  cheti na  mkuu wa  mkoa wa  Iringa
Mwakilishi  wa Blog  ya  Mwangaza wa Habari  akipokea  cheti
Mwakilishi wa Mwananchi Beldina akipokea cheti
Mwakilishi  wa EBONY  FM akipokea  cheti
Mwakilishi wa Azam TV akipokea  cheti
Mwakilishi wa  Radio  Furaha  FM  Tukuswiga  Mwaisumbe  akipokea  cheti 
Mwakilishi wa ITV Iringa  akipokea  cheti
Mwakilishi wa CLouds TV akipokea  cheti
Mwakilishi wa Chanel  Ten Clement  Sanga  akipewa  cheti
SERIKALI ya  mkoa wa Iringa  imepongeza vyombo  mbali mbali vya habari vya  mkoa wa Iringa na nchi ya  mkoa kwa kazi nzuri ya  kuhabarisha  umma wakati wa sherehe za  wafanyakazi duniani (MEI MOSI)  zilizofanyika  kitaifa  katika uwanja wa Samora  mjini Iringa .

Akitoa  pongezi  hizo leo  ofisini kwake   mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa amefurahishwa na kazi  kubwa ya  vyombo vya habari mkoa wa Iringa  chini ya Mwamvuli wa chama cha waandishi wa habari  mkoa wa Iringa (IPC) kwa  kufanya kazi  hiyo kubwa .

Alisema  idadi kubwa ya watu  waliofika  katika uwanja wa Samora  kujumuika na  Rais  Dkt  John Magufuli kwenye  sherehe  hizo ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa  na vyombo hivyo  vya habari  ikiwemo  mitandao ya kijamii kama  Blogu   ya  matukio Daima, Fullshangwe , Mwangaza  wa Habari  Bongo  Leaks na nyingine  nyingi .

Pamoja na  mitandao  ya  kijamii  pia  alipongeza  vyombo  vya utangazaji  mkoa  wa Iringa na  nje ya  mkoa kama Nuru  Fm , Country Fm , Ebony  FM ,  Furaha  Fm , Overcomers  FM , Qbla Teni ,  Furaha Fm , Bomba  FM , Radio Maria  FM  na  radio nyingine nyingi .

Pia  TV ambavyo  ziliungana na  blogu na Radio  kupewa  pongezi za  vyeti  vya  shukrani  ni  pamoja na  ITV , Star  TV , Cloud  TV,  TV One , TBC  ,  Chanel  Ten  na nyingine .

Huku upande  wa magazeti  ni pamoja na  gazeti  la Mtanzania ,  Uhuru, Nipashe , Tanzania  Daima, Mwananchi  na  mengine  mengi 


Hivyo  aliomba  ushirikiano  huo  wa vyombo  vya habari  kuendelea  zaidi

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE