May 31, 2018

RC MASENZA AWAONYA MAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI , KUWA WAKIHARIBU HAKUNA KUPEWA KAZI TENA

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  (kulia)  akimtua  ndoo  ya maji  mwanamke  mkazi  wa  Kidabaga  wilaya ya  Kilolo  wakati wa  ziara  yake ya  kukagua  miradi ya  maji  Kilolo
wakuu  wa Idara  Kilolo  wakimpokea  mkuu wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  ,kushoto  kwake ni mkuu wa wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah 
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  akipokelewa  na  wakuu wa  Idara  Kilolo  wakati wa ziara  yake ya  kukagua  miradi ya  maji wilayani  Kilolo  ,kushoto  kwake ni mkurugenzi wa Halmashauri ya  Kilolo Aloyce Kwezi
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akiukaribisha ugeni wa  mkoa  wilaya ya  Kilolo  kutoka  kushoto ni katibu tawala  wa  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayub na  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  kulia  akimsikiliza kwa makini katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja  Ayub wakati  akifafanua  jambo  mbele ya  wakuu wa  idara  Kilolo
Wakuu  wa idara  Kilolo  wakiwa katika  kikao  na  mkuu wa mkoa  wa Iringa
Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza na  msafara  wake  wakikagua  mradi wa  maji unaojengwa kwa  ushirikiano na  WARIDI
Mkuu wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akichota  maji katika  mradi wa maji Kidabaga  Kilolo  mradi  unaojengwa  kwa  ushirikiano na  Waridi
Mradi  wa Maji  wa  Kidabaga  ukikaguliwa na mkuu  wa mkoa wa Iringa

Na MatukiodaimaBlog 

MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  amepiga marufuku  wakandarasi  wa  miradi mbali mbali  ikiwemo ya  maji kupewa  kazi  kwenye  Halmashauri  iwapo  wajenga  chini ya  kiwango miradi ya  awali  waliyopewa .

Akitoa  agizo hilo jana  wakati wa  ukaguzi wa  miradi ya  maji katika  wilaya ya  Kilolo ,mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema  lengo la  serikali ya  mkoa ni  kuona   wakandarasi  wa ndani ya  mkoa wanapewa  kipaumbele  pindi  tenda  zinapotangazwa  katika Halmashauri  hiyo  ila  iwapo  watapewa kazi na  kushindwa  kufanya kwa  ubora  basi  wasitegemee tena kufanya kazi katika mkoa wa  Iringa .

“ Naomba  sana  wakandarasi  ambao  mnapewa  kazi mbali mbali  zikiwemo  za miradi ya  maji ndani ya Halmashauri  za  mkoa wa Iringa fanyeni kazi kwa  ufanisi mkijenga  miradi  chini ya  kiwango  mtawajibika kisheria  na  pia itakuwa ni  mwanzo na mwisho  kupewa  kazi ndani ya  mkoa wa Iringa”

Mkuu   huyo wa  mkoa alitaka  pia  wahandisi   katika  Halmashauri  zote  pindi atakapoendelea  kupita  kukagua  miradi ya  maji na miradi  mingine  kuhakikisha  wanakuwa na vithibitisho  vya kazi  iliyofanyika na malipo  yaliyotolewa  kwani wakati wa hadhidhi  na maneno   matupu  kwa  sasa hatataka kusikia  na  kuwa  kupitia   kiongozi  wa  mbio za  mwenge wa  uhuru mwaka  huu Charlesy  Kabeho iwe ni  elimu endelevu  kwa  wasimamizi wa  miradi  yote .

Aidha  Masenza  alisema  kuwa kazi nzuri imefanyika  kupitia miradi ya maji  inayoendelea  katika  wilaya za  mkoa  wa Iringa  kupitia  serikali ya Tanzania na shirika  la  maendeleo  la Kimarekani ( USAID) kupitia mradi  wake wa WARIDI  kuwa utaratibu unaotumiwa na  WARIDI wa  kununua  vifaa vya  ujenzi wa  miradi  kutoka  kiwandani  ni  mzuri  na  unapaswa   kuigwa na Halmashauri badala ya  kumpa kazi  yote  mkandarasi ikiwemo ya  kununua  vifaa vya  ujenzi ni  vizuri  Halmashauri  kwenda  kiwandani   kununua  vifaa vya  ujenzi na  wakandarasi  wao kulipwa   fedha za  ufundi  pekee.

“ Ukipitai  miradi  inayojengwa kwa  ushirikiano wa  WARIDI  ni  miradi  bora  na ya gharama  nafuu  ukilinganisha na  miradi  inayosimamiwa na Halmashauri  kupitia  wakandarasi  hao ambao  wanakuja na  vifaa vyao nashauri  kuangalia  namna ya ufanyaji kazi wa  WARIDI   ili  kuwa na  miradi  bora  kwa  gharama nafuu “

Hata   hivyo   alitaka  wananchi  kuepuka  kuharibu  vyanzo  vya maji  katika maeneo ya  miradi kwani  iwapo  vyanzo hivyo  vya maji  vitaharibiwa  miradi hiyo  itakufa .

“ Naagiza mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Kilolo  kuwaagiza madiwani  kusimamia  chanzo cha maji Mgombezi  na Ihimbo  pamoja na  vyanzo  vyote  kutunzwa  pia  mkuu wa  wilaya  naomba  hili  usimamie “

Katika   taarifa  ya  miradi ya maji Kilolo ya mkurugenzi  wa Halmashauri   hiyo Aloyce  Kwezi  alisema  kuwa  Halmashauri  hiyo  imefanikiwa kutekeleza  ilani ya  uchaguzi  kwa  kuendelea  kusogeza  huduma za maji  vijijini kama  agizo la   Rais Dkt  John Magufuli  kutoka aslimia 58    mwaka 2013 hadi kufikia  asilimia 72  April 2018  kuona wananchi  wanapata  huduma ya maji  safi na  salama .

Alisema   utekelezaji wa  Programu  ya  awamu ya  pili  wilaya ya  Kilolo imeanza miradi ya maji  Lundamatwe ,Kitelewasi  na  Ihimbo  kwa  upande wa maji  vijijini  na  miradi  mikubwa ya  maji ya  Ilula na Kilolo  mjini  kwa  upande wa  huduma  ya maji  mijini  na  kuwa  utekelezaji wa  miradi hiyo  upo hatua mbali mbali na  upo  uwezekano mkubwa wa kufikia  asilimia 85 ifikapo  mwaka  2020 kama  agizo la  serikali ya  awamu ya  tano.


“ Mradi  wa maji wa  Lundamatwe na  Kitelewaji  unajengwa na mkandarasi Fesa  Buildingi  and Civil Construction Company Ltd  kwa  gharama za shilingi 735,328,422  ,maradi wa Ihimbo  unajengwa na mkandarasi JITA  kwa  gharama za  shilingi 218,886,932 kwa  muda wa miezi sita pia “

Aliitaja  miradi  inayofadhiliwa na  WARIDI  kuwa ni  miradi iliyopo  vijiji  vitano  inayojengwa kwa shilingi 1,517,540,000 na  vijiji  hivyo ni pamoja na Kilolo, Kidabaga, Nguruwe, Ihimbo na  Irindi   .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE