May 9, 2018

RC MASENZA AAGIZA WALIOSHINDWA KULIPA MADENI YA USHIRIKA WAKAMATWE KWA UHUJUMU UCHUMI

Image result for RC  MasenzaMKUU  wa  mkoa  wa  Iringa Amina  Masenza ameagiza  wale wote waliokopa katika  vyama  vya  ushirika  vya  kuweka  na  kukopa (SACCOS)  kulipa madeni  yao  kabla ya  kukamatwa na kufunguliwa  kesi  za uhujumu  uchumi .

 Alisema  pamoja na  kuwa  sheria  za  ushirika  zimekuwa  ni  sheria  za kubembeleza mdaiwa  kulipa  deni lake  huku vyama  vya  ushiriki  vikiyumba  sasa  umefika  wakati wa sheria   hiyo  kufanyiwa  marekebisho  na ili pesa  za ushiriki ziweze kurejeshwa lazima  wote waliokopeshwa na  kushindwa  kulipa madeni  yao  kusakwa na  kufikishwa mahakamani .

Mkuu  huyo  wa  mkoa  alitoa  kauli  hiyo jana katika  ukumbi wa siasa ni  kilimo mjini  Iringa  wakati  akifungua kongamano la  siku  moja la jukwaaa la  ushirika mkoa  wa  Iringa , kuwa  wanaushirika wenye mikopo kulipa madeni yao kwa wakati ilikuepukana na riba inayoendela kupanda.

“Natambua mchango wa Ushirika katika kaulimbiu ya ujenzi wa Viwanda  Kumekuwa na maendeleo mazuri ya uanzishwaji wa viwanda kadhaa kupitia vyama vya Ushirika. Mfano mzuri umeonyeshwa na Chama cha Ushirika cha Kilimo na masoko cha Pamoja Tunaweza Sadani kilichopo katika Halmashauri ya Mufindi Chama hicho kimeweza kuanzisha kiwanda cha kusindika unga na kuchuja alizeti”

 Alisema  kuwa  Kupitia mfano huu mzuri ulionyeshwa na chama hicho bado anasisitiza  wanaushirika kuendelea kushirikiana katika masuala mbali hata kwa kuunganisha nguvu za vyama zaidi ya kimoja kuiga mfano wa Pamoja Tunaweza Sadani AMCOS Ltd.

 Aidha alisema amepata  taarifa kuwa chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Iringa pia kina mpango wa kuanzisha Kiwanda cha kusaga unga .

 “Nachukua fursa hii kuwaataka wasimamizi wa ushirika huo kuhakikisha mpango huo unafanikiwa endapo tutafanikiwa kuanzisha kiwanda cha kusaga unga kupitia chama chetu Kikuu cha Ishirika cha Iringa tutakuwa tumewasaidia wakulima na wanaushirika kupata soko la kuuza mahindi yao na kuondokana na tatizo la ukosefu wa soko mkulima ataweza kuuza mazao yake kwa bei nzuri hivyo kumuwezesha kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza kilimo chake”

 Kuwa SACCOS ni kimbilio la mkulima au mjasiriamali mdogo ambaye hana dhamana za kuwekeza benki ili akopesheke kwani hutoa mikopo mara mbili au tatu kupitia Akiba za wanachama kwa riba ndogo ambayo wanaushirika wamekubaliana.

       Kuwa kinachotokea kwenye Vyama hivi wanachama wakishakopeshwa mikopo hawarejeshi tena mikopo ile waliyopewa, matokeo yake wanawaathiri wale ambao hawajakopa kwa kipindi hicho hivyo kukifanya chama kisimamishe huduma kwa sababu ya kukosa fedha za kuwakopesha wengine.

 “Hii wanaushirika ni hujuma na mimi katika Mkoa wangu sitakubali Vyama hivi vihujumiwe na wanachama wachache wenye nia mbaya aidha nasisitiza kwa vyama vya Akiba na Mikopo kuhakikisha kuwa wanachama  wanakuza mitaji yao ya ndani kwa kuwekeza akiba zao ili waweze kujikopesha kwa riba iliyonafuu”

 Hivyo aliwaagiza  wanachama wote wanaodaiwa na vyama vyao warejeshe mikopo yao haraka iwezekanavyo  na Wakurugenzi kusaidia  kusimamia ili wale wanachama waovu wachukuliwe hatua za uhujumu uchumi.

 Kwa  upande  wake  mrajisi  wa  vyama  vya  ushirika mkoa  wa Iringa  Robert George  alisema kuwa jumla ya vyama vya Ushirika 261  katika vyama hivyo vyama hai ni 176 na Vyama sinzia ni 85 vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) vipo 156 vina wanachama 52,448  ambao wamewekeza Hisa za shilingi 2,374,470,234 akiba shilingi 4,687,465,346 na amana shilingi  1,743,345,165.


 Alisema  kuwa SACCOS hizo zimeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi  25,127,637,497 kuwa Katika Vyama vya mazao na Masoko (AMCOS) kuna Vyama 78 jumla ya wanachama 7,906 na hisa zenye thamani ya shilingi 154,189,620,Vyama vya aina nyingine vipo 27ambavyo ni Chama cha Madini 1, Ufugaji 3, viwanda 4, Uvuvi 2, Upangishaji nyumba 1, Maduka 4, Umwagiliaji 4, Vyama vya Muungano 3, chama wapiga picha 1, Chama cha ufugaji nyuki 1, Chama cha wauza samaki 1, Chama cha Wapasua mbao 1 na Chama Kikuu 1.
MWISHO 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE