May 2, 2018

RAIS DRK MAGUFULI AAGIZA WALIOHUSIKA NA UFISADI WA UJENZI WA UKUMBI WA BILIONI 8.8 CHUO CHA MKWAWA WAKAMATWE

Image result for Mkuu  wa  chuo Mkwawa Prof Mushi

RAIS   Dkt  John Magufuli ameagiza  aliyekuwa  mkuu wa  chuo  kikuu  cha  Mkwawa mkoani  Iringa  Prof  Philimon   Mushi   na  mkandarasi  wa kampuni   Engineering  Service  Ltd ambaye  alihusika  na  ujenzi  wa ukumbi wa  bilioni  8.8  katika  chuo  hicho  kukamatwa  na  kufikishwa mahakamani  kwa kuwa  ujenzi  wake  umefanyika  kifisadi .

Akitoa  agizo  hilo leo  katika mkutano  wake  wa hadhara  chuoni hapo  alisema kuwa katika maisha  yake  huwa  hawekagi  jiwe la msingi  wala  kufungua mradi  uliojengwa  kifisadi kama  huo  hivyo  ndio maana  aligoma  kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa ukumbi .

“ Lakini  ni  ukweli  kuwa  chuo  kikuu  hiki cha mkwawa  kinanisukuma  sana na ndio  maana  sikuja kuweka  jiwe la Msingi katika ukumbi mnaojenga pale  siwekagi  mimi jiwe la Msingi wala kufungua  miradi ya  kifisadi na  ndio  lazima  tuwe  tunafika mahali  tuelezani ukweli  tu  haiwezekani  ukumbi huu Mkwawa  ujengwe  kwa bilioni  8.8  wakati   mabweni  yote ya chuo  kikuu  cha  Dar es Salaam  kinachochukua  wanafunzi 4000 yamemejengwa kwa shilingi  bilioni 10 “

Kuwa kuna Prof Mushi  aliyesimamia mradi huo bado  huyo  mtaa wakati  amefanya  ufisadi  huo  hivyo  atafutwe na  kupelekwa mahakamani  na  sio  kuwa maprofesa  hawatakiwi kwenda Mahakamani .

Huku  mkandarasi wa kwanza  aliyepewa  kazi  hiyo alilipwa  pesa  za kwanza  kinyume  na utaratibu wa  ukandarasi  kwani  mkandarasi hawezi  kulipwa  pesa kabla ya  kukabidhi  satifiketi ya kazi yake .
  Sasa nilitegemea   kwenye  chuo hicho cha wasomi kikawa  kikaweza  kusimamia  vizuri  matumizi sahihi ya  fedha  wanafunzi  wanateseka kwa  kukosa sehemu ya  kukaa kutokana na watu  waliokuwa  wakiwaongoza na mimi  najua hamuwezi  kushangilia kwa kuwa mnawaogopa  sasa naomba mshangilie  maana  wote  watakamatwa  ifike  sehemu  sisi  watanzania  tuwe na uchungu wa kodi zao “

                        Zaidi  soma gazeti la Mtanzania  Kesho  Alhamisi 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE