May 2, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AJIBU OMBI LA MBUNGE MWAMOTO BARABARA YA LAMI KUJENGWA KILOLO

RAIS  Dkt  John  Magufuli ameahidi  kujengwa  kwa  barabara  ya  lami  kutoka Ipogolo  hadi  Kilolo  yenye  urefu  wa  kilometa  33 kama  ahsante  yake  kwa  wananchi  wa Iringa  vijijini na  Kilolo  ambao pekee  walimdhamini  wakati wa mchakato  wa  kura za maoni baada ya  Iringa mjini  kukuta wagombea  wenzake  wamewanunua  wapiga  kura  wote .

“ Ninafahamu  kuwa  Kilolo mnahitaji  barabara  ya Lami na nafahamu  kuwa  barabara  hii mumeanza  kujenga  kidogo kidogo  toka  kipindi cha Prof Msolla  ama Mwamoto maana  hawa wanakawaida ya  kupokezana  ubunge ,nataka  kuwawaambia  ndugu  zangu  serikali  hii imejenga barabara nyingi  nataka  kuwaahidi  ndugu  zangu wa  hizi kilometa  zilizobaki  zitajengwa   kama  nilikuwa  nikisema na kutekeleza nikiwa  waziri  leo  ni Rais  nitashindwa  kujenga  tunaanza  ujenzi  huo na kwa kuwa mawaziri wangu mpo  hapa Lukuvi ,Jafo na Mwijage mkamwambie waziri wa  ujenzi Prof Mbalawa  kwa kushirikiana na Tanroard na Tarula barabara  hii ianze kujengwa kwa lami na mimi nitafuatilia na kama hii ndio  itakuwa ni  shida ya  Kilolo  nitashukuru  pamoja  na  kuwa  bajeti yake  haikutengwa ila  sote tunaamini  jungu  kuu halikosi  ukoko “

 Rais Dkt Magufuli alisema wakati  akielekea  Kilolo  alipoona  barabara  zimechongwa  alijua  kabisa  kuwa  hiyo ni  danganya  toto  na  wamefanya  hivyo kwa  ajili ya ziara  yake .

Rais Dkt  Magufuli  aliyasema hayo leo   wakati akiwahutubia  wananchi wa  Kilolo  baada ya  kuweka  jiwe la msingi katika  ujenzi wa  Hospitali ya wilaya  hiyo , kuwa anawashukuru sana  wananchi  waliomdhamini na hata  wasahau .

 Kuwa  alipofika  mkoani Iringa  wakati wa  mchakato wa  kutafuta  wadhamini  wa  kumdhamini ndani ya CCM  ili agombee  Urais  aliambiwa  Iringa mjini wadhamini  wote  wamenunuliwa na  alipotaka  kwenda  Jimbo la  Isimani  mbunge wa  Ismani  Wiliam  Lukuvi  alimweleza nako  wamenunuliwa na pia Tosamaganga jimbo la Kalenga  pia  wana CCM  walikuwa  wamenunuliwa .

Hivyo  alisema  alilazimika  kufunga  safari   kuelekea  wilaya ya  Kilolo na alipofika mpakani  mwa  Kilolo na Iringa  vijijini  Ndiwili  Sokoni  akiwa amesimama  wananchi  wa  hapo  walimfuata na  kumhakikishia  kuwa asubiri  atafutiwe  wadhamini  na  aliweza  kuwapata  wadhamini  wote  waliohitajika  kutoka   eneo la  Kilambo  Iringa  vijijini akiwa  anaelekea  Kilolo na hawakumuomba  hata  senti  tano  ya  kumdhamini .

  Hii nawakumbusha  wenzangu  wana  CCM  kuwa  rushwa  ni  mbaya na  Iringa  Rushwa  ilikuwa  juu ila nashukuru  mmeanza  kuwashugulikia  watu hao   Rushwa  inatuchelewesha  na  kuwanyima haki  hata  wale  wanaostahili   nataka  kuwakumbusha  wananchi  wa mkoa  wa Iringa  wadhamini  wangu  wote  wametoka  Kilolo  na ndio maana  nasema  Kilolo  siwezi  kuisahau “

Kuwa alipoelezwa na waziri  wa  Tamisemi  Suleman Jafo  kuwa  Hospitali ya  wilaya  ya  Kilolo imekwama kwa zaidi ya  miaka  mitano  haijapata   fedha  imesimama inahitaji  shilingi bilioni 4.2  niliagiza  pesa  hizo  zitolewa maana  Kilolo  si  wapenda  rushwa na  wachapakazi  hivyo  wnawahakikishia  wananchi  wote  wa  mkoa  wa Iringa na  watanzania  kuwa  sitawaangusha .

Alisema  kuwa  uongozi  si ufalme  bali ni  kuwatumikia  wananchi  hivyo ndio  maana  huwa anaomba  siku  zote  kuwaomba watanzania  kuendelea  kumuombea  ili asisahau  wajibu  wake na kutanguliza  kiburi katika  uongozi  wake .

  Ndio  maana  nilipoingia madarakani  nilianza  kufanya marekebisho  ya  kuwatumikia  wananchi kama  ni  serikali iwe ni ya  wananchi na kama ni chama  basi  kiwe  ni chama  cha wanachama  na  sio vinginevyo “

Akielezea  kuhusu  elimu  Rais  Dkt Magufuli  alisema  mambo  yote  ambayo   yaliahidiwa  yatatekelezwa na  kuwa  awali  kulikuwa na  changamoto  kubwa katika  elimu ya  watoto  kurudishwa  kwa  kukosa ada  na  serikali yake  ilipoingia madarakani iliamua  kufuta ada  na kutoa elimu bila malipo .

“ Watoto  wengine  walikuwa ni yatima  na  wengine  hawana  uwezo  hivyo  wakifika  shule  walikuwa wakirudishwa  nafahamu  kuwa suala  la  kutoa elimu  bure  halikubaliki  hata  kwa  wafadhili  ila  serikali yangu  ikaona  ngoja  ianze kwa  kutoa  shilingi bilioni 23.8  kila  mwezi  na  hizi  fedha  tukaamua  kuwa  tunapeleka mashuleni maana  tungesema  zipitie  kwa wakurugenzi  ndipo  ziende  shule  huenda zingefika  zimepungua “

Alisema  baada ya  kuanza  kwa  mpango  wa  elimu  bure kwa  mwaka mmoja  pekee  ongezeko la wanafunzi  liliongezeka kutoka watoto  milioni 1  hadi  milioni 2 kwa  kujiandikisha  shule .
Rais  Dkt  Magufuli  alisema  changamoto ya  elimu  ina historia  ndefu  kwani  enzi  za  baba wa Taifa  kwenye  miaka  ya  1974 kutokana na  shida ya walimu na  changamoto ya  walimu walianzisha  upe  kwa mwalimu kumaliza elimu ya  darasa la saba na kwenda  kufundisha  na  shule za  msingi  zilikuwa  hazifaulishi  hata  watoto  wawili .

Pia  alisema  changamoto  ya shule za sekondari  ilikuwa kubwa  na  kuwa elimu ya upe  ilifanya kazi  kubwa  na ilikuwa mipango ya baba wa Taifa  kwa wale  waliomaliza darasa la  saba  kwenda  kufundisha  wenzao  akaja Mwinyi  na Mkapa  waliendeleza  haya  baada ya  kukuta changamoto  hiyo  na amekuja  Kikwete awamu ya nne  akaanzisha  shule za  sekondari za kata  kwa  kila kata  kujenga  shule ya  sekondari  ambazo  zilizalisha  watoto  wengi  na kuongeza walimu  wengi na ndio maendeleo ya sasa  ambayo kwa  upande wake  ameendeleza hayo ambayo ni kazi nzuri ya  watangulizi  wake  na  sasa  serikali ya  awamu ya tano  imekuja na  elimu  bure .

“ Kwa  hiyo  tufike  sehemu  watanzania  tujipongeze  kwa  safari  hii  ndefu hadi hapa  tulipofikia  kuliko  kulaumu  bila  kujua  tumetoka  wapi   tumetoka mbali  tumefika mbali  na  tutaelekea  mbali”
Alisema kwa  sasa  sehemu kubwa ya  vyuo  nchini  zimejaza  wanafunzi  waliotokana na   shule za kata  na kwa sasa  serikali imetoa  mikopo kwa  wanafunzi 130,0000 mkopo wa bilioni  483  naomba  mzipongeze  serikali za awamu  zote kwa  kazi  hii.

Hata  hivyo  alizema  serikali  ya awamu ya  tano  imeendelea  kushughulikia  changamoto mbali mbali kama  miundo mbinu  ya barabara ,umeme ,maji  na nyingine  nyingi .

Akizungumzia  kuhusiana na  afya  alisema   kuwa kwanza anawapongeza wananchi wa Kilolo kwa  kuwa na mwelekeo mzuri wa kuwa na Hospitali hiyo na  anatambua  kuwa hata  mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto  siku za nyuma alikuwa akizungumzia  kero ya Hospitali  kuwa  hospitali   kutokana na  wilaya  hiyo kuwa na miundo  mbinu mibovu ya barabara .

  Kila  nikikutana na mbunge  wenu  Mwamoto kilio  kikubwa  alichokuwa akieleza ni Hospitali  kuwa unajua  mheshimiwa  miundo mbinu ya barabara  ya  Kilolo ni mibovu hivyo naomba  utusaidie  Hospitali  hii ikamilike  sikutegemea  kama leo  angeniambie  changamoto  ni  barabara  tena  ndio  maana  tunatafuta  shilingi bilioni 4.2  ili  Hospitali hii ikamilike na kuwa na kila  kitu”
Aidha  Rais  Dkt  Magufuli  aliagiza  wasimamizi wa Hospitali  hiyo  kukamilisha kwa  wakati na  serikali itatoa  pesa  zinazohitajika .

Alisema  kuwa  changamoto ya   afya  imekuwa ikichangia vifo  vya akina mama na watoto  na  hivyo  serikali  yake  imejipanga kuona  changamoto  hizo  zinatatuliwa kwani  kipaumbele  kwa  sasa ni  sekta ya  afya  huku  akiwataka  wananchi  kujiunga na mifuko ya  bima ya  afya kwa  wingi  kwani  ugonjwa haupigi  hodi kuwa na  bima ya  afya  ni uhakika kwao  kutibiwa  wakati  wowote .

Pia  Rais  Dkt Magufuli  alizitaka  Halmashauri  kuacha  kuwasumbua  wananchi  kwa  kuwalipiza  tozo  za  ushuru  ambao  umefutwa na  kutaka tozo  zote 87 zilizofutwa  kubandikwa maeneo ya  wazi  ili  wananchi  wajue .

Huku  akizitaka Halmashauri  kutumia mapato  yanayotokana na makusanyo ya  ndani  kutatua  changamoto za maji  katika  maeneo yao .

“ Pia  wabunge  mna pesa za  mifuko ya jimbo tumieni  fedha  hizo  kusaidia  kutatua  kero  za maji  hata kwa  kununua  mota za  kusukuma maji  japo  wabunge  wengi  huwa  hawataki  kuyasema haya”

Rais  Dkt Magufuli akiwa  njiani  kuelekea  Kilolo  wananchi wa  Kilambo ambako  walimdhamini walimsimamisha na  alitoa pesa taslimu kiasi cha shilingi  milioni 11 kwa  ajili ya ujenzi wa  vyumba  vya madarasa  shule ya msingi milioni 5 na ujenzi wa kituo cha afya milioni 5  na kiasi cha  shilingi milioni 1 kwa ajili ya  ukarabati  ofisi ya  CCM Kilambo .

Kuhusu  janga la  UKIMWI Rais Dkt Magufuli alisema anashangazwa na  kasi kubwa ya maambukizi ya  UKIMWI kwa mkoa wa Njombe na  Iringa  kuwa wakati  kitaifa  maambukizi ya  UKIMWI yakipungua kwa  mkoa wa Njombe unaongezeka kwa kuwa na  asilimia 11.6  na Iringa ni  asilimia 11.2

Akitoa taarifa  ya ujenzi wa Hospitali  hiyo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo  Aloyce  Kwezi  alisema  kuwa  wilaya  hiyo ina  jumla ya  vituo  vya  afya 62 ,Hospitali moja ya  inayomilikiwa na Kanisa la kiinjili la kilutheri  Tanzania (KKKT) vituo  vya afya  viwili   na  zahanati 59 na  kuwa  ili  Hospitali  ya  wilaya  ya  Kilolo  ujenzi wake  ukamilike  inahitaji  jumla ya  shilingi  bilioni 4.2 na kati ya  hizo tayari  serikali imetoa  shilingi  bilioni 2.28.

Kwa upande wake  waziri wa Tamisemi Suleman  Jafo  alisema  kuwa   kuna  Halmashauri 185  nchini na  toka    nchi  ipate  uhuru  kulikuwa na Hospitali  za  wilaya 77 pekee ila  kwa  sasa kwa  kipindi cha serikali ya awamu ya  tano  kuna ujenzi wa  Hospitali  za  wilaya  67  na  kuwa serikali hii imefanya  makubwa ambayo hayajapata  kufanyika toka nchi ipate  uhuru .
Kuwa vituo vya  afya  vilikuwa ni 115 toka  nchi ipate  uhuru  kwa sasa kwa  utawala  wa Rais Magufuli kuna  vituo vya afya  208.
Kwa upande wake  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  aliipongeza  serikali ya  awamu ya  tano  kwa kuupatia  mkoa wa Iringa kiasi cha shilingi bilioni 26 za miradi  mbali mbali ya  kimaendeleo.

Kwa upande  wake  mbunge wa  Kilolo, Mwamoto alimpongeza  Rais Dkt Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya maji katika mji wa Iringa kwa  kutoa pesa kiasi cha  shilingi  bilioni 5  kwa  ajili ya mradi wa maji Ilula huku  akiomba  kwa  tarafa ya Mahenge  kusaidia  miradi ya mabwawa  ya umwagiliaji  na  kumshukuru kwa kuahidi ujenzi wa barabara ya  lami  Ipogolo hadi  Kilolo.

Huku mbunge  wa  viti maalum  mkoa wa Iringa Ritta Kabati pamoja  na kumpongeza Rais  aliomba  kusaidiwa gari la  wagonjwa  kutokana na Jografia ya  wilaya  hiyo  pia  dawa  kwa  ajili ya usingizi katika Hospitali za  wilaya  hiyo .

Waziri wa Ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi  Wiliam Lukuvi akitoa  salam  zake mbele ya Rais  aliwataka  wananchi wa Kilolo  kuacha kuendelea  kuuza ardhi kwani  takwimu  zinaonyesha  wilaya  hiyo inaongoza kwa kasi ya uuzaji wa ardhi  tena  viongozi wa vijiji kuingilia  hadi mamlaka ya  Rais kwa kuuza ardhi zaidi ya ekari 700

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE