May 3, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AHAHIDI KUTEKELEZA MAOMBI YA MBUNGE RITTA KABATI

RAIS  Dkt  John  Magufuli  ameahidi   kuzifanyia  kazi changamoto  za  Hospitali ya  Manispaa ya  Iringa  pamoja  na  ile  ya  kutaka magereza  ya Iringa  kuhamishwa kupisha  upanuzi  wa Hospitali ya  rufaa ya  mkoa  wa  Irina kama  alivyoomba mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati (CCM).

Akizuingumza  katika  ziara yake mkoani  Iringa Rais  Dkt  Magufuli alisema  kuwa amezipokea  changamoto  hizo kama  alivyoombwa  kuzifanyia  kazi na mbunge  Kabati  na  kuwa atazifanyia  kazi  kwani  zina  tija  kubwa  kwa jamii ya  mkoa  wa Irina.
Alisema  kuwa  anawapenda  sana  wabunge  wa  mkoa wa Iringa kwa kazi  kubwa wanayoendelea  kuifanya  na  kuwa ataendelea  kuleta  kila  kitu  wanachokiomba  kwani  mkoa  wa Iringa anaupenda  sana na  ana historia  kubwa  kwa  kuwa  amepata  kusoma  katika  mkoa  wa  Iringa  sekondari  ya  Mkwawa .

“ Nimepokea  changamoto  hizo  za Hospitali ya rufaa ya mkoa  wa Iringa na juu ya  kupatiwa mashine katika  hospitali ya Frelimo nitazifanyia kazi  kwa kupitia kwa mawaziri  wa  wizara   husika  kwani hizi  hospitali  zote  mbili ni  muhimu  sana  si  tu  kwa  wakazi wa  mji  wa Iringa na mkoa  bali hata  kwa watumiaji wengine  wa barabara   hii ya kimataifa  ya  kutoka  Afrika  ya  kusini  hadi Cairo iliyofunguliwa 

Rais  Dkt  Magufuli  alisema  serikali  inaendelea  kuboresha   sekta ya  afya  na  kuwa  itafanya  mkakati  wa kuongeza  pesa  zaidi  kwa  ajili ya Hospitali ya  Frelimo ,pamoja na  upanuzi wa  Hospitali ya Mafinga na  ujenzi  wa  Hospitali ya wilaya ya  Kilolo pamoja na  upanuzi wa  vituo  vya afya  vya  Ihongole , Malangali , Idodi na  vingine .


Rais Dkt  Magufuli  alisema kuwa serikali imekusudia  kuvipatia  umeme  vijiji  vyote 179  ambavyo  vilikuwa  havina  umeme katika  mkoa   huo  wa Iringa  pamoja na  kuendelea  kuboresha  barabara  kwa  kiwango  cha lami .

Awali  mbunge  wa  viti  maalum  katika  salam  zake kwa  Rais wakati  wa uzinduzi wa barabara  ya Iringa , Migori  na  Fufu alimwomba Rais  Dkt Magufuli  kusaidia  kutatua  changamoto  ya  uboreshaji wa Hospitali ya  Frelimo  kwa  kuiwezesha  kuwa na mashine pamoja na kuomba magereza ya  Iringa  iliyopo  jirani na Hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa  Iringa  kuhamishwa kwenda Mlowa kwani  eneo  la  Hospitali ya  rufaa ni  finyu.

Kuwa  kutokana  na  gereza   hilo kuwepo jirani na  Hospitali ya  rufaa  kunafanya  eneo la  Hospitali  kuwa  finyu  zaidi na  kushindwa kuongeza majengo  mengine na  kuwa  iwapo gereza litahamishwa  eneo  la  Hospitali  litakuwa kubwa  zaidi .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE