May 1, 2018

NITAONGEZA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI KABLA YA KUMALIZA MIAKA YANGU MITANO - RAIS DKT MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa Mshikamano Diama wakati wa sherehe za Mei Mosi katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa leo Jumatatu
Sehemu ya wafanyakazi wakiwa katika  sherehe za Mei Mosi katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa leo
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  akisalimiana na kiongozi wa kimila wa kabila la  Wahehe Chifu Adam Mkwawa wakati wa sherehe za Mei Mosi katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa
Taswira ya  sherehe za Mei Mosi katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa leo

 POlisi wakimshusha  mkazi  wa  Iringa  aliyepanda  juu  kutaka  kutoa  kero yake kwa  Rais  bila  utaratibu .

RAIS wa  jamhuri  ya  Muungano wa  Tanzania   Dkt  John  Magufuli  amesema   iwapo  wafanyakzi wataendelea na ushirikiano  kama  huu  wa  sasa  na iwapo  miradi mbali mbali ya  serikali ikienda  vizuri  atawaongeza mshahara  wafanyakazi  hata  kabla ya  kipindi chake cha urais  kumalizika  tena sio  nyongeza  ya shilingi  10,000.


Akiwahutubia  leo  katika  uwanja wa  Samora  mjini  Iringa katika  kilele  cha   Mei  mosi  Taifa   Rais  Dkt  Ma gufuli  alisema  kuwa alitamani  sana mwaka huu  kupandisha  mishahara  lakini baada ya  kuona  changamoto   zilizopo  ikiwa  ni  Pamoja na kusimamia  bei ya  bidhaa.
Alisema  kuwa  wakati  wafanyakazi  wanafikiria  kupandishwa  mishahara  pia   wafanyakazi  wengine kama  wakulima  nao  wanahitaji  kufaidika na matunda ya  nchi  hii .

 Rais  Dkt  Magufuli  alisema  kuwa  serikali  yake  imefanikiwa  kudhibiti  mfumko wa  bei  toka  alipoingia  madarakani  mfumko wa  bei   ili  kuwapa  unafuu  wafanyakazi na  wananchi kwa  ujumla  na kuhakikisha  bidhaa  muhimu  zinapatikana  kirahisi .

Kwani  kupandisha  misharaha  hakutakuwa na faida  yoyote  iwapo  bei  za bidhaa  mbali mbali  zinapanda  kiholela  hivyo  serikali  itaendelea  kufanyajitihada za  kudhibiti  mfumko wa  bei
Kuhakikisha  serikali  kutoa  elimu  bure kwa  kila  mwezi  kutoka bilioni 285.6 kwa  mwaka   na kwa  kipindi  cha miaka  miwili  serikali yake  imetoa  kiasi cha  shilingi bilioni  714 na  kuwa elimu  bila malipo  imekuwa na faida  kubwa hata kwa  wafanyakazi  kwa  kuwa watoto wao wananufaika
“Tumelipa  madeni ya  mifuko ya  hifadhi ya jamii  kwa  kulipa madeni  toka  mwaka  2013   ilikuwa  ikidaiwa  kwa  kulipa Trilioni  1.6  ila  hadi sasa imelipwa  trilioni 1.4  na  madeni mbali mbali ya  makandarasi na  wazabuni  yamelipwa “

Alisema  kila  mwezi serikali inalipwa  bilioni 900  ambayo hulipwa  madeni ya  ndani  kwa miaka  miwili imelipa  Trilioni 2.7  .

Wakati  mishahara  kila mwezi  inalipwa  zaidi ya  bilioni 5064. Toka  bilioni 777 kwa mwezi baada ya  kua  watumishi  hewa  kwa mwaka  ni trilioni 6.77  kwa  miaka  miwili na nusu   aliyokuwepo madarakani  trilioni 16.935 .

Pia  alisema  serikali  inatekeleza  miradi mbali mbali ya  kijamii  na kukamilika  kwake  kutaleta  faida kwa  watanzania  wakiwemo  wafanyakazi  miradi hiyo ni Pamoja na ule wa reli ya  Dar es Salaam   hadi Dodoma  ,viwanja vya ndege  ,ununuzi wa  ndege  na mingine .

Alisema kuwa  kupanga  siku  zote ni kuchagua   kama  unaweza kujenga  reli  ,kuboresha  mashule  na  Hospitali  ,kununua  ndege  na  kujenga  barabara  ama  kupandisha mishahara na  kuyaacha yote  hayo .
“ Kwangu mimi naamini  ukijenga  reli  na  kubeba mizigo mingi utaongeza  pesa ,ukipeleka  pesa  Hospitalini kutawezesha   vifo kupungua  kuliko  hizi  pesa  kutumika kuongeza mishahara , kwangu  mimi naomba  ukijenga  viwanda  ni  kutaongeza pesa”

Kuhusu  kuunganishwa  kwa mifuko ya  hifadhi ya jamii Rais alisema  kuwa  anaunga mkono na kuwa  suala   hilo  litakamilika  wakati  wowote na  kuwa  na mfuko wa Pamoja
Awali  katibu  wa  shirikisho la  wafanyakazi Tanzania  (TUCTA )  Dkt  Yahaya  Msigwa  akisoma  risala ya  wafanyakaazi  alisema  kuwa  kilio cha  wafanyakazi ni  kuomba  kuongezwa  nyongeza  ya misharaha  Pamoja na  kufanikisha  kuunganisha  mifuko ya   hifadhi Pamoja  .

Aidha  rais  alisema  aliwataka  wakurugenzi wa Halmashauri za  wilaya  kuacha  mara  moja  kuhamisha  watumishi pasipo kuwalipa  stahiki  zao na  kumtaka  waziri mkuu  kuwashughulikia  kwa  kuwafukuza kazi wakurugenzi watakaaoendelea  kukiuka agizo lake .

Katika hali nyingine licha ya kupata kizuizi kikubwa kutoka kwa
walinzi na kisha Rais kumuona na kuwaamuru walinzi wamuache  ma mmoja
mjane aliyefahamika kwa jina la Salma Sanga alimuomba Rais Magufuli
amsaidie kupata haki yake baada ya kupigwa na kumizwa na kasha
mahakama kumuachia mtuhumiwa huru.

Sanga alisema kuwa ni muda mrefu sana amekuwa akiteseka kwa maumivu
makali baada ya kushambuliwa na kijana mmoja ambeya alimpiga mpaka
kusababisha kiumbe kilichokuwa tumboni kutoka jambo liliopelekea
kuondolewa kizazi chake.

“Mh nimekuja unisaidie mahakama iweze kunitendea haki nilipigwa na
kuumizwa mpaka sasa ninaumwa ninawatoto wananitegemea lakini nashindwa
kufanya kazi lakini Mahakama imemuachia mtuhumiwa yuko huko mitanii
wakati mimi nazidi kuteseka Magufuli baba naomba nisaidi” alisema mama
huyu huku machozi yakimtiririka.

Mara baada ya Rais Magufuli kusikia kilio hicho alimtaka kamanda wa
polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire pamoja na mkuuwa mkoawa Iringa Amina
Masenza waweze kumsikiliza mama huyo ili aweze kusaidiwa  shida yake .

“Usiliee tena mama nyanyuka usipige magoti mulinichagua ili
niwasikilize sasa RPC na mkuu wa mkoa nawagiza msikilizeni mama huyuu
na muhakikishe anapata haki yake na kama huyo kijana yuko njee
mkamateni tena kesi ianze upya halafu mutanipa Mrejesho alisema Rais
Magufuli”


Mara baada ya mama huyo kuondoka wakati Rais akiendelea kutoa vyeti na
zawadi kwa wafanyakazi bora alijitokeza kijana mmoja ambaye jina lake
halikufahamika alipanda katika jukwalinalotumiwa na wapig picha wa
matangazo ya moja kwa moja huku akipiga kelele akiomba asaidie lakini
walinzi walifanikiwa kumshusha licha ya kuonekana kuwasumbua walinzi
na kungangania vyuma vilivyoko kwenye jukwa hiyo bila kwa muda.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE