May 10, 2018

MWANAMKE ALIYEDAIWA KUOLEWA MARA 11 APIGWA HADI KUUWAWA

Wanamgambo wa kiislamu wanadhibiti maeneo kadhaa nchini SomaliaWanamgambo wa kiislamu wanadhibiti maeneo kadhaa nchini Somalia
Mwanamke mmoja amepigwa na mawe mpaka kifo nchini Somalia baada ya mahakama moja inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, al-Shabab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.

Shukri Abdullahi Warsame alishutumiwa kuolewa mara 11 bila kutalikiwa na waume zake waliopita.
Sehemu ya kiwiliwili chake kilifukiwa ardhini kichwa kikiachwa juu kisha akapigwa mawe na wanamgambo mjini Sablale mpaka umauti.
Mwaka 2014,wapiganaji wa al-Shabab walimpiga mwanamke mmoja na mawe baada ya kumshutumu kuolewa na wanaume wanne kwa siri, wilaya ya Barawe nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE