May 3, 2018

MUCOBA BENK PLC YAMWAGA MIKOPO YA BILIONI 11.9 KWA WATEJA WAKE ,YATOA ZAWADI YA MILIONI 5 KWA MFANYAKAZI BORA MWAKA 2018


Image result for meneja  Mucoba  MahengeBENKI  ya  wananchi  wilaya ya  Mufindi (MUCOBA PLC) imewapatia  mikopo  wateja  wake  8000 yenye thamani  ya zaidi  ya  shilingi bilioni 11.9 kwa  ajili ya  kufanyia  shughuli  mbali mbali zikiwemo  za  biashara na  kilimo .

Akizungumza  mara  baada ya  kumkabidhi  zawadi  ya shilingi  milioni 5 Hamis Lalika  baada  ya  kuibuka   mfanyakazi  bora kwa mwaka  2018 ,meneja  wa benki hiyo Beny Mahenge (pichani)  alisema  kuwa benki  yake  imeendelea kuboresha  maisha ya  wateja  wake kama  sehemu  ya  kuunga  mkono  jitihada za serikali ya  awamu ya  tano ya  uchumi  wa  viwanda .

Kwani   alisema  kwa  kuwa  viwanda  vingi  vinahitaji malighafi zitokanazo na  kilimo  wao kama  benki  wameweza  kuwakopesha  wateja  wake  3,465 mikopo  yenye thamani ya  shilingi  bilioni 2.3 kwa ajili ya  kilimo  cha mazao  mbali mbali.

Wakati  wateja 6,688  wamekopeshwa  mikopo   yenye thamani ya  shilingi bilioni 7 kwa ajili ya kuanzuisha  na  kuboresha  biashara  zao .

Mahenge  alisema  kuwa kwa  upande  wa wafanyakazi  benki  hiyo   imetoa  mikopo  yenye   thamani ya  shilingi bilioni 2 kwa wafanyakazi 482 ambao ni  wateja  wake  na mikopo  ya kuboreshamakazi  imetolewa  kwa  wateja  78 .

Alisema  kuwa  mikopo  hiyo  ambayo ni mipya imeanza  kutolewa  sasa kwa  wateja  hao  78  kwa  kukopeshwa  mikopo  yenye  thamani ya  shilingi milioni 642.

Hata  hivyo  aliwataka  wateja  ambao  wamepatiwa mikopo  hiyo  kuitumia  kwa malengo  yaliyokusudiwa  ili  wakati wa  kurejesha  kurejesha kwa  uaminifu  ili kuwezesha  wateja  wengine  kunufaika  .

Mahenge  alisema  kuwa  benki  hiyo ya MuCoBa PLC  kwa kuzingatia maombi ya wananchi na  kutokana na mafanikio  makubwa  ya  ukuaji  wake imelazimika  kuwasogelea  wananchi  wengi  zaidi kwa   kufungua matawi  katika  miji na vijiji  mbali mbali  vya  wilaya ya  Mufindi na wilaya  nyingine kama Manispaa ya  Iringa na wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE