May 9, 2018

MKANDARASI ALIYEJENGA UKUMBI WA BILIONI 8.8 AFIKISHWA MAHAKAMANI ASOMEWA MAKOSA MATATU LIKIWEMO LA UHUJUMU UCHUMI

Image result for RAIS  Magufuli  MKwawa
Rais  Dkt  John Magufuli  ndie  aliibua  ufisadi  huu  chuo cha Mkwawa wakati wa  ziara  yake  mkoani Iringa
...................................................................................................................................................................
Na  MatukiodaimaBlog

MAHAKAMA  ya  hakimu  mkazi  mkoa  wa  Iringa imemnyima  dhamana   mkurugenzi  wa kampuni   Engineering  Service  Ltd  mhandisi  Godwin  Mshana  mkazi wa Gangilonga  mjini  Iringa mkoani  Iringa  aliyefikishwa  mbele ya  hakimu  mkazi wa  mkoa wa Iringa  David  Ngunyale akikabiliwa na makosa  matatu likiwemo la  kugushi  nyaraka mbali mbali na uhujumu  uchumi .

 Akisoma mashitaka  hayo  jana mbele ya  hakimu mkazi  wa  mkoa  wa  Iringa David   Ngunyale  wakili  upande  wa  jamhuri Blandina Manyamba   alisema  kuwa  mshitakiwa   huyu  alitenda makosa  hayo matatukati ya  mwaka  2010/2012   katika  ujenzi  wa   ukumbi wa  chuo cha  Elimu  Mkwawa  mjini  Iringa .

Aliyataja  makosa  hayo  kuwa ni  kosa la  kwanza  ni kugushi nyaraka   mbali mbali   na  kosa  la  pili  ni kujipatia  pesa  kiasi  cha shilingi bilioni  3,623,509,196 kinyume  na  utaratibu na  kosa la tatu la  uhujumu  uchumi  wa  shilingi bilioni 2,47,943,822.96  na  kuwa  upelelezi  wa kesi   hiyo bado haujakamilika .

Mshitakiwa  Mshana  anayetetewa na  wakili  wake  Erick  Nyato hakutakiwa  kujibu  chochote  kutokana na mahakama   hiyo  kutokuwa na  uwezo  wa  kusikiliza  kesi   hiyo na  hivyo kurudishwa  mahabusu hadi Mei  22  mwaka  huu kesi hiyo itakapotajwa  tena . 

Kufikishwa mahakamani  kwa mkandarasi  huyo  kumekuja  baada ya  Rais John Magufuli kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa thamani ya fedha iliyotumika kujenga ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Mkwawa (Muce) 

Ikumbukwe mei   Rais Dkt  Magufuli akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa Muce mjini Iringa, Rais Magufuli aliagiza vyombo hivyo ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kufuatilia ujenzi huo uliogharimu Sh8 bilioni.
Pamoja  na  agizo hilo pia aliagiza aliyekuwa mkuu wa chuo hicho, Profesa Phillemon Mushi kuhojiwa , mkandarasi kukamatwa na  wote  waliohusika  watafutwe .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE