May 7, 2018

MBUNGE ROSE TWEVE ATOA MSAADA WA PESA KWA VIKUNDI VYA VICOBA KIASI CHA TSH MILIONI 27 KUTOKA KATIKA MSHAHARA WAKE ,MNEC ASAS AONGEZA NGUVU


Mbunge  wa  viti maalum  mkoa wa  Iringa  Rose  Tweve  (kushoto)  akikabidhi  msaada   wa pesa  kiasi cha  shilingi 600,000 kwa  kikundi cha UWT  vicoba  cha Kiwere 
Mbunge  Tweve  akizungumza na wanawake  wa UWT  Vicoba  Kiwere 
Mbunge  Rose  Tweve  akikabidhi pesa  kwa  kikundi cha Pawaga 
Wanakikundi  wa  UWT  vicoba  Pawaga  wakimpongeza  mbunge  Tweve 
Mbunge  Tweve  akihakiki  pesa  
Viongozi wa UWT vicoba Magozi  wakipokea  pesa 
Wanakikundi  wakimpongeza  Mbunge Tweve 
MBUNGE   wa viti maalum  mkoa  wa  Iringa Rose Tweve  (CCM)  na  mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya  CCM Taifa (NEC) Salim  Asas wamekabidhi  kiasi cha  shilingi  milioni 27  kwa vikundi  45  vya  VICOBA vya   umoja  wa wanawake  wa  chama  cha mapinduzi (CCM)  kwa  ajili ya  kukopeshana.

Akizungumza  jana  wakati wa hafla ya  kukabidhi pesa  hizo mbunge  Tweve  alisema  kuwa amelazimika  kutoka pesa  hizo  ili  kuwawezesha  wanawake  hao  kujikwamua  kiuchumi na  kutokuwa  watu wa  kuomba omba na  ataendelea kufanya hivyo kwa  kati  zote  106 za  mkoa wa Iringa.

Alisema  kuwa moja kati ya ahadi yake  ni  kuwawezesha  wanawake  kiuchumi  na  kutokana na ahadi hiyo moja  aliyoitoa  wakati  akiomba  kuchaguliwa ameamua  kutumia  sehemu ya  mshahara  wake  na posho za  bungeni  kutekeleza  ahadi hiyo kama  alivyo ahidi .

“ Mtakumbuka  wakati  wa naomba  kuchaguliwa  kuwa  mbunge  nilitoa  ahadi moja  pekee  ya  kuwawezesha  wanawake  kiuchumi ahadi ambayo  ilikuwa  ndani ya  uwezo  wangu na  sikutaka kutoa ahadi  nyingi na mlinichagua leo  nimerudi  kutekeleza  ahadi  hiyo kwa  vitendo “

 Alisema  kuwa baada ya  kufanya  vizuri katika  maeneo  aliyoanza  kufanya   mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya  CCM Taifa (NEC) anayewakilisha  mkoa  wa Iringa  Salim Asas alionyesha  kupendezwa na kasi  hiyo  ya  kuwasaidia  wanawake  na aliongeza nguvu kwa  kuchangia  mpango huo kiasi cha zaidi ya  shilingi  milioni 53 kwenye  mfuko  wa  mbunge   Rose  Tweve  mkoa  wa  Iringa .

“ Kazi nzuri  iliyoanza  kuifanya katika  kata  mbali mbali  kwa  kuwawezesha  wanawake  wa UWT  kiuchumi  ilimvutia  MNEC  Asas  na  kulazimika  kuchangia  kiasi kikubwa  cha  pesa katika  mfuko  wa  mbunge  ili kuendelea  kuwawezesha  wanawake zaidi  japo  manufaa haya  si kwa wanawake  wa  CCM pekee hata  wengine  wanaweza  kujiunga japo kigezo  lazima afuate kanuni na kikundi  hapa  suala la kadi  ya  CCM  na ulipaji ada  vinahusika”

Mbunge  Tweve  alisema  alianza katika  wilaya  ya  Mufindi , Kilolo na  Iringa mjini na  kuendelea  katika  wilaya ya  ya  Iringa vijijini katika  jimbo la  Kalenga na Ismani  lengo ni  kuwawezesha  wanawake zaidi .

Alisema  kuwa vipo  baadhi ya vikundi  vimefanya  vizuri kama  kikundi  cha  Nzihi  ambacho kwa sasa  kina mtaji wa  zaidi ya  milioni 8 baada ya  kukopeshwa 600,000 na  kutokana na kasi hiyo kikundi hicho kimepewa    tuzo ya  shilingi   400,000 .

Huku  baadhi ya   vikundi kama  Ulanda  kimeshindwa  kutumia  pesa  hizo  vema na kushindwa kujiendeleza na  hadi sasa viongozi wake  wanatakiwa  kurejesha  pesa  hizo baada ya  kutumia kugawana kufanmyia starehe  badala ya  shughuli  za kiuchumi .

“ Mimi kama  mbunge nafanya haya  kuunga  mkono  jitihada za Rais  wetu  mpendwa Dkt  John Magufuli za  kuwawezesha watanazania  kuwa na uchumi  wa kati ambao utawawezesha  kupiga hatua  na kama  mtatumia  vizuri pesa  hizi  nitaendelea  kuwaongeza zaidi kikubwa  msiwe watu wa kutumika katika kampeni  bila  kuwajali sasa najua  wakati wakampeni  watakuja  wengi ila  wakati wa  kuwasaidia ni  sasa “

Hata  hivyo  alisema  mpango  wake  kupitia mfuko   huo  ni kutembelea kata  zote   106  za  mkoa wa Iringa  na kupitia kata  hizo wanaweza  kushuka chini kwa  kuanzisha vikundi vya  matawi kupitia  mtaji  watakaopata  na  kuwa  kila mwezi  kikundi  kitapaswa kurejesha  kiasi cha shilingi 15,000  na pindi   kwenye mfuko  wa wanawake wilaya   ili  kusaidia  viongozi  weanapokwenda katika  mikutano na vikao  vya UWT  wilaya .

Katibu  wa  UWT wilaya ya Iringa Vjijini, Asha Stambuli alisema  kuwa kwa  kiongozi ambayo atasababisha  pesa  hiyo  kupotea  atawajibika na  kuchukuliwa hatua kali kwani  pesa hiyo  sio sadaka ni pesa inayopaswa  kuleta maendelea katika jumuiya hiyo ya UWT .

Huku mwenyekiti  wa UWT  Iringa  vijijini Lenah Hongole pamoja na  kupongeza kazi kubwa inayofanywa na  mbunge  Tweve katika  kuwawezesha  wanawake alisema kuwa lengo la UWT  wilaya  hiyo ni  kuwana  benki ya  wanawake wilaya ya  Iringa vijijini na lengo   la chama  chochote  cha siasa  duniani ni  kushika  dola  na kwa  chama  kilichopo madarakani  ni kuona  kinaendelea  kuongoza ,wao   kama  moja kati  kiunganishi  cha jumuiya  za  chama wameamua kuwa  na mipango mikakati ya kazi.
“ Wanawake  ni  jeshi  kubwa ndani ya  CCM  hivyo  ushindi wa  CCM unaongezwa chachu  kubwa  na  wanawake   hivyo lazima sisi kusimama  imara  kuona  tonatofautiana na wanawake  wa  upinzani ambao wenzetu  mipango na  mikakati yao  ni  kuona  wanaandamana  mara  ngapi  ama  wanashiriki vurugu mara  ngapi kwa miaka  mitano”
Alisema  kuwa  UWT ina   mipango mikakati yenye  kuisaidia  jamii  kupata   huduma  bora  na kwa  wakati wanawake  wenzao wanaishia kukaa mahabusu kwa maandamano  ama  kwa kutumia  mitandao  ya  kijamii  kutukana serikali .

Huku  akipongeza  jitihada za  wadau mbali mbali kama MNEC Iringa  Salim Asas  na mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa  Arif  Abri  ambao  wameungana  kuona  UWT  inapiga  hatua .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE