May 3, 2018

MBUNGE MWAMOTO AMPONGEZA RAIS JPM KUSIKIA KILIO CHA WANAKILOLO Rais  Dkt  Magufuli kushoto  akiwa na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto katikati na waziri wa Tamisemi Suleman Jafo 
................................................................................................................................................
MBUNGE wa jimbo la Kilolo  mkoani Iringa  Venanci Mwamoto  amempongeza Rais Dkt  John Magufuli kwa kuahidi  kujenga  barabara  ya  lami  kutoka Ipogolo mjini  Iringa  hadi makao  makuu ya  wilaya ya  Kilolo .

Akitoa  pongezi   hizo  jana  mara  baada ya  Rais Dkt Magufuli kuahidi  barabara  hiyo  yenye  urefu wa  kilometa 33 kujengwa  yote  kwa  kiwango  cha lami ,Mwamoto  alisema  kuwa amefarijika  sana  kwa Rais kusikiliza  kero  ya  wanakilolo juu ya  ubovu wa barabara  hiyo .

Hivyo  alisema  kwa  kupitia ahadi  hiyo ya Rais  wanakilolo wamepatiwa ufumbuzi  wa kero ya  barabara na  kuwa  ziara  ya  Rais ndani ya  kilolo imekuwa ni ziara  yenye Baraka  kubwa  na kuwa kujengwa  kwa  barabara  hiyo  ambayo pia  ilikuwepo katika  ilani ya  chama  cha  mapinduzi (CCM)  itawezesha  wananchi  wa Kilolo kunufaika  zaidi na  kilimo  wanacholima ukilinganisha  na  sasa  ambapo  wanalazimika kuuza mazao yao kwa  bei ya  chini   shambani  kutokana na ubovu wa  miundo mbinu.

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akimpongeza Rais Dkt  Magufuli kwa  kuahidi makubwa  Kilolo .
..............................................................................................................................................
“Mheshimiwa Rais wetu  Dkt  John Magufuli amesikia  kilio   chetu  wana Kilolo na  kujengwa  kwa barabara   hii kwa  kiwango cha lami ni ukombozi  mkubwa  na wakulima  watanufaika  zaidi kwani  wataweza  kulima  kilimo  chenye  tija kwa  kusafirisha  wenyewe  mazao hadi  sokoni  Iringa ama  kuuza  shambani kwa  bei nzuri kwani visingizio  vya  walanguzi wa mazao kutokana na ubovu wa barabara  havitakuwepo  tena”

Mbunge Mwamoto  alisema Rais  Dkt Magufuli pia  ameweza  kutekeleza ahadi  yake  wakati wa kampeni kwa wakazi wa mji wa Ilula  kuwa  wakimchagua yeye kuwa Rais  na kumchagua Mwamoto kuwa  mbunge atahakikisha  kero ya maji iliyodumu kwa miaka  mingi Ilula  inapatiwa  ufumbuzi  na  kuwa  hadi  sasa  tayari ametoa  pesa  kiasi cha  shilingi  bilioni 5 kwa  ajili ya  ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Ilula.

Hivyo Mwamoto  pamoja na kupongeza jitihada za Rais na  serikali ya  awamu ya tano kwa  kazi nzuri na kubwa inayoendelea  kuifanya  alisema kutokana na  wilaya ya  Kilolo  kijografia  kuwa na ukanda wa mvua na  joto  anaomba  kusaidiwa  kujengewa  mabwawa ya  umwagiliaji katika  tarafa ya Mahenge  ambayo inategemea  kilimo cha umwagiliaji  zaidi.
Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo Aloyce  Kwezi  akipongezwa na  rais Dkt Magufuli baada ya kusoma risala ya  wilaya ya Kilolo

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE