May 10, 2018

MBIO ZA MAGARI KUKUTANISHA NCHI ZAIDI TANO KUTIMUA VUMBI MJINI IRINGA MEI 12 -13 MWAKA HUU

mwenyekiti wa mashindano hayo  Amjad Khan katikati  akitoa taarifa ya mashindano hayo
Mdhamini  mkuu  wa mashindano hayo kutoka Maji  mkwawa  katikati  akifafanua  jambo
Wadau  wa  mashindano ya mbio za magari  Iringa


Katika mashindano hayo ya  mbio  za magari yanayofahamika kwa  jina la  Rally Of Iringa ni ya  pili  kufanyika mkoa Iringa  chini ya udhamini  wa maji Mkwawa .

Akizungumza leo  na wanaandishi wa habari  mwenyekiti wa mashindano hayo  Amjad Khan alisema kuwa nchini  zilizojitokeza  kushiriki mashindano  hayo ni Uganda , Kenya , Zambia , Zimbabwe na Wenyeji  Tanzania .


Alisema mashindano hayo kwa mwaka huu yatakuwa yanapita njia za mashambani kwa sababu za usalama wa wananchi na mali zao pia  kuepusha msongamano mjini  Iringa .
Khan alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa na njia tatu ambapo yataanzia katika kiwanda cha maji cha mkwawa  kilichopo manispaa ya Iringa,kwenda kuzunguka uwanja wa CCM wa Samora na kuelekea hadi Tanesco ya zamani na baadaye yataenda kijiji cha Kalenga,Nzihi na Zimamoto ambavyo vipo katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.

Msaidizi  wa mwenyekiti wa mashindano  hayo Hidaya Kamanga alisema kuwa  washiriki mwaka huu wameongezeka hadi kufikia 19 tofauti na mwaka jana ambao walikuwa 12 pekee.

Hata  hivyo  alisema kuwa hadi sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 na wanategemea washiriki wote watashiriki ikiwamo pia kuwahakikishia usalama wao pindi wawapo mkoani Iringa.Kuhusu  wadhamini  wengine  waliojitokeza alisema ni pamoja na Iringa  Sun set hotel ,Famari store,Ymk Garage,Planet 2000  huku  maji ya Mkwawa superior pure drinking water.ndio  wadhamini  wakuu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE