May 23, 2018

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ATAKA WANANCHI MUFINDI KUTUNZA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa taarifa ya miradi ya mwenge katika mapokezi ya mwenge mkoa wa Iringa leo
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Charles Kabeho akikabidhi kadi ya matibabu bure kwa wazee wa kijiji cha Sadani Mufindi
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Charlesy Kabeho akizungumza na wanawake wajawazito kabla ya kuwapatia neti
Viongozi wa CCM Mufindi Daud Yasini kushoto na Mbunge wa Mufindi kusini Mheshimiwa Mendrady Kigola wakifuatilia hotuba ya kiongozi wa mbio za mwenge


KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa Charles Kabeho amewataka wananchi wa Halmashauri ya Mufindi mkoani Iringa kutunza miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.1 ya kimaendeleo iliyofunguliwa na mbio za mwenge.

Akizungumza kwa nyakati tofauti leo wakati wa ufunguzi wa miradi  6 wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru jana ,kiongozi huyo alisema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuona wananchi wanaendelea kupatiwa huduma mbali mbali ikiwemo ya elimu,afya na nyinginezo.

Hivyo alisema pamoja na ushiriki wa wananchi katika uchangiaji wa nguvu zao katika miradi hiyo bado wanawajibu wa kulinda miradi hiyo na kuwafichua wahujumu wa miradi iliyojengwa.

"Leo tumefungua miradi hii nawaombeni kila mmoja wenu kuwa mlinzi wa miradi hii tusiruhusu watu wasiopenda maendeleo kuharibu miradi yetu"

Kabeho alisema kuwa katika suala la elimu serikali imejipanga kuona wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari wanapata elimu bila malipo na kuwa jukumu la wazazi kuwapatia watoto mahitaji ya msingi ya shule kama Sare na mingine ambayo yapo katika uwezo wao.

Aidha alisema halmashauri za wilaya zinapaswa kujenga miradi ya elimu na mingine kwa kuzingatia ubora wa miradi hiyo .

Kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi alitaka mkoa wa Iringa kuendelea kupunguza kasi ya maambukizi ya UVVU na kutoka katika nafasi ya pili kitaifa.

"Kasi ya UVVU kwa mkoa wa Iringa ni asilimia 11.3 huku Njombe ikiwa ni asilimia 11.4 na Mbeya ni asilimia 9 hii si hali nzuri kwa mkoa hii mitatu lazima jitihada zinanyike kutoka katika nafasi hii"

Akitoa taarifa ya miradi ya kimaendeleo iliyopitiwa na mbio za mwenge wa Uhuru 2018 Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alisema miradi hiyo 6 ni pamoja na mradi wa uwekaji jiwe la msingi vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari Igombavanu,uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa,mradi wa msitu wa Kupandwa wa halmashauri,mradi wa hifadhi ya mazingira wa msitu wa kupandwa na mradi wa ujenzi wa zahanati na mingine.

Alisema kuwa wilaya ya Mufindi imeendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Alisema jumla ya miradi hiyo 6 ina thamani ya shilingi bilioni 9,199,229,136.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE