May 11, 2018

IRINGA SUN SET HOTELI KUJULIKANA KIMATAIFA KUPITIA MBIO ZA MAGARI


Image result for Iringa  Sun Set Hotel 
Mkurugenzi  wa Iringa Sun Set  Hoteli  Batsta Filipatali  akipongezwa na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza baada ya  kupata  huduma katika  Hoteli  hiyo .
Image result for Iringa  Sun Set Hotel
Rais Mstaafu  wa awamu ya  nne  Dkt  Jakaya  kikwete  akiwa na wafanyakazi wa Iringa Sun Set Hoteli

........................................................................................................
IRINGA  Sun Set  Hotel   imekuwa ni hoteli pekee mkoani Iringa kujitokeza kudhamini mashindano ya  mbio  za magari yenye  sura kimataifa yatakayofanyika  kuanzia  kesho  jumamosi na  jumapili  mjini Iringa .

Akizungumza na mtandao  wa matukio daima mkurugenzi wa Iringa  Sun set  Hoteli Batsta  Filipatali  alisema  kuwa  Hoteli   hiyo  yenye  hadhi  kubwa ya  kiutalii mjini  Iringa toka  ianzishwe  imekuwa ni nguzo  ya  maendeleo ya  mkoa wa Iringa na ndio  sababu ya kuendelea  kuunga mkono  jitihada  mbali mbali zenye kuuletea mkoa  wa  Iringa  heshima  za  kimaendeleo .
Image result for Iringa  Sun Set Hotel

Alisema  kuwa  hoteli   hiyo ambayo ni  moja kati ya  Hoteli  zilizopo  eneo lenye utulivu ambalo  linakuwezesha  kushuhudia mji  wa Iringa na  jua linapozama kwa  urahisi zaidi  inapataka na  shule ya  Msingi Mapinduzi na imekuwa na utaratibu wa  kutoa  huduma  zenye  uhakika  za vyakula  ambavyo Hoteli  nyingine   huwezi kupata  kwa  ubora kama  wa  Iringa  sun Set  Hoteli .Mwenyekiti wa mashindano hayo  Amjad Khan alisema kuwa nchini  zilizojitokeza  kushiriki mashindano  hayo ni Uganda , Kenya , Zambia , Zimbabwe na Wenyeji  Tanzania .
Alisema mashindano hayo kwa mwaka huu yatakuwa yanapita njia za mashambani kwa sababu za usalama wa wananchi na mali zao pia  kuepusha msongamano mjini  Iringa .
Khan alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa na njia tatu ambapo yataanzia katika kiwanda cha maji cha mkwawa  kilichopo manispaa ya Iringa,kwenda kuzunguka uwanja wa CCM wa Samora na kuelekea hadi Tanesco ya zamani na baadaye yataenda kijiji cha Kalenga,Nzihi na Zimamoto ambavyo vipo katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.

Msaidizi  wa mwenyekiti wa mashindano  hayo Hidaya Kamanga alisema kuwa  washiriki mwaka huu wameongezeka hadi kufikia 19 tofauti na mwaka jana ambao walikuwa 12 pekee.

Hata  hivyo  alisema kuwa hadi sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 na wanategemea washiriki wote watashiriki ikiwamo pia kuwahakikishia usalama wao pindi wawapo mkoani Iringa.
Kuhusu  wadhamini  wengine  waliojitokeza alisema ni pamoja na Iringa  Famari store,Ymk Garage,Planet 2000  huku  maji ya Mkwawa superior pure drinking water.ndio  wadhamini  wakuu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE