May 27, 2018

HII NI KALI YA MWAKA MANISPAA YA IRINGA YANASWA ,MAFINGA MJI TARURA YAHARIBU

Kiongozi  wa  mbio  za  mwenge Kitaifa  Cherlresy  Kabeho  akichimbua  barabara  ya  mji mafinga kupata  usahihi  wa zenge  iliyotumika WAKATI  kiongozi  wa  mbio  za  mwenge  Kitaifa  Charlesy Kabeho  akitoa  muda  wa  wiki mbili   kwa  Taasisi ya  kuzuia na kupambana na  Rushwa ( TAKUKURU )  kuchunguza  mradi wa  barabara ya  kiwango cha lami ya  Samora  ,Mashine tatu  Mkwawa  katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa   yenye  urefu wa Kilomita  3.4 iliyojengwa kwa  kiasi cha  zaidi ya  shilingi Bilioni 5.3  kiongozi  huyo atilia shaka mradi wa maji Halmashauri Mji Mafinga .

Akitoa  maagizo hayo  leo  kiongozi  huyo  aliiagiza  vyombo  vinavyohusika ikiwemo Takukuru  ndani ya  wiki mbili   kuanzia jana  kutuma  taarifa ya  uchunguzi wa pesa  zilizolipwea kwa mkrandarasi  wa  barabara   hiyo  pamoja na vielelezo  vyote .

Kwani alisema  pamoja na mradi  huo  kujengwa  kwa kiwango  kinachofaa  ila ana hofu ya  pesa  zilizoptumika katika  ujenzi  huo  hivyo lazima uchunguzwe na taarifa  azipate kwa  muda  huo na kama wapo  waliohusika na matumizi mabaya ya  pesa  basi  waweze   kuwajibika.

Kuhusu Halmashauri ya mji Mafinga  pamoja na  kupongeza  miradi  mbali mbali mbali ya  kimaendeleo miradi 9 yenye  thamani  ya  shilingi bilioni 1.7 bado  kiongozi   huyo  alitaka  mradi  wa  ujenzi  wa  darasa  shule ya  sekondari  Ihongole  kufanyiwa  marekebisho  ya  haraka  huku  mradi wa  ujenzi wa  tenk la maji  mtaa Tanganyika lililojengwa  kwa shilingi milioni  407,658,553 kupatiwa vielelezo  vya malipo ,vipimo  vya  udongo na  vingine.

Kabeho  alisema  lengo la  kutoa maagizo hayo ni  kuona  pesa za seriokali  zinazotolewa na  serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt  John Magufuli  zinatumika kwa  kuzingatia ubora  wa  miradi.
  Sijaukataa mradi  wenu  nimeukubali na umejengwa  vizuri ila nataka  tu nijiridhishe  na matumizi ya  pesa  zilizotumika na kama  kuna mtu  amehusika  kula  pesa  basi  hatua  kali  zichukuliwe dhidi yake”
Alisema  kuwa  suala la  ujenzi  wa  miradi  linapaswa  kuzingatia  ubora  na  matumizi   sahihi ya  pesa  na  kuwa  wakimbiza  mwenge wa  safari  hii  wamejidhatiti kwa kuwa  na  wataalam wa  miradi  na watalamu  wa  tathimini ya  miradi na ndio  sababu  wamekuja na  kila aina ya  vifaa vya  kukagulia  miradi  hiyo kama sululu  na vifaa vingine .
Mkurugenzi wa Halmashauri  mji  Mafinga  Saada Mwaruka  alisema  katika  miradi   hiyo  9 ya  kimaendeleo  iliyozinduliwa na Mwenge  mwaka  huu  ,wananchi  wamechangia shilingi 954,545,000,halmashauri  imechangia  shilingi 47,259,000, serikali  kuu  imechangia  shilingi 741,491,653 na wahisani  wamechangia 954,545,000 na  kufanya  jumla  ya  fedha  zote  kufikia  shilingi 1,781,296,053.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE