May 15, 2018

Halotel yazindua Super Halo kwa kishindo

ANNIV SIGNATURE-03
-          Pia yazindua Facebook bure kwa wateja wote
Dar es Salaam,  Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua kifurushi kisichokuwa na kikomo cha muda kitakacho wawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano bila kikomo cha muda wa kutumia kifurushi hicho kilichopewa jina la Super Halo.
Wateja wa mtandao wa Halotel watakao jiunga na kifurushi hicho wataweza kupiga simu au kutumia intaneti hadi pale kifurushi kitakapokwisha na mteja hatokuwa na hofu ya kuisha kwa muda wa kifurushi chake.
Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, uzinduzi huo wa kifurushi cha Super Halo ni mapinduzi mengine makubwa katika sekta ya mawasiliano kwa kuondoa ukomo wa muda katika vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti.
“Hii ni hatua nyingine kubwa ya ubunifu wa hali ya juu katika utoaji wa huduma zetu ili kuwawezesha wateja  wetu wote walioko  nchi nzima kunufaika na huduma za mawasiliano bila ya kuwa na wasiwasi wa kuisha kwa muda wa matumizi ya mawasiliano hayo pamoja na kukidhi mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi kupitia kifurushi hiki” Alisema Semwenda na Kuongeza.
“Kifurushi hiki kinawapa fursa kubwa watanzania wote ambao ni wateja wa Halotel walioko nchi nzima kuweza kujiunga na kufurahia dakika nyingi za muda wa maongezi za kuweza kupiga Halotel kwenda Halotel na Halotel kwenda mitandao mingine pamoja na MB za intaneti za kutosha ambavyo vifurushi vyote hivi wateja watavitumia bila bila kikomo, cha muda wa maongezi Aliongeza Semwenda.
“Mteja wa Halotel anaweza kujiunga kwa kuanzia shilingi 500 na kupata dakika 17 za  kupiga Halotel bila kikomo vha muda na kwa shilingi 500 hiyo hiyo mteja anaweza kujiunga na kupata MB 110 za intaneti za kutumia bila kikomo. 

Lengo kubwa katika kifurushi hiki ni kumwezesha mteja kuona thamani ya pesa yake na kuweza kufurahia mawasiliano  ya kupiga simu na kutumia MB za intaneti bila kikomo cha muda”.Alisisitiza Semwenda.
Mbali na Kifurushi hicho cha SUPER HALO, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo alipata fursa ya kuzindua huduma nyingine mpya  ya Facebook Bure, ambapo kuanzia sasa wateja wote wa Halotel nchi nzima wataweza kuperuzi mtandao wa Facebook bure.
““Tutaendelea kuhakikisha wateja wetu walioko mijini na vijijini wanapata huduma bora inavyoendana na uhalisia wa maisha yao, na kuhakikisha hili linaendana na uhalisia, pamoja na kifurushi cha SUPER HALO, leo tunazindua huduma nyingine mpya ya Facebook Bure itakayowawezesha wateja wetu nchi nzima kuweza Kulike, kukomenti,kuchat na rafiki na ndugu zao kokote walipo nchini pamoja kuperuzi  taarifa mbalimbali kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook bila gharama yoyote. Aliongeza Semwenda.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE