May 13, 2018

HALMASHAURI YA MJI MAFINGA KUJENGA STENDI YA KISASA KAMA KITEGA UCHUMI


HALMASHAURI  ya  mji  Mafinga  wilayani  Mufindi mkoani  Iringa  imetarajia  kujenga  stendi  kubwa ya  kisasa kama  kitega  uchumi  eneo la  Kinyanambo kutokana na mji  huo  kutokuwa na  stendi ya Mabasi toka  ulipopandishwa  hadhi ya  kuwa  mji  mdogo  wa  wilaya ya  Mufindi.

Akizungumza  katika  kikao  cha  kawaida cha baraza la madiwani  mwenyekiti  wa Halmashauri ya  mji Mafinga Charles Makoga   aliyasema  hayo   wakati  wa  kikao  hicho  kubwa  Halmashauri  hiyo  imekusudia  kujenga  stendi ya  kisasa  itakayokuwa moja kati ya  kitega  uchumi  cha Halmashauri  hiyo ambayo  itazungukwa na  milango ya  biashara .

Kuwa  tayari  eneo la  ujenzi wa  stendi  hiyo  wameshalinunua  na  lipo katika  hatua ya  kufanyiwa usafi na  kuendelea  na michoro ya  stendi  na  baada ya  hapo   wataliombea  mkopo  ili  kuanza  ujenzi  wake

Kwani  alisema  pamoja na  kuwa  Halmashauri  hiyo ni changa  ila  imeendelea  kufanya  vizuri  katika ukusanyaji wa mapato yake ya  ndani na  kufikia  wastani  wa  shilingi  bilioni 3  kwa mwaka na  kuwa  jitihada za  kutafuta  vyanzo  mbali  mbali  vya mapato   ili  kuongeza  ukusanyaji  wa mapato  zinaendelea  ikiwa ni pamoja na kubuni  na  kuweka  mikakati ya  kukusanya mapato katika  vyanzo  mbali mbali  vilivyokuwa   vimesaulika katika  ukusanyaji wa mapato.

" Lakini  zipo  changamoto  mbali mbali za  ukusanyaji  wa  mapato  mfano  kodi  za majengo na  mabango  ambazo awali zilikuwa  zikichangia  mapato ya Halmashauri  kwa sasa  kodi  hizo  zimeondolewa na  kupelekwa  serikali  kuu  hivyo  vyanzo  hivi kuondolewa kwetu  tunalazimika kuanzisha  vyanzo  vipya vya  ukusanyaji wa mapato  ya  ndani " alisema  Makoga

Hata  hivyo  alisema  changamoto  nyingine  kubwa kwa  Halmashauri ya  mji  Mafinga na upungufu  wa watendaji  wa  mitaa na  ndio  maana  wamekuwa  wakishindwa  kukusanya  kodi za  ujenzi pamoja na  ukamataji  wa  watu  wanaojenga  kiholela katika maeneo mbali mbali  japo  tayari  gari linafanyiwa matengenezo  ili  kuanza msako  wa  kuwakamata na  kuwatoza faini wale  wote  wanaojenga   na  waliojenga bila  vibali .

Pia  alisema  Halmashauri ya  mji Mafinga  imeendelea  kujipanga  kunufaika na  utalii  kwa  mikoa ya  nyanda  za  juu  kusini kufuatia  ahadi ya  Rais  Dkt  Magufuli  ya  kuujenga  uwanja wa Ndege  wa Nduli kwa  kiwango  cha lami  ili  kuwezesha  ndege  kubwa  za  watalii  kutua katika uwanja  huo  kwa  ajili ya  kufanya  utalii katika  hifadhi ya Ruaha  na   vivutio  vingine  vya utalii .


Hivyo  tayari wameanza  kuboresha  maeneo ya  vivutio  vya utalii  vilivyopo katika  Halmashauri  hiyo   ili  kuwavutia  zaidi  watalii  pindi  nguvu ya  serikali  kutangaza  vivutio  vya  mikoa  ya  kusini itakapoanza .

Akielezea  utekelezaji  wa agizo la  Rais  Dkt  John  Magufuli la  kuelekeza  vita  ya  kupunguza kasi ya  maambukizi ya  virusi vya  UKIMWI baada ya  mkoa  wa  Iringa  kuwa  mkoa  wa pili kwa  maambukizi  kutoka  mkoa  wa  Njombe  unaoongoza  kitaifa  ,alisema  kuwa  mji wa Mafinga  ni moja kati ya  miji  ambayo  inawageni  wengi na  hata kasi ya  VVU  ipo  juu  hivyo  wameanza makakti wa  kuona  wanaendelea  kutoa  elimu pamoja na  kusambaza kondom katika  nyumba za  kulala  wageni .

kaimu  mkurugenzi  mji  Mafinga  Francis  Maghembe  alisema  kuwa kutokana na  kuongezeka  kwa  ukusanyaji wa mapato  ya ndani  Halmashauri  pamoja na utekelezaji  wa miradi  mbali mbali ya  kimaendeleo  imeendelea  kuwawezesha   vijana ,wanawake na walemavu  kwa  kuwapa  mikopo  kwa  mujibu  wa  agizo la  bunge la  Halmashauri  kutumia  makusanyo yake ya  ndani  kutoa mikopo  asilimia 10  kwa makundi  hayo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE