May 10, 2018

HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA YAENDELEA KULIPA MADAI YA WATUMISHI WALIOHAMISHWA


 Kaimu  mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa  Omary Mkangama  kushoto akiwa na  baadhi ya  watumishi  wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa .
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
WAKATI  Rais  Dkt  John Magufuli  akizitaka  Halmashauri  nchini  kutohamisha  watumishi  bila  kulipa pesa zao za  uhamisho  ,Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  imekuwa  mfano kwa kuendelea  kuwalipa madeni watumishi hao  waliohamishwa  vituo vyao  vya kazi.

Akizungumza na wanahabari leo kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Omari  Mkangama   alisema  kuwa wapo  baadhi ya  walimu  walihamishwa katika  shule za Msingi na  sekondari  ambao  walihamishwa na  tayari  wameanza  kulipwa  stahiki  zao .

Alisema  kuwa katika  Halmashauri  hiyo  kulikuwa na walimu    125  ambao  walihamishwa  toka   Sekondari  kwenda  shule za msingi  kati ya hao  Halmashauri  imewalipa  asilimia  65   ya madai  yao  ambayo ni  zaidi ya milioni 69  zimelipwa .


"wapo  ambao  walikuwa  walimu  wa  shule  za  msingi na  sekondari  waliohamishwa  na  tunaendelea  kufanya mchakato  wa  malipo na  wote  watalipwa "

Hata  hivyo  alisema wapo  baadhi  yao  ambao  walihamishwa kabla ya  agizo la Rais  ila  Halmashauri  haina  mpango  wa kuwachelewesha  malipo yao na  wote  watalipwa na  kuwa taka  kuendelea  kuchapa kazi katika maeneo yao .

Pia  alisema  tayari  katibu wa chama cha  walimu  wilaya ya  Iringa amefika  ofisini kwake  akiwa na walimu  wanaodai na  wamekubaliana  kuwa   siku  si  nyingi  watalipwa  haki zao .

Aidha  alisema  wapo  walimu  wanne  kutoka  shule ya  Msingi Mapinduzi  ambao  walikwenda  CMA  kulalamika  na tayari  wamekubaliana  kulipwa madai  yao  na hadi  sasa hakuna mgogoro kati ya Halmashauri na walimu .

Alisema  walimu hao  kulikuwa na marekebisho ya  barua  zao na hadi  sasa  tayari  barua  zao  wamezifanyia marekebisho na  wapo katika  orodha ya  walimu  wanaopaswa  kulipwa  stahiki  zao .

Kuhusu  aina ya  malipo wanayopaswa kulipwa  walimu hao waliohamishwa  alisema  kisheria  mtumishi kutoka  ndani ya Manispaa analipwa  pesa  ya usumbufu  kutoka  eneo  moja  kwenda nyingine  wakati yule wa  kijijini  anapaswa  kulipwa  pesa ya  usumbufu na kujikimu na  wao kama  Manispaa  wanadaiwa  pesa  ya  malipo ya  usumbufu  pekee.

Mkangama  alisema  kuwa  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa ipo  kwa ajili ya  kutekeleza maagizo yote  yanayotolewa na serikali na itaendelea  kuwa karibu na  walimu  kwani  inatambua  mchango  wa  walimu katika  kuiwezesha  Halmashauri  hiyo  kuwa  bora kielimu .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE