May 16, 2018

HAKIMU WA KESI YA ABDUL NONDO ASEMA HAWEZI KUJITOA KUSIKILIZA KESI HIYO

Mshitakiwa  Abdul  Nondo kushoto akizungumza na wakili  wake Jebra Kambole leo  nje ya  viwanja  vya mahakama ya  hakimu mkazi  mkoa wa Iringa .
 Na MatukiodaimaBLOg
WAKATI  mshitakiwa  wa  kesi  ya  kudaiwa  kujiteka  Abdul Nondo  juzi  aliwasilisha barua ya  kumkataa hakimu John Mpitanjia  anayesikiliza  kesi   hiyo ,hakimu   huyo  amekataa  kujitoa  kusikiliza  kesi kwa madai sababu za  kumkataa hazina  msingi .


Nondo  ambae ni  mwenyekiti wa mtandao wa Wanafunzi wa  vyuo vikuu Tanzania (TSNP)  katika  kesi  hiyo anawakilishwa na mawakili  wawili Chance  Luoga na Jebra Kambole alilazimika  kuandika  barua  hiyo ya  kumkataa  hakimu  Mpitanjia wa mahakama  ya hakimu  mkazi  mkoa wa  Iringa .

Akitoa majibu ya barua  hiyo  ya  Ndondo  juu ya  kumkataa hakimu  huyo leo mahakamani hapo  ,hakimu  Mpitanjia  alisema  kuwa hoja   zilizotolewa na  mshitakiwa za  kumkataa hakimu  hazina msingi  hivyo ataendelea na  kesi  hiyo kama kawaida .

Hata  hivyo pamoja na wakili  upande wa utetezi  kuomba kesi hiyo  kuendelea kesho mahakama  hiyo  imelikubali  ombi la  wakili  upande  wa jamhuri  la  kutaka kesi hiyo kuandelea Mei  18  kutokana na mmoja kati ya mashahidi  wawili wa  kesi hiyo  kutoka  jijini Dar es Salaam .
 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE