May 17, 2018

DIWANI IBRAHIM NGWADA NI MWIBA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA IRINGA

Katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilikuwa ni moja kati ya Halmashauri zilizochukuliwa na chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema) na kati ya kata takribani 17 za jimbo la Iringa mjini ni Kata nne pekee CCM iliambulia.

Kati ya Kata hizo ambazo ni Kitanzini,Nduli na Mlandege  ,Kata ya Mshindo pia ilikuwa miongoni na Ibrahim Ngwata kufanikiwa kuwa Diwani kwenye Kata hiyo.

Ngwada si mgeni katika ulingo wa siasa kwani ukiacha familia anayotoka kuwa ni familia ya siasa ,Ngwada alipata kuwa mwenyekiti wa Uvccm Iringa mjini na nafasi mbali mbali amepata kuzitumikia na udiwani wake si alipata kwa bahati nasibu lah hasha .

Kutokana na ukomavu wa kisiasa Ngwada ameendelea kuwa mwiba katika baraza la madiwani katika Halmashauri inayoongozwa na Chadema na pamoja na uchache wa madiwani wa CCM ila bado kwa uwepo wake ni kama Chadema na CCM kwenye baraza wapo sawa.

Ukiacha wakati huo walipo kuwa wanne sasa nguvu imeongezwa zaidi na kufikia madiwani sita baada ya Kata ya Kitwiru na kihesa kuongezeka hivyo Baraka Kimata ameweza kuongeza moto zaidi katika baraza hilo kwani nae si mgeni wa siasa za Chadema kwa kuwa alikuwa Diwani wa Chadema kabla ya kujiuzulu na kugombea kwa CCM.

Hivyo nguvu za madiwani hawa zimekuwa zikimkosesha raha Meya Alex Kimbe kwani ni madiwani wanaojenga hoja zinazompa wakati mgumu Meya na hata kufikia hatua ya kutishia kuwatoa nje ya kikao.

Inaendelea.........

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE