May 16, 2018

DC KASESELA ATOA SIKU 7 KWA WADAIWA SUGU WA MIKOPO YA SIDO , VIPO VIKUNDI VYA MUNGU AMETENDA


Mkuu wa  wilaya ya Iringa  Richard  Kasesela  akizungumza na wanahabari  leo  ofisini  kwake  kuhusu  wadaiwa  sugu  wa  SIDO  kuanikwa
Mkuu  wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akifafanua  jambo  leo juu ya  wakopaji wa SIDO
Afisa  biashara wa  SIDO  Niko Mahinya  akifafanua  kuhusu  wakopaji  walioshindwa  kurejesha kwa  wakati  mikopo ya  SIDO ,kushoto  ni  meneja  wa  Sido  mkoa  wa Iringa  Francisca Simon
Afisa  mikopo  wa  Sido  mkoa  wa  Iringa Neserian  Laizer  akifafanua  kuhusu  mikopo  ambayo haijarejeshwa  kulia  ni meneja wa  Sido  mkoa  wa Iringa Francisca Simon 

Na  MatukiodaimaBLog 

MKUU  wa  wilaya ya  Iringa mkoani Iringa Richard  Kasesela  ametoa  siku  saba  kujisalimisha kwa wadaiwa  sugu vikuwemo  vikundi viwili vya vya  Mungu ametenda ambavyo kwa pamoja  vinadaiwa mkopo wenye thamani ya  Zaidi ya  million  293,380,925 iliyotolewa na  shirika la  kuhudumia  viwanda vidodo (SIDO) mkoa  wa  Iringa  .
Akizungumza na  wanahabari jana  ofisini  kwake  mkuu  huyo wa  wilaya ya  Iringa ,Kasesela  alisema  kuwa  vikundi  namba  moja na namba  mbili  vya Mungu  ametenda pekee  yake  vinadaiwa  kiasi cha shilingi milioni 32 wakati wadai sugu  wengi  wapo  katika  Manispaa ya  Iringa ambao kwa pamoja  wanadaiwa  kiasi cha shilingi   269,331,225 wakati halmashauri ya Iringa  vijijini  wanadaiwa  4,858,700 ukiacha  wadaiwa wa  wengine  kutoka  wilaya za  mkoa  wa Iringa .


Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema  kuwa  shirika   la  SIDO ni la umma na lengo  lake kuu  toka kuanzishwa  kwake  ni kupanga na  kuratibu na kukuza ukuaji ,upanuzi na maendeleo ya viwanda  vidogo  na vya kati Tanzania bara  kwa  ajili ya  kuwezesha  watanzania  wengi kupata ajira .

Hivyo  alisema  pamoja na shughuli  hizo  limekuwa likitoa ushauri  wa fedha na  mikopo ambayo inalenga  kukuza biashara  na viwanda  vidogo  vinavyoanzishwa  au  vilivyoanzishwa  tayari  lakini vinahitaji  mikopo ili  kukua  Zaidi.
Kasesela  alisema  kutokana na taarifa  aliyofikishiwa na meneja  wa SIDO mkoa ilionyesha  kuna  malimbikizo mengi ya  mikopo kwa  kuwa na  wadaiwa  sugu  wengi  Zaidi  na  pesa  nyingi  ipo  nje .

Alisema  katika  mikopo  hiyo  ipo  mikopo ya  mtu moja  moja na vikundi  na  kuwa  kwenye taarifa  ya  SIDO kuna  wadaiwa 891 wamelimbikiza  jumla ya  shilingi 293,380,925 huku    wadaiwa binafsi  wapo  167  ambao  wanadaiwa jumla ya shilingi 181,396,500 na  vikundi 15 vyenye  wanachama 721 vinavyodaiwa jumla ya  shilingi 111,984,425 ndani  yake  vipo  vikundi  hivyo  viwili  vya Mungu ametenda .

Hivyo  alisema  kwa  kuanza  msako  huu utakaosimamiwa na ofisi yake amelazimika  kutoa  siku  6 hadi  jumatatu ijayo  mdhamini wa  vikundi  vya Mungu  ametenda awe  amejisalimisha pamoja na  wanachama wake  katika  ofisi yake na  wadaiwa  wengine ndani ya siku  saba  kuanzia  leo Mei 16 wawe  wamejisalimisha  ofisini  kwake na  kuanza  kurejesha  mikopo  hiyo .

“ Nawaagiza  wakopaji  wote  kupitia  vyombo vya  habari  popote  walipo ndani ya  wilaya ya  Iringa ama  mkoa ama  wawe  nje ya  mkoa huu  waanze kujisalimisha  kwa  kulipa madeni kabla ya kutangaza majina yao na  picha  zao katika  vyombo  vya habari na wapo  wengine ni  viongozi  wakubwa katika jamii ila katika  hili watatusamehe  lazima  walipe madeni “

Meneja  wa  SIDO mkoa wa Iringa  Francisca Simon alisema  kuwa  wameendelea  kuwasaka wakopaji  hao  kwa  kutumia  madalali ila  baadhi ya madalali  wamekuwa  si waaminifu  badala ya  kuwataka  wakopaji  kulipa  mikopo yao  kupitia akaunti  ya SIDO  wamekuwa  wakipokea  pesa  mkononi na  kula na  kuwa  wapo  baadhi ya madalali  wanawasaka  kwa kukiuka taratibu walizokubaliana .

Pia  alisema kukosekana kwa  uaminifu kwa baadhi ya madalali kumechangia   wakopaji  wasumbufu  kufanya marejesho kwa  wakati na  kuwa  sasa  wameweka  dalali  mwingine ambaye  hatapokea  hata  senti  moja  toka kwa  wadaiwa  hao.

Ofisa  mikopo wa SIDO  mkoa wa Iringa  Neserian  Laizer  alisema  kuwa  mikopo  hiyo  ya  serikali masharti yake  huwa nafuu  tofauti na  mikopo ya  taasisi  nyingine ila  hata  hivyo  wakopaji  huwa  wanakuwa na dhamana  na  kutolea  mfano  vikundi  vya Mungu  ametenda  ambavyo  kiongozi wake  aliweka  dhamana shamba  lake la  miti  pamoja na nyumba na  kuwa mwanzo  walifanya  vizuri ila  mara ya  pili  wameshindwa  kurejesha  mikopo  hiyo.

Alisema  kuwa   vikundi vya  Mungu  ametenda  ni  vikundi ambavyo  awali  vilikuwa  vikifanya  vizuri na  kukopeshwa  zaidi ya  mara mbili na kurejesha  kwa  wakati  ila  awamu ya  mwisho  wameshindwa  kurejesha kwa madai  wanachama  wamekimbia  Afisa biashara  wa  SIDO mkoa  wa Iringa  Niko Mahinya alisema  kuwa  kupitia  mikopo  hiyo  baadhi ya  wateja  waaminifu  wameweza  kuboresha  biashara  zao na  kuwa  lengo  moja wapo  la  SIDO  kuendelea  kuunga mkono jitihada za  serikali  katika  kuwawezesha  mikopo  ili  kuelekea uchumi  wa  viwanda.

Hata  hivyo  alisema SIDO  mkoa  wa Iringa  imeanza  kuwafikisha  wakopaji  hao  sugu mahakamani  na  wataendelea  kufanya   hivyo  kwa  wote  ambao ni  wadaiwa  sugu  hawajalipa  mikopo kwa  mujibu  wa  taratibu  walizokubaliana.0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE