May 15, 2018

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA IRINGA LAMPONGEZA SALIM ASAS,DC KASESELA ASEMA RAIS DKT JPM KAMPONGEZA SANA MBUNGE MSIGWA ..............

Madiwani  wa  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  wakiomba  dua  kabla ya  kuanza  kwa  baraza  leo
Diwani wa kata ya Mivinjeni Frank  Nyalusi  akitoa pongezi  kwa  kada  wa  CCM  Salim Asas  kwa kujitolea  kusaidia maendeleo  Iringa
Mstahiki  meya  Manispaa ya Iringa  Alex  Kimbe kushoto  akiwa na katibu  wa  baraza la madiwani  Omary  Mkangama leo  kabla ya kuanza  kikao cha  baraza la madiwani
Katibu  wa  kikao  cha madiwani Omary  Mkangama  ambae ni kaimu  mkurugenzi Manispaa ya  Iringa  akisoma  agenda za  kikao ,kulia  kwake ni Meya  Kimbe na kushoto kwake ni DC  Iringa  Richard Kasesela
Meya  Kimbe  akiongoza  kikao  hicho
diwani  wa  viti maalum  CCM  Dola Nziku  akichangia  katika kikao  hicho  leo
Meya  na kaimu  mkurugenzi  wakiteta  jambo wakati  akikao  kinaendelea
Na  MatukiodaimaBlog

BARAZA  la  madiwani  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa limewapongeza  wadau  mbali mbali  wa  maendeleo  katika Manispaa hiyo  ikiwemo  familia ya  mjumbe wa Halmashauri  kuu ya  chama  cha MapinduziTaifa  (NEC) Salim  Asas   kwa  kujitolea  kujenga wodi la  watoto  wanaozaliwa  kabla ya  wakati .

Akitoa pongezi  hizo  kwa niaba ya baraza la madiwani leo  diwani wa kata ya Mvinjeni Frank  Nyalusi (Chadema )  alisema  kuwa  pamoja  na kuwa familia   hiyo ya  Asas  ni makada wa CCM  ila  kazi  inayofanywa na  familia  hiyo hasa katika Manispaa ya  Iringa  si kazi ya  kichama ni kazi  yenye  sura ya  kimaendeleo  mapana kwa Halmashauri  hiyo ya inayoongozwa na  Chama cha  Demokrasia  na maendeleo (chadema) .

" Naomba  nitumie  nafasi  hii kupitia  kikao  hiki cha baraza la madiwani  kumpongeza  sana  Salim  Asas  kwa  michango mbali mbali ya  kimaendeleo  ambayo  ameendelea  kuisaidia  Manispaa  yetu  na suala  hili  halina  chama  kwani  wanaokwenda kulazwa  katika wodi  alilojenga katika  Hospitali  yetu ya  rufaa ya  mkoa  wa Iringa ni  wananchi  wote  walio na  vyama  na  wasio na vyama "

Hivyo  alisema  suala la  kupongeza  mdau wa maendeleo  anayeisaidia  Manispaa  hiyo  kupiga hatua  ni  la msingi  zaidi  na kuomba wadau   wengine  na  Asas  kuendelea  kusaidia maendeleo ya Manispaa ya  Iringa kwa  faida ya  wananchi wote .

Nyalusi  alisema  tayari  wamekwisha  mwandikia  barua  ya  kumpongeza na  kutambua  mchango  mkubwa  ambao  ameendelea  kuufanya katika  kusukuma  mbele  maendeleo ya  Manispaa ya  Iringa huku  akimpongeza  mbunge  wa   jimbo la  Iringa mjini mchungaji  Peter  Msigwa  (chadema)  kwani  kupitia  fedha za mfuko wa  jimbo Manispaa ya  Iringa  imeendelea  kufanya  vizuri  katika  miradi  mbali mbali.

Kwa  upande  wake  Msitahiki  meya wa Manispaa ya  Iringa  Alex  Kimbe  pamoja na kuungana na  diwani  Nyalusi  kupongeza  mdau  Asas  kwa  michango  yake  bado  alisema  wanampango kama Manispaa  kumwandikia  barua  nyingine ya  kumpongeza  huku  akiwataka  madiwani  wa  CCM  na  Chadema kuendelea  kufanya kazi  za  kuwatumikia wananchi wanapokuwa katika  vikao  vya madiwani  badala ya  kuleta mivutano ya  kiitikadi katika  vikao   vya madiwani .

Kimbe  alisema  iwapo madiwani  watakuwa  kitu  kimoja na kuja na hoja  za  kuwapigania  wananchi badala ya  kupinga kila jambo  kutokana na itikadi za kisiasa watakuwa  wanawachelewesha  wananchi  kupata maendeleo  na  kuwa  pamoja na kazi kubwa  inayofanywa na kada wa CCM Asas katika  kusaidia maendeleo ya Manispaa ya  Iringa bado  wao kama madiwani  wanaotokana na Chadema  wanakipongeza  CCM kwa  kusaidia mashine za kufulia  nguo katika Hospitali ya  Manispaa ya  Iringa na  kuomba  wanapopata  zaidi  misaada kwa ajili ya wananchi  kuendelea  kufanya  hivyo.

Aidha  meya  huyo  alisema   kuwa  wapo  baadhi ya madiwani  wanaohoji  juu ya kazi ya mfuko wa  jimbo la  Iringa mjini ila  pesa  hizo  zimekuwa  zikitumika kwa  utaratibu mzuri  wa  kuunga  mkono miradi mbali mbali ya  wananchi pasipo  upendeleo na  kata  moja  wapo  ambayo  imefaidika na  pesa za mfuko wa  jimbo ni kata ya Nduli ambayo  diwani  wake ni CCM.

Akielezea  kuhusu  hoja  ya madiwani wa CCM na Chadema ambao  waliungana  jana  kutaka  sheria  za  mipango miji  kubadilishwa  ili  wananchi  wa Kitanzini na Mshindo  waruhusiwe  kubarabati  nyumba  zao kutokana na nyumba  hizo  kuchakaa ila  wanabanwa na  sheria  inayozuia  ukarabati na  kutaka  wajenge  maghorofa  ,alisema kuwa  suala  hilo ni kisheria  na lilipitishwa na madiani  hivyo kama  wanaona  lina  shida  ni  vema  kupeleka hoja binafsi  katika baraza  na si vinginevyo.

Awali  diwani  wa kata ya  Mshindo Ibrahim Ngwada  (CCM) , diwani  wa Makorongoni  Raphael Ngulo  (Chadema)  na diwani wa kata  ya  Kitanzini Mahadhi  Hepautwa  (CCM)  waliomba  kikao  hicho  kubariki  eneo la  Kitanzini na  Mshindo  wananchi  wao  waruhusiwe  kukarabati  nyumba  zao  hoja  ambayo ilileta  mvutano  mkubwa na  kupelekea  mkuu wa  wilaya  ya  Iringa Richard Kasesela ambae  alikuwa mualikwa katika  kikao  hicho  kushauri  madiwani hao  kama  wanaona  hoja  hiyo ina uzito  wake  kupeleka  hoja  binafsi  katika  kikao  ila  sio  kuvunja  sheria  zilizopitishwa  na  wao  wenyewe .

Wakati  huo  huo baraza  hilo la Madiwani  limekitaka  CCM  Iringa mjini  kuvuta  subira  juu ya  eneo lao la uwekezaji wa kituo cha Mafuta  eneo la  Saba saba  ambalo  wamekuwa  wakilalamika  kuwa  Halmashauri ya  Chadema  imezuia  ujenzi huo .

Kwa mujibu  wa Meya  Kimbe  alisema  suala  hilo  lipo katika mchakato  kwa  kushirikisha  wataalam  na kuwa  muda  ukifika  wa  wataalam  kumaliza  kazi yao  CCM wataruhusiwa  kuendelea na uwekezaji  huo wenye  tija kubwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa.
Akitoa  salam  za  pongezi  za Rais Dkt John Magufuli  katika  kikao  hicho mkuu  wa wilaya ya  Iringa Kasesela   alisema  kuwa ,Rais  amepongeza  Manispaa ya  Iringa kwa  usafi  pamoja na  kumpongeza  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa kwa kazi  nzuri anayoifanya  pamoja na hoja  zake  nzuri  alizozitoa  mbele  yake katika  chakula  cha pamoja  kati ya  viongozi na wadau  mbali mbali  wakati wa ziara  yake  mkoani Iringa .

"  Mheshimiwa  Rais amesema  atakuja  tena  Iringa na  amempongeza  sana  mbunge  mchungaji Msigwa na ameahidi kuendelea  kumuunga mkono katika kuwatumikia  wananchi wake

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE