May 7, 2018

AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA ,MKANDARASI WA UKUMBI WA BILIONI 8.8 AKAMATWA

Kamanda  wa  polisi mkoa  wa  Iringa wa  Iringa Juma  Bwire  na kamanda wa  takukuru  mkoa  wa Iringa Aidan Ndomba  wakitoa  taarifa ya  kukamatwa wa mkandarasi  aliyeagiza  Rais Dkt John Magufuli  akamatwe  na  wenzake
..............................................................................................................................................
 Na  MatukiodaimaBlog

ZIKIWA  zimepita  siku sita   toka   Rais  Dkt  John  Magufuli  kuagiza  vyombo vya  ulinzi na  usalama  mkoa  wa  Iringa kuwakamata   aliyekuwa  mkuu wa  chuo   cha  elimu Mkwawa  Prof Pak Mushi na  mkandarasi  aliyehusika  katika  ujenzi  wa ukumbi  wa bilioni 8.8  katika  chuo cha Mkwawa Iringa ,tayari jeshi la  polisi mkoa  wa  Iringa  limemkamata  mkandarasi wa  ujenzi huo .

Wakizungumza na  waandishi  wa  habari leo   kamanda wa  polisi wa mkoa  wa  Iringa Juma  Bwire   na kamanda  wa  taasisi ya  kupambana na  rushwa  nchini (Takukuru ) Aidan  Ndomba walisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo  Godwin shanMa wa  kampuni ya  Engineering  Service  Ltd  mkazi wa Gangilonga  mjini hapa alikamatwa  toka   Mei  3 mwaka  huu ikiwa ni  siku moja  toka  Rais  alipotoa  agizo hilo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE