May 14, 2018

ABDUL NONDO AMKATAA HAKIMU ANAYESIKILIZA KESI YAKE

Mawakili  wa  Nondo  Kambole   kushoto na  Luoga kulia  wakimsikiliza  mratibu  wa THRDC Onesmo  Olengurumwa mwenye  miwani katikati leo baada ya  mahakama  ya hakimu  mkazi mkoa  wa  Iringa  kuahirisha  kesi hiyo  hadi kesho  kutwa katikati  mwenye kitambulisho  shingoni ni Abdul  Nondo
Nondo  akizungumza na  wananchi wa Iringa  waliofika  kusikiliza kesi yake
Olengurumwa  katikati akitoa  namba  yake
Nondo  akisalimiana na  wananchi  waliofika kusikiliza  kesi yake
Nondo  akitoka mahakamani
Nondo  akiwa  ameongozana na mratibu wa  THRDC  Onesmo  Olengurumwa   katikati na  wakili  Luoga kushoto
Mawakili wa Nondo wakizungumza na wanahabari  leo mjini Iringa
Olengurumwa  katikati  akifafanua  jambo
Nondo  akizungumza na wanahabari leo
Mratibu  wa  THRDC  Onesmo  Olengurumwa  akimsikiliza  Nondo  wakati akizungumza na wanahabari  leo
Mratibu  wa  THRDC  Onesmo  Olengurumwa  katikati  akiwa na  mawakili  leo
Olengurumwa  akiwa na  wakili wa Nondo Kambole  kushoto 
Na  MatukiodaimaBlog

KESI ya  mwenyekiti wa mtandao wa Wanafunzi wa  vyuo vikuu Tanzania (TSNP)  Abdul Nondo anayedaiwa  kujiteka imeingia  katika sura  mpya  baada  ya mshitakiwa Nondo kuandika  barua ya  kumkataa hakimu John Mpitanjia anayesikiliza  kesi   hiyo kwa madai ya  kuwa karibu na mkuu  wa  upelelezi wa  polisi  mkoa  wa  Iringa (RCO). 

Wakili  anayemtetea  Nondo  Jebra Kambole aliiambia mahakama   hiyo leo   sababu  tano  zilizopelekea mteja  wake  kuandika  barua   hiyo  toka Mei 11  mwaka  huu  kumtakaa  hakimu   huyo kuwa  moja kati  ya  sababu ya  kupelekea  mteja  wake  kuandika  barua  hiyo  ni  baada ya hakimu anayesikiliza  kesi   hiyo  kuonekana akiingia katika  gari  la  RCO  Iringa na  sababu  nyingine  ambazo mteja  wake  ameona  haki  haitatendeka katika  utoaji  katika  kesi  hiyo .

Pamoja na hakimu  kuonekana  akiingia katika  gari la  RCO  Iringa  kwenda  sehemu  isiyojulikana  pia sababu  nyingine ni hakimu  kukutwa  alikaa na Paul Kisapo  ambae ni shahidi  wa  tatu katika  kesi na  sababu  nyingine ambazo mteja  wake  anaona  haki  haitatendeka.

Kwa  upande  wake  wakili  wake  wakili  wa  jamhuri  katika  kesi   hiyo Abel  Mwandalama  alisema  kuwa  amesikiliza  maelezo ya wakili  anayemtetea mshitakiwa  pamoja na  kupokea  barua  ya mshitakiwa ya  kumkataa  hakimu katika shauri  hilo  ila ameona hayana  msingi katika  kesi  hiyo.

Kwani  alisema  suala la  kujiondoa hakimu  ni la  kisheria  katika malalamiko  ambayo  nayaletwa na mshitakiwa  iwapo  yana  ushahidi  ila malalamiko ya mshitakiwa  hayana  ushahidi wowote  unaohusiana na madai  yake yote .

Alisema  kuwa mwenye  kesi  hiyo  upande  wa jamhuri  ni  mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)  na RCO  ni mpelelezi  tu wa  kesi hiyo  na  kuwa  hadi  sasa  hakimu  hajaonyesha  kuwa na maslahi  yoyote katika  kesi  hiyo na kuwa  malalamiko  ya  mshitakiwa  yamepanga kuchelewesha kesi hiyo .

"  Tunasema hayo kwa  kuwa April 19 mwaka huu shahidi wa tatu katika  shauri hilo alitoa  ushahidi  wake na  mshitakiwa  hakuandika  barua yoyote  na  hata  kesi hiyo  ilipokuja  Mei 10  mwaka  huu hakuna barua  iliyoandikwa  iweje  barua  hiyo  kuandikwa Mei  11 baada ya mahakama  hiyo  kukubali  vielelezo  vilivyotolewa  na upande  wa jamhuri  kutumika kama  ushahidi "

Wakili  huyo  aliiambia  mahakama  hiyo kutokana na  vielelezo  hivyo kupokelewa wamekuja na  hisia  kuwa haki  haitatendeka  kwani mshitakiwa katika lalamiko la kwanza  linalomkabili kuwa alijiteka  na  sio  alitekwa kama  alivyodai yeye na ndio maana  upande wa  jamhuri umekuja  na  ushahidi .

"  Kwa  misingi  hiyo ofisi ya  RPC  Iringa na  Dar es salaam   ilikuwa sahihi  kutoa  taarifa  juu ya  mshitakiwa kujiteka  na  walifanya  hivyo  kwa kutimiza  wajibu  wao  wa kazi  yao  hivyo tunaomba  mahakama  yako itoe majibu  baada ya  kusikiliza ushahidi pande  zote  mbili "

Alisema  hoja  yao ya  pili  inasema kuwa Hakimu huyo  alikaa na Paul Kisapo  ambae ni shahidi  wa  tatu katika  kesi  hiyo  japo  wameshindwa  kuleta  ushahidi  unaoonyesha uhalisia  wa hoja  yao .

 wakati  sababu  yao  ya  nne  inasema RCO  Iringa alikuwa katika  gari  moja  na  hakimu  huyo  wakienda  sehemu  isiyojullikana na  wameshindwa  kuleta  ushahidi  hata  wa namba za  gari  walilokuwa  nalo  . pamoja na  kuwa RCO  Iringa  sio mlalamikaji  katika  kesi hiyo .

Kuhusu  sababu ya  tano alisema kuwa ni  kuhusiana na malalamiko  ya upande wa jamhuri  ambayo  iliyawasilisha mahakamani hapo  kuwa mshitakiwa anafanya  mawasiliano na mmoja kati ya  mashahidi  wa  kesi  hiyo na  mahakama  ilitoa  mwongozo  kwa  kuzitaka  pande  zote  mbili kuacha kufanya   hivyo

"  Sababu  ambazo  zimeletwa  si sababu za msingi  za  wewe hakimu  kujiondoa katika  shauri  hili  kusikiliza   sababu  ambazo  zimeletwa ni  hofu ya  vielelezo G 7 na  8 ambavyo vilipokelewa na mahakama  hiyo  maombi  ambayo  yameletwa na mshitakiwa  yamelenga  kuchelewesha  haki  kutolewa  kwa wakati kwa  mtu  anayetaka  haki  katika  sababu  zote  sijaona  sehemu inayokulazimu kujitoa  jamhuri  tunaomba  uendelee na kesi hakuna  sababu za  kujitoa  tunaomba  leo  uendelee  kuwasikiliza mashahidi  wetu  wawili  ni hayo  tu"

Kwa  upande  wake hakimu  Mpitanjia  alisema baada ya  kusikiliza  hoja  za  pande  zote  mbili  juu ya barua ya  mshitakiwa  kutoka hakimu  kujitoa katika  shauri  hilo uamuzi  wa  kujitoa ama  kuendelea na kesi  hiyo  utatolewa Mei 16  mwaka  huu (keshokutwa )

Akizungumza  na  wanahabari  nje ya  mahakama  hiyo Nondo  alisema  amelazimika  kuandika barua  hiyo  kumkataa hakimu  kutokana na  kuwepo  kwa  dalili  za  haki  kutotendeka katika  kesi hiyo  .

Nondo  alisema jamhuri  sio  mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pekee  yake  kwani polisi ,wakili  huyo wa  serikali na hakimu huyo na  polisi   wote  ni jamhuri    hivyo kudai  kuwa jamhuri ni DPP  pekee  si  sahihi  hivyo  kutokana na hofu  ya  haki  yake  kutotendeka ameamua  kumkataa hakimu  huyo .

"  Kutokana na sababu  nilizozitoa katika barua  yangu leo  kuona  RCO  na hakimu  wanapanda  gari  moja na  ndio  wanahusika na kesi yangu mimi binafsi  lazima  niwe  na  wasi wasi "

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC Taifa, Bw. Onesmo Olengurumwa akizungumza na wanahabari  mahakamani  hapo  alisema  kuwa Nondo  amefanya  hivyo kwa mujibu wa  sheria  za  nchi na  kuwa  amefanya  hivyo  baada ya  kuona mwenendo  wa  kesi  hiyo  unakwenda tofauti na  alivyokusudia .

"  Kinachotakiwa hapa ni haki  kutendeka  pande  zote  mbili  bila kuwepo kwa  dalili za kuegemea  upande  mmoja  ninyi  mliopo  huku Iringa nanaweza  kuwa na picha nzuri  ya  jambo  hili kwani jamhuri ndio  iliyomshitaki  na  kumkamata  Nondo  leo  jamhuri  hiyo  hiyo  inakuwa na mahusiano na hakimu  anayeendesha  kesi  hiyo"

OleNgurumwa  alisema  toka mwanzo  polisi  ndio  ambao  walimkamata  na  kuchunguza na kumfikisha mahakamani   Nondo  hivyo kwa mazingira kama  hayo ni  vigumu  kwa  mshitakiwa  kumkubali hakimu ambaye anahisi  hawezi  kutenda  haki katika kesi  yake na  kuwa  wanachotaka  kuona haki inatendeka pande  zote  mbili .

Alisema  kuwa imani  ya THRDC  ni  kuona  hukumu  hiyo  ya Mei 16  juu ya malalamiko ya  mshitakiwa  inatenda  haki  kwa kupata  hakimu  mwingine  ambaye atasimamia  haki  katika  kesi hiyo

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE