April 3, 2018

WINNIE MANDELA KUZIKWA APRIL 14,2018


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa taarifa rasmi juu ya mazishi ya Winnie Mandela ambaye Taifa hilo linamtambua kama mama wa Taifa, aliyefariki April 1, mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia ya marehemu, Rais Ramaphosa amesema Winnie Mandela atazikwa kwa heshima zote za serikali na utamaduni wa Afrika Kusini hapo April 14, huku zikitanguliwa na shughuli zingine za mazishi kuanzia April 11.
Rais Ramaphosa ameendelea kwa kusema kwamba kama Taifa linatambua mchango wa Winnie Mandela, hivyo watampa heshima zote pamoja na watu wote wanaowatakia mema taifa la Afrika Kusini.
“Kwa ngazi ya serikali ya kitaifa, tumetangaza kuwa Winnie Mandela atakuwa na mazishi ya kitaifa rasmi. Tungependa kutoa shukrani zetu na shukrani zetu kwa wengi nchini kote na ulimwengu ambao wanatutaka sisi vizuri, "amesema Rais Ramaphosa.
Winnie Mandela alikuwa mke wa pili wa aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, na alikuwa ni mmoja wa wapigania uhuru wa watu weusi na kuendeleza harakati hata wakati viongozi wa ANC akiwemo Nelson Mandela wakiwa wamefungwa jela, kwa muda wa miaka 27.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE