April 20, 2018

WASICHANA WA MIAKA 14 WAPATAO 14,840 MKOANI IRINGA KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

Mkuu wa  mkoa wa Iringa akifungua  warsha ya  mafunzo kwa  wadau wa afya  juu ya  kuanza kwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa miaka 14  mkoani Iringa
Wadau  wa afya  wakiwa katika  warsha ya  mafunzo  ya  saratani ya  mlango wa kizazi
Kaimu  mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa kulia  akiwa na  wadau  wa  afya
Baadhi ya  washiriki wa warsha  ya  saratani ya  mlango wa  kizazi  wakiwa katika mafunzo

Viongozi mbali mbali wa  mkoa wa Iringa wakiwa katika  picha ya  pamoja

Na MatukiodaimaBlog
 WASICHANA wenye  miaka 14   wasiopungua  14,840  mkoani  Iringa  kufikiwa  na  huduma  ya chanjo ya saratani ya mlango  wa  kizazi .

Akifungua  warsha  ya mafunzo ya  siku  moja kwa  wanahabari   na wadau  wa afya  mkoani Iringa katika ukumbi wa  chuo   kikuu Hurua Tanzania mjini Iringa  ,mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa chanjo  hiyo itaanza  kutolewa  bure  katika  vituo na maeneo yote  ambayo yatabainishwa  kwa  ajili ya huduma   hiyo.
                                        
“Wizara  ya  afya  ,maendeleo ya  jamii ,jinsia na watoto  kwa  kushirikiana na wadau  wa chanjo  tumeambiwa  itaazisha  chanjo  mpya ya kuwakinga  na ugonjwa  wa  saratani ya mlango wa  kizazi  kwa  wasichana wenye  umri wa  miaka 14 kuanzia April 2018 nchi  nzima  na  serikali  imeamua  kuanza kutoa  chanjo  hii kwa  sababu saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa  kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine hapa  nchini”

Alisema  kuwa  saratani ya  mlango wa  kizazi  inachangiwa na  vitu vingi ikiwemo kuanza  kujamiana  katika  umri mdogo ,kuwa  na  wapenzi wengi  ,kuwa na ndoa za mitala ,kuzaa watoto  wengi  na uvutaji wa  sigara .

Hivyo  alitaka  wanahabari  mkoani Iringa  na  wadau  wa  chanjo  hiyo  kufanya kazi  ya  kuhamasisha  jamii  ili  kujitokeza  kwa  wingi kushiriki  chanjo  hiyo ambayo imewalenga  wasichana  wa  miaka  14 kwa  mwaka  huu 2018.

Mkuu  huyo wa  mkoa  alizitaja dalili  za saratani ya  mlango wa kizazi mara  nyingi  hujitokeza ikiwa imesambaa mwilini kuwa ni pamoja na   kutokwa  damu ya  hedhi bila mpangilio ,kutokwa na damu  baada ya  kujamiana ,maumivu  ya mgongo ,miguu  ama  kiuno , kupungukiwa au kukosa  hamu ya  kula ,kutokwa na uchafu  wenye rangi ya kahawia au wenye damu kwenye uke ,na maumivu ya  miguu au  kuvimba .

Masenza  alisema   kuwa  dalili  mbaya  zaidi  zinazoweza  kujitokeza  ni  pamoja na  kuishiwa damu ,figo kushindwa  kufanya kazi ,kupatwa na  fistula  na  uvimbe  wa  tezi .
Hivyo  aliwataka walengwa  wa chanjo  hiyo  kujitokeza  kupata  chanjo  na  kuepuka  upotoshaji  unaoweza  kujitokeza kwani  lengo la  serikali  ni  kupunguza  vifo  vya  akina  mama  vinavyotokana na  saratani ya  mlango  wa  kizazi  hivyo  kuanza  kutoa  chanjo   hiyo .
 Image result for Chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi
  Lengo hasa ya  kuanzisha  chanjo   hii ni kukinga mabinti  wetu kutokana na madhara  makubwa yanayoweza  kuwapata  ambayo husababisha  vifo vingi kwa wanawake  na hivyo  kuboresha afya  za jamii ya wanawake  watanzania  kwa  ujumla 

Alisema  kutokana na  uzoefu  uliopatikana  wakati wa majaribio  utoaji wa chanjo hii  mkoani Kilimanjaro  chanjo  hiyo  itatolewa  katika  utaratibu wa kawaida kwenye  vituo  vya  kutolea huduma za chanjo,baadhi ya  shule zitakazochaguliwa ,baadhi ya maeneo katika jamii ambapo zitatolewa kwa njia ya  mkoba japo  asiwepo  mtu atakayetoza gharama  katika  chanjo  hiyo .
                          
Mkuu  huyo wa mkoa  alisema  kuwa kwa  Tanzania ,saratani ya  mlango wa  kizazi ni ya kwanza kwa  vifo ikifuatiwa na saratani ya  matiti  na kuwa  saratani hizi  mbili kwa pamoja  husababisha  zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote  vya akina mama  vitokanavyo  na saratani .

Kuwa  idadi  hii ni  kubwa sana  hivyo  juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika  katika kupunguza vifo hivi  pia  aisema takwimu  zinaonyesha  ni asilimia  5 tu  ya fedha za saratani duniani  zinatolewa katika nchi  za  kusini mwa jangwa la  sahara  hivyo   hakuna budi kutumia  vyanzo vyetu  vya ndani  pamoja  na kushirikiana na wadau mbali mbali  katika  kutoa  huduma  za chanjo .
Image result for Chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi
“ Napenda  kuchukua nafasi hii  kuwashukuru wadau wetu wa  huduma za chanjo likiwemo shirika la Gavi ,pamoja na  serikali yetu chini ya  Rais Dkt  John Magufuli kwa  kuwa mstari wa  mbele  kufadhili  huduma  za  chanjo ikiwemo ya  kuzuia dondakoo,kifaduro ,homa ya  utiwa mgongo ,homa ya  ini ,pepopunda ,NOmonia ,kuzuia kuhara , surua na  Rubella na sasa  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi “

 Aidha  mkuu  huyo wa mkoa  aliwapongeza wadau  mbali mbali  katika  kufanikisha utoaji   bora wa huduma za  chanjo nchini  likiwemo shirika la GAVI, shirika la afya  ulimwenguni (WHO),shirika la  kuhudumia watoto (UNICEF,) CHAI, JSI, PATH, AMREF, JHPIEGO, pamoja na wadau wengine wote .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE