April 12, 2018

WANAUME WANAOPIGWA NA WAKE ZAO NJOONI KWANGU -DC KASESELA


MKUU  wa   wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela (pichani)amewataka  wanaume wanaopigwa na  wanawake  wake  zao ama wanawake wanaopigwa na  waume  zao zao kufika  ofisini kwake  ili awawajibishe  kisheria.

Akizungumza  katika  warsha ya ujasiliamali iliyoandaliwa na UVCCM Iringa mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  kuwa kumekuwepo  unyanyasaji na ukatili wa  hali ya juu unaoafanywa na  baadhi ya  wanaume  kupiga  wake  zao pia baadhi ya  wanaume kupigwa na  wake  zao jambo  ambalo halivumiliki .

"Nasema  ni marufuku kwa  mwanaume  kumpiga  mke  wake  katika wilaya  yangu ya  Iringa niwaombe  wanawake  wote  wanaiopigwa na waume  zao  fikeni ofisini kwangu ili  mimi  niwakamate  hawa  wanaume na  kuwafikisha  polisi "

Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  pamoja na  wanawake  kuongoza kwa  kupigwa na waume zao takwimu  zinaonyesha   wapo  pia   wanaume  ambao  wamekuwa  wakinyanyaswa na  kupigwa na wake zao ila  wamekuwa  wakiendelea   kuvumilia maumizi na mateso  pia kama  wapo  wasiogope kujitokeza .

Alisema  katika  ofisi yake  ameendelea  kupokea  kero  mbali mbali za  wananchi  kila jumatatu na  kuwa katika  suala  hilo la ukatili dhidi ya wanawake  wakati  wote  wanawake  wanaopigwa na waume zao wasingoje  siku  hiyo  wafike  kila  wanapopigwa .

Pia  Kasesela  aliwataka  wakazi  wa Iringa kuendelea  kuwafichua  wale  wote  wanaoendekeza  vitendo vya  ukatili kwani suala   hilo  halikubaliki ndani ya  wilaya  yake  huku  akionya  wale  wote  wanaonyanyasa  watoto .

Wakati huo  huo  mkuu  huyo wa  wilaya  amepiga marufuku Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa kuwanyanyasa  wafanyabiashara  wadogo wadogo (machinga  )  bila ya  kuwatengea maeneo ya  kufanyia  kazi na  kuwa  kuendelea  kuwanyanyasa  pasipo kuwatengea maeneo ni  kosa .

Aidha  mkuu  huyo wa  wilaya alipiga marufuku Manispaa ya  Iringa  kuagiza  sare  za mbio  za  mwenge wa Uhuru nje ya mkoa  wa Iringa na  kutaka sare  za  mwenge kwa  mwaka huu zitengenezwe na  vijana  zaidi ya 400  waliopewa  mafunzo ya  ujasiliamali ya  utengenezaji wa batiki .

" Kumekuwa na utaratibu wa Manispaa ya  Iringa  kutumia  pesa  nyingi kwa  kuagiza  sare za  mwenge Dar es Salaam sasa ninaagiza mwaka  huu katika  mbio za mwenge  zitakazo kimbizwa Manispaa ya  Iringa sare za  Mwenge zitumike  batiki ambazo zinatengenezwa na hawa  wajasiliamali  wetu"

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE