April 30, 2018

WANAHABARI KUTUMIKA KUTANGAZA MISITU NCHINI - PROF SILAYO

Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Prof Dos Santos  Silayo  akizungumza na  wataalam wa  kitaifa    wa upimaji  na uhakiki wa  ramani za  misitu  ya umma  ya  asili na  ya kupandwa leo  katika  shamba la  Sao Hill Mufndi
Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Prof Dos Santos  Silayo akisisitija  jambo
Baadhi ya  wataalam  wa kitaifa wa  upimaji  na uhakiki wa ramani za  misitu  ya  asili na ya kupandwa  ya umma wakimsikiliza mkurugenzi  wa TFS leo
Wataalam  wa  upimaji  misitu ya  umma  ya  asili na ya kupandwa  wakimsikiliza Prof Silayo
Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Prof Dos Santos  Silayo  akizungumza na  wataalam wa  kitaifa    wa upimaji  na uhakiki wa  ramani za  misitu  ya umma  ya  asili na  ya kupandwa leo
Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Prof Dos Santos  Silayo  akizungumza na  wataalam wa  kitaifa    wa upimaji  na uhakiki wa  ramani za  misitu  ya umma  ya  asili na  ya kupandwa leo mjini Mafinga
Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Prof Dos Santos  Silayo  katikati  waliokaa akiwa na  vingozi wa Msitu wa Taifa wa Saohill na   wataalam wa  kitaifa    wa upimaji  na uhakiki wa  ramani za  misitu  ya umma  ya  asili na  ya kupandwa leo  katika  shamba la  Sao Hill Mufndi
Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Prof Dos Santos  Silayo  akisalimiana na wataalam wa  kitaifa    wa upimaji  na uhakiki wa  ramani za  misitu  ya umma  ya  asili na  ya kupandwa leo  katika  shamba la  Sao Hill Mufndi
Prof  Silayo  akiwa na mmoja kati ya  wataalam wa upimaji wa misitu na uhakiki wa  ramani  za  misitu ya  umma
Wataalam  wa  upimaji wa  misitu ya  umma  wakiwa  katika  shughuli  hiyo leo msitu wa  SAo Hill
Wataalam  wa  upimaji wa  misitu ya  umma  wakiwa kazini


..............................................................................................................
Na  MatukiodaimaBlog 

MKURUGENZI  Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)Prof Dos Santos Silayo amesema utaratibu unaandaliwa wa w   wanahabari  nchini  kutumika  kutangaza   misitu hapa  nchini nchini  .

Akizungumza   leo   katika  ofisi  za  msitu  wa  Sao Hili  wilayani  Mufindi  baada ya  kuwatembelea  timu  ya wataalam  kutoka  taasisi  mbali  mbali  nchini  kwa  ajili  ya  upimaji   na uhakiki  wa ramani  za  misitu ya Taifa  ya asili  na ile  ya  kupangwa   alisema   kuwa  kumekuwepo na  wanahabari  wazuri  nchini ambao wamebobea katika  masuala ya  uandishi wa habari za mazingira na  iwapo  watatumika    vizuri  ni  rahisi  kwa  misitu  yetu  kutangazaka  zaidi .

Hivyo  alisema  kupitia  wanahabari hao  na  wasanii  nchini  wanaweza  kutumika  kutangaza  misitu  iliyohifadhiwa  na  misitu ya  kawaida  ili  kuwavuta  watalii kutembelea  misitu  .

  Tanzania  ni nchi  ambayo  imebarikiwa  kuwa na rasmimali  nyingi  kwa  kuwa  na  misitu katika  sehemu  kubwa ya  nchi  asilimia  karibu  54  ya  nchi  ni  misitu ya  asili  na ya  kupandwa  na  maeneo hayo  yanavivutio  vingi  zaidi  kwanza  kuna bainuai  ya wanyamapori ,mimea  na maporomoko ya  maji na kama itatangazwa  vizuri ni  sehemu  nzuri ya utalii “

Alisema  tayari   jitihada za  kuyatangaza  maeneo hayo imeanza kufanyika  pamoja na  kuwakaribisha   wawekezaji  kufika  kuwekeza katika maeneo hayo na  njia nzuri  ya kutangaza ni  kuwatumia  wanahabari na  wasanii kufikisha  ujumbe wa  uhifadhi na kuhamasisha  waandaaji  wa sanaa  na wengine  kutumia  misitu  hiyo  badala ya  kwenda  kutumia  misitu ya  nje ya  nchini .

 Kuwa  kwa  kutumia  misitu ya  ndani ni  fursa  ya ukuzaji wa  uchumi  wetu  kupitia  sekta ya  utalii kwani  misitu ya  Tanzania  ina sifa  nzuri  zaidi  na inavutia  sana   hivyo  wakati umefika  wa  kutumia  misitu   hiyo  kuvuta  watalii  hapa  nchini .

Alisema  ni  wajibu wa taasisi  mbali mbali  zinazohusika na  misitu na mazingira   kutumia  vyombo vya  habari  katika  utangazaji wa misitu  na  vivutio  vya  utalii na kuwa kwa  upande wa  ofisi yake  itawekeza  zaidi katika  eneo la kutumia  vyombo  vyote vya habari kama  magazeti , radio ,TV  na mitandao ya  kijamii katika  kufikisha ujumbe  kwa  jamii .

Prof  Silayo  alisema  kuwa  kwa  hivi  sasa  matukio ya  moto katika  misitu  iliyohifadhiwa ,misitu ya  asili na  ile ya  kupandwa   yamepungua  baada ya  serikali  kupitia  TFS   kufundisha  watalaam  ambao  walikwenda  kujifunza  Afrika  ya  kusini kujifunza kutambua  alam  za  moto  pamoja na  kujifunza  jinsi ya  kuandaa vikundi  vya  kijamii  kwa  ajili ya misitu  hiyo  isikumbwe na  matukio ya moto.

“ Kupitia  mafunzo  ya  uandiji  vikundi  tumefanikiwa  kuanzisha  vikundi   vinayozunguka  msitu wa  Sao hill na  misitu mingine  na kazi yao  kubwa  kupambana na  moto  pindi  unapotoke  lakini  kama  serikali  tumewekeza  kwa  kununua  mtambo wa kutambua moto  unaoanza  kuwaka katika  misitu  kote  nchini na  kutoa taarifa kwa  njia ya simu na njia  nyingine  kujulisha  kuwa  eneo  furani  kuna moto  unawake  

Alisema  uwekezaji wa Tenknolojia  umesaidia  sana  kupunguza matukio ya  moto na  siku  za  hizi karibuni  wamekusudia  kuanzisha  jeshi la  kupambana na  moto katika maeneo ya   hifadhi za  misitu na kazi yao  ni  kuzima  moto kwa  haraka  pindi  unapotokea  .

Akizungumza zoezi la  upimaji wa misitu ya umma alisema  kuwa  wamelazimika  kutuma  kikosi kazi hicho  ili  kuzunguka  nchi  nzima  kupima  misitu  yote ya  umma ya  kupandwa na ile ya  asili  ili  kuweka  mkakati wa  kuisimamia  kwa  kujua maeneo  halisi  yana  ukubwa  gani  pia  kupitia  ramani za  maeneo yote ya  misitu ya  umma .

Hivyo  aliziomba  Halmashauri za wilaya  nchini  kuendelea  kusimamia  misitu ya  umma  na  kuwapongeza  wakuu wa  wilaya ya  wakurugenzi kwazi kubwa ya  usimamizi wa  misitu ya  umma na kuwa changamoto  iliyopo ni  baadhi ya  halmashauri  kuingiza  siasa  katika  usimamizi wa misitu  .
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE