April 4, 2018

VODACOM YAWATOA HOFU WATEJA WAKE WA LUKU KUPITIA M-PESA


Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imewatoa hofu wateja wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwamba itaendelea kutoa huduma ya ununuzi wa umeme (LUKU) kupitia mfumo wa malipo wa serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG).
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya kampuni hiyo, hatua hiyo inatokana na mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuhusu kuanza kutoa huduma ya kununua umeme kwa kupitia mfumo wa Serikali wa GePG.
“Vodacom Tanzania inapenda kuwatoa hofu wateja wake kwamba wataendelea kupata huduma ya kununua umeme ya LUKU kupitia Vodacom M-Pesa kama ilivyokuwa mwanzo.
“Mfumo mpya utaiwezesha Tanesco kuunganisha mauzo moja kwa moja kutoka kampuni nyingine za simu na benki kwenda GePGi ikiwa ni matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.
“Aidha, kutakuwa na ongezeko la asilimia 1.1 ya gharama halisi anayotozwa mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa,” imesema taarifa hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE