April 26, 2018

ULINZI MKALI WATAWALA MJI WA IRINGA KUWASAKA WAANDAMANAJI , RPC ASEMA HADI SASA IRINGA SHWARI

Wanafunzi  wa  chuo  cha  Ruaha  mkoani Iringa (RUCU)  wakipita  jirani na gari  la washawasha  lililoegeshwa  langoni mwa  chuo   hicho   ili kupambana na  waandamanaji  iwapo  wangefanya  hivyo ,katika  chuo  hicho  ulinzi umewekwa na vyuo vingine ila hadi  sasa  chuo  hicho wanafunzi wawili wa  sheria  wanashikiliwa kwa  kumahasisha maandamano  mitandaoni
FFU  wakipita  mitaani  mjini  Iringa
Ulinzi  wa   wawekwa kila kona
FFU  wakiwa katika  ulinzi mjini Iringa  leo

Mwanafunzi  wa  chuo  cha  RUCU  Iringa  ambae  jina lake  halikuweza  kufahamika  akipiga stori na askari wa FFU  wakati  akielekea chuoni  kuendelea na masomo  yake leo
magari ya  FFU yakiwa langoni mwa chuo cha RUCU Iringa .

WANANCHI  wa mji wa Iringa  leo  wameendelea na  shughuli zao kama ilivyo  siku  zote  huku jeshi la  polisi  likiwa  limeweka ulinzi mkali kila kona ya  mji  huo kuwabana wale  ambao  watajaribu  kuitikia  wito wa Mange Kimambi kwa  kuandamana  leo.

 Matukio daima  imeshuhudia  ulinzi  mkali  ukiwe  umewekwa katika  maeneo mbali mbali ya  vyuo vikuu kikiwemo chuo cha Ruaha (RUCU)  ambako  wanafunzi wake  wawili  walikamatwa  wiki  hii kwa  kuhamasisha maandamano  katika makundi ya  WhatssAp  .

 Hata  hivyo  baadhi ya  wananchi  wa mji wa Iringa  waliozungumza na mtandao wa matukiodaima akiwemo Omary Ally , Yohana  Kalinga  na  Asha John  walisema hata  bila  ya polisi  kuweka ulinzi huo hakuna mtu ambaye  amekubali  kuacha shughuli zake na kuingia barabarani  kufanya maandamano hayo ambayo kwao hayana  tija.

" Leo  mtu  anatuhamasisha kwa mitandao  kuwa  eti  tuandamane  kumpinga Rais Dkt  John Magufuli , wakati  sisi wenyewe  tulimchagua na  tulimpenda  ukilinganisha na  wagombea  wengine tunasema hatudanganyiki kufanya  ujinga   huo sisi tuna shughuli nyingi za  kufanya maandamano si mahitaji yetu "

Aidha  wananchi hao  walipongeza  jeshi la  polisi  mkoa wa Iringa kupitia kamanda wa  polisi Juma Bwire kwa  kuchukua tahadhari hiyo  kwani  bila  kufanya hivyo  wapo ambao  wangeweza  kuandamana  ili  kutumia maandamano  hayo kufanya  uharifu ama  mambo yao ya  kisiasa .
Image result for RPC Iringa Bwire
Kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa Juma  Bwire  alisema hali  toka  asubuhi mji wa Iringa  upo  safi  hakuna tukio lolote la  uvunjifu wa amani na kuwa hadi jioni ulinzi utaendelea  kuwepo na kuwataka  wananchi  kutoa  taarifa  kwa mtu ama  kikundi cha  watu kinachohamasisha ama  kufanya maandamano kwa  siri .

"Tunasawaka  hata  wanaotumiana  jumbe  mbali mbali kwenye mitandao ya  kijamii  kuhamasisha ama  kuunga mkono maandamano hayo  tutawasaka  popote  walipo tumejipanga  ombi langu  kila mwananchi aendelee na  shughuli yake kwa amani na utulivu na wajiepushe na watu wanaofika katika maeneo yao ya kazi  kufanya  uchochezi woworte  vijana  wetu  wapo  mitaani kwenye  vijiwe na  popote  ulipo   wapo "
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE