April 18, 2018

TAARIFA YA MAGARI YA MAFUTA KUWAKA MOTO USIKU HUU IRINGA

Habari zilizotufikia muda huu was saa 2:45 usiku zinadai kuwa kuna ajali ya magari mawili ya Mafuta yanateketea kwa moto .

Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza Mtandao huu wa matukiodaima kwa njia ya siku kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Ulete wilaya ya Iringa vijijini kwenye barabara kuu ya Iringa - Mbeya.

Hata hivyo wamedai gari la zimamoto bado halijafika huku polisi wakiwepo eneo la tukio kuweka ulinzi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire ameuthibitishia Mtandao wa matukiodaima kutokea kwa tukio hilo na kuwa taarifa zaidi ataitoa Mara baada ya askari waliokwenda eneo la tukio kurejea.

Endelea kuwa nasi matukiodaima tutakujuza

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE