April 20, 2018

SERIKALI YASISITIZA HAKUNA UPOTEVU WA TSH TRILIONI 1.5


Image result for naibu  waziri wa  fedha
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali imesema hakuna upotevu wa shilingi Trilioni 1.5 kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya wanasiasa kufuatia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioshia June, 2017.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu hoja za kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali Shilingi Trilioni 1.51.

"Shilingi Trilioni 1.51 zilizodaiwa kutooneka kwenye matumizi ya Serikali zilitokana na mchanganuo ufuatao; matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva shilingi trilioni 0.6979, mapato tarajiwa (receivables) shilingi trilioni 0.6873, mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya serikali ya Zanzibar shilingi trilioni 0.2039 na kufanya jumla ya shilingi 1.5891," alisema Dkt. Ashatu.

Aliendelea kwa kusema, fedha iliyotolewa ni zaidi ya mapato (bank overdraft) ni shilingi trilioni 0.0791 ambapo fedha zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ni shilingi trilioni 1.51 .

Amesema, kwa mchanganuo huo, ni dhahiri kwamba kwa mwaka 2016/2017 matumizi ya Serikali yalikuwa makubwa kuliko mapato kwa shilingi bilioni 79.07 ambazo ni Overdraft kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha amesema, utaratibu wa kutoa fedha zaidi ya mapato (Overdraft facility) uko kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

"Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ipo makini na haiwezi kuruhusu upotevu wa aina yoyote wa fedha za Umma. Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona kwamba, kila mapato yanayokusanywa yanatumika ipasavyo na kwa manufaa ya Wananchi wa Tanzani," alisema Dkt. Ashatu.

Wakati huohuo,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof.Mussa  Juma Assad leo Jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la uapisho wa Majaji uliofanywa na Mhe. Dkt. Magufuli, amethibitisha mbele ya Majaji kuwa hakuna mahali katika ripoti yake aliposema kuna shilingi trilioni 1.51 zimefujwa.

Mwisho...                                   

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE