April 23, 2018

RC MASENZA AZINDUA ZOEZI LA UTOAJI WA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI AWAPA RUNGU MA -DC KUWAKAMATA WAPOTOSHAJI

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  wa nne kutoka kulia  akiwa na wasichana  waliopata  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi na wakuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  kutoka  kushoto ,mkuu  wa wilayaa ya  Mufindi Jamhuri  Wiliam na  wa  kwanza kulia mkuu wa  wilaya  ya  Iringa Richard Kasesela   na kulia kwake mtoa huduma ya  sanjo ,
Wakuu wa  wilaya ya  Mufindi na  Iringa kutoka  kulia  wakiwa na  watoa huduma  ya  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi  na mkurugenzi  wa Halmashauri ya  mji Mafinga 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa  hotuba  ya  uzinduzi wa  chanjo  ya saratani ya  mlango wa  uzazi kwa  wasichana wa  miaka  14  mkoani Iringa 
Viongozi  mbali mbali  wakifuatilia  hotuba ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amiana Masenza leo 
Wanafunzi  wa  shule za msingi na  sekondari mjini Mafinga  wakiwa katika  uzinduzi wa   chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi leo 
Baadhi ya  watoa  huduma  na  walimu  wakifuatilia  hotuba ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa 
Mkuu wa  wilaya ya Mufindi  Jamhuri  Wiliam akicheza  nguma ya  njuga na kikundi cha  sanaa
Utamu wa  ngoma  ya  njuga 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akijumuika kucheza ngoma  ya njuga  
Mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  akipata  maelezo kabla ya  kukata  utepe  kuzindua zoezi la  chanjo ya saratani ya  mlango wa  kizazi kwa wasichana wa  miaka 14 
Masenza  akikata  utepe  kuzindua  zoezi la  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akishuhudia  uzinduzi wa  zoezi la  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi kwa  wasichana wa miaka 14 
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akimpongeza msichana  wa miaka 14  aliyepewa  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi leo 
Zoezi la  Chanjo  ya  saratani  ya mlango wa  kizazi yapokelewa  vizuri  Iringa 
Mtoa  huduma  akimpa  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi msichana wa miaka 14  huku mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akishuhudia 
Binti  wa nyumbani  akijiandaa  kupewa  chanjo ya  saratani ya  mlango wa  kizazi 
RC Masenza  akisisitiza  umuhimu wa  wazazi  kuwapeleka mabinti zao wa miaka 14  kupewa chanjo 
Binti wa  nyumbani  akipewa  chanjo hiyo 
Mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza akiwa katika  picha ya  pamoja  na wasichana  wa  miaka 14 waliopatiwa chanjo ya  saratani ya  mlango wa  kizazi 
Picha ya  mkuu wa  mkoa na mabinti wa  miaka 14  waliopewa  chanjo ya  saratani ya  mlango wa  kizazi  wakionyesha kadi  zao 
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akiwa na  viongozi wa  dini na  mkurugenzi  mji Mafinga wa  pili  kushoto  mara  baada ya  kuzindua  zoezi la  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi leo mjini Mafinga 
Watoa huduma ya  chanjo  na  mkuu wa mkoa wa Iringa wakiwa katika  picha ya pamoja na wasichana  wa miaka 14  waliopewa  chanjo ya saratani ya mlango wa  kizazi  
Wadau  wa  chanjo na mkuu wa mkoa katika  picha ya pamoja na  wasichana  waliopewa  chanjo  hiyo 
Watoa   huduma wa  chanjo na  walimu wakiwa katika  picha ya pamoja  
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akizungumza na  wasichana wa miaka 14  waliojitokeza  kupewa  chanjo ya  saratani ya mlango wa  kizazi  leo mjini Mafinga 

...................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog 

MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina  Masenza  ameziagiza kamati  za  ulinzi na  usalama za  wilaya  ya Mufindi , Kilolo  na  Iringa  kuwakamata  wale wote  watakaopotosha  ama  kufanya  uchochezi  kwa  jamii  dhidi ya  chanjo  ya  saratani  ya  mlango wa  kizazi  iliyoanza  kutolewa mkoani hapa.

Akizundua  zoezi la  chanjo ya  Saratani  ya mlango wa  kizazi kimkoa katika  uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga   wilaya ya  Mufindi  leo  mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema kuwa  serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais  Dkt  John  Magufuli Pamoja na  wadau mbali mbali   wamegharamia  chanjo  hiyo na  hivyo  wasichana  wato  wa  miaka  14  wapatatiwa  chanjo  bila malipo .

Hivyo  alisema kutokana na  nia  njema  ya  serikali  kwa  kuwajali watu  wake  kwa  kuwakinga na  vifo  vitokanavyo  na  saratani ya  mlango  wa  kizazi asingependa   kuona ndani ya  mkoa wa Iringa kunakuwepo  na  upotoshaji  wa  kukwamisha  zoezi hilo na  pale  itakapobainika   kuna  mtu ama  kikundio  cha watu  wanafanya  upotishaji  vyombo   vya  ulinzi na  usalama  zisisite  kuwachukulia hatua.
“  Chanjo   hii  ni  salama  haina madhara  yoyote   hivyo  wasichanaa   wote  wa  miaka 14  wafike  kupewa  chanjo  nawaombeni  sana  viongozi wa  dini  zote   kuhamasisha waumini  wao  kupeleka mabinti wa  miaka 14  kupata  chanjo   hii wapo baadhi ya  watu wamezoea  kupotosha kwa  kujifanya madaktari  wakija  na upotishaji  walilizeni  wamesoma  chuo  gani na  waonyeshe  vyeti vyao pia  ila  niwaombea wakuu wa  wilaya kama viongozi wa kamati za  ulinzi na usalama watakaofanya opotoshaji kamateni “
Alisema  kuwa uanzishwaji wa chanjo hiyo  utahusisha Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na  kuwa walengwa wa chanjo hii kwa mwaka huu wa 2018 ni wasichana wote wanaotimiza umri wa miaka 14, ambapo takribani wasichana wasiopungua 616,734 wanatarajiwa kupatiwa chanjo nchi nzima.

Wakati  kwa mkoa wa Iringa kwa mwaka 2018 wamekusudia kuwafikia  kwa  chanjo  wasichana 17,840.

“Ni vyema sote kwa pamoja tukafahamu njia za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi ni njia ya kwanza ni kwa kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi,kubadili tabia ili kujiepusha na maambukizi ya kirusi cha Papilloma “

Alisema  mkuu  huyo wa  mkoa kuwa njia ya pili ni kufanya uchunguzi wa mabadiliko ya awali mara kwa mara ili kubaini dalili za awali na kupata matibabu stahiki mapema wakati  njiaya tatu ni kupata matibabu maalum kwa mtu ambaye tayari amepata saratani ya mlango wa kizazi.


Masenza alisema  kuwa huduma za uchunguzi na tiba zinapatikana mkoa wa Iringa akatika vituo 16 zikiwemo  Hospitali ya mkoa Iringa, Hospitali zote za Wilaya na vituo vichache vya Afya.

“Napenda kuchukua nafasi hii kupongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kwa kutoa kipaumbele kwenye sekta ya afya na hususan uanzishwaji wa chanjo ya Papilloma  pia nawashukuru  sana Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Jinsia, Wazee an Watoto, wadau wa chanjo likiwemo Shirika la Gavi, Shirika la Afya Duniani (WHO),Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Jhpiego kwa kutoa msaada mkubwa kwenye Mkoa wetu. Kipekee shukurani ziwaendee mdau Jhpiego kwa ufadhili wa GAVI kwa kufadhili uzinduzi huu”

Mratibu  wa chanjo   hiyo  wilaya ya  Mufindi Jacquline  Mwendwa    alisema  kuwa  kumekuwepo na hamasa  kubwa  walengwa  wa  chanjo   hiyo  kujitokeza  katika  wilaya ya  Mufindi na  kuwa  wanauhakika wa  kufikia  malengo  yaliyowekwa  ya  utoaji  chanjo  hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE