April 13, 2018

RC MAKONDA APONDWA NA WAGANGA WA TIBA ASILIA KUWA AMEKURUPUKA 

 MWENYEKITI  wa shirikisho  la    waganga  wa  tiba asilia  mkoa  wa  Iringa Simba  Kasige  amemtaka  mkuu  wa  mkoa wa  Dar es Salaam Paul Makonda kusitisha zoezi lake la wanawake  waliotelekezewa  watoto kwani limelenga  kuwavunjia  heshima  wanaume  na kuvunja ndoa  za  watu .

Akizungumza  leo   mjini Iringa wakati wa mahojiano katika  kipindi cha  gari la Matangazo Radio  Nuru FM alisema  kuwa zoezi  hilo limeanzishwa  pasipo  kutafakari  madhara  yake  na kuwa  wanawake  wanaokwenda  kwa Makonda  wanapaswa  kuchukuliwa  hatua kwa  kuingilia ndoa za  watu .

Alisema  kuwa ni kweli  wapo  wanawake  wanaotelekezewa  watoto ila  wapo  baadhi ya  wanaume  wanachafuliwa katika  zoezi  hilo na  kuwa  ufumbuzi  wa  changamoto hiyo  haupo kwa  mkuu wa  mkoa ila  unapatikana ustawi  wa  jamii ama  mahakamani  na  kuwa  kinachofanywa na  mkuu wa   mkoa  huyo ni  kuchafua  watu na  kufanya kazi isiyo  mhusu.

"   Sisi kama  waganga  wa  tiba  asilia tunaomba  sana serikali  kutumia  vizuri  ofisi   za umma ziwe  kwa ajili ya  kujenga amani na kuleta maendeleo ya  Taifa  sio  kutafuta umaarufu unaovunjia  watu  heshima  zao hii  ni ajabu sana  ni  kituko kuona ofisi ya  mkuu wa  mkoa inatumika  kuwachafua watu "

Mwenyekiti  huyo  alimkata  Makonda kufikiri kwa kina kabla ya  kufanya jambo ambalo  linaweza  kuchafua  taifa kama  zoezi lake  hilo  linaloendelea  la  wanawake  waliotelekezewa  watoto .


 " kwa  wanawake  ambao  wamejitokeza kwa Makonda kudai  wametelekezewa  watoto wanapaswa  kuchukuliwa  hatua  ya  kuingilia  ndoa za  watu wao  wanalalamika  kuzalishwa  hivi kama  walikuwa  na maambukizi ya  UKIWI sio  ndio  wamesababisha  majanga  kwa  wake  wa  hao  waliozaa nao"

Alisema  wote  waliokwenda  kwa Makonda  kudai  wametelekezewa  watoto majina  yao yachukuliwe  ili  wake  wa waume  hao  wafungue  kesi mahakamani kwa  wagoni  wao  waliojitokeza kudai  wametelekezewa  watoto .

Hata  hivyo  alisema  kuwa  wengi  wao  wanatumia  njia  hiyo  kutafuta  pesa kwa  watu  wenye  heshima  zao jambao  ambalo  halitavumiliwa .

" Tunamuomba  sana  mkuu wa  mkoa wa  Dar es Salaam Paul Makonda kutumia nafasi yake  vizuri  sio  kuendelea  kuingilia majukumu ya  idara  nyingine pia  wakuu wa  mikoa  wengine na  wakuu wa  wilaya wasiige zoezi hilo la Makonda "

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE