April 28, 2018

RAIS DKT MAGUFULI KUANZA ZIARA YA SIKU SITA MKOANI IRINGA KESHO


Image result for magufuli na Masenza

RAIS  Dkt  John Magufuli  kuanza  ziara ya siku  sita  mkoani Iringa  kesho .

 Akizungumza leo   na  waandishi wa habari  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  alisema  kuwa  katika  ziara hiyo mkoani Iringa Rais Dkt Mafuguli
ataweka  jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo pamoja na  shughuli  nyingine na atakuwa mgeni rasmi siku ya  wafanyakazi duniani itakayofanyika kitaifa mkoani Iringa .
  Image result for magufuli na Masenza

“ Rais Dkt  Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atafanya ziara ya Kikazi katika Mkoa wa Iringa kuanzia tarehe 29/4/2018 hadi tarehe 4/5/2018”

Alisema Katika Ziara hiyo, Rais anatarajia kufungua, kukagua na kuelekeza shughuli mbalimbali za Maendeleo  mkoa wa Iringa.


Alisema  kuwa  Rais yatapokelewa  kesho jumapili  kwenye Kijiji cha Cha Ndolea Wilaya ya Iringa  na baada ya mapokezi atasomewa taarifa ya Mkoa na kufungua Barabara ya Iringa – Migori – Fufu.
Mkuu  wa  mkoa  alisema Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi Kitaifa Mkoani Iringa.
Alisema  kuwa sherehe hizo pia zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo makamu wa Rais, waziri Mkuu,  Spika, Naibu Spika,  Mawaziri,  Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, mabalozi. Image result for magufuli na Masenza

Hivyo alisema  ni bahati  kubwa kwa mkoa wa Iringa  kupata ugeni mkubwa kama  huo  na  kuwataka wananchi  kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Samora  kushuhudia sherehe hizi za kitaifa.
 Hata  hivyo mkuu  huyo wa mkoa alisema  Mei 2 Rais ataweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.
Wakati Mei 3 Rais atazindua kiwanda cha Silverland na  pia atafungua barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga (Ihemi) na kuwa Rais anatarajia kuondoka  Mei 4

Masenza aliwataka wananchi,  kujitokeza kwa wingi na kwa shamrashamra, nderemo na vifijo na furaha tele wakati wa mapokezi (Ndolela), Mei Mosi (Samora) na maeneo yote ya miradi anayotembelea ambapo atapata fursa ya kuwasalimia wananchi.

“Kwa kuwa Iringa kuanzia sasa tumepata wageni wengi wakiwemo wa Kitaifa naomba tuwahudumie vizuri hasa Wamiliki wa mahoteli, watengenezaji wa vyakula. Tuonyeshe kwa vitendo dhana ya kuendeleza utalii wa Ndani ya karibu kusini ili wageni hawa watamani tena kurudi Mkoani Iringa”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE