April 29, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA

Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza akimpongeza Rais Dkt John Magufuli  baada ya  kufungua barabara ya Iringa -  Dodoma  leo

RAIS Dkt  John Magufuli  amewaagiza  wakuu wa  mikoa  na wakuu wa  wilaya  nchini kuendelea  kuwasaidia  wananchi  wanaowaongoza na  kuepuka  kuwakandamiza  kwa  kuacha  wanyanyasike  na  ushuru mdogo mdogo.

Akizungumza  leo katika uzinduzi wa   barabara  ya Iringa – Dodoma  rais Dkt Magufuli  amesema kuwa lengo la  serikali  kufuta  ushuru  mbali mbali ambao ulikuwa ni  kero kwa  wananchi  ni  kutaka  wananchi kutonyanyasika na  manyanyaso ambayo walikuwa  wakiyapata zamani .

“ Sasa  nawaombeni  sana  wakuu wa  mikoa na  wakuu wa  wilaya  siamamieni wanyonge sitapenda kusikia ama  kuona  wananchi  wanyonge wananyanyasika  kwa ushuru  huu mdogo mdogo “


Alisema  kuwa baada ya  bunge kufuta  ushuru mdogo mdogo  wananchi wanayonafasi ya  kusafirisha  mazao  yao tani moja bila  kulipia ushuru  hivyo kazi  ipo kwa  wananchi  kutumia nafasi  hiyo  kuendelea  kusafirisha  mazao yao .

“ naomba  kuwapeni  mbinu  watani  wangu  wahehe   wewe  una  mazao  yako   unaweza  kusafirisha  usiku  kucha  kwa  kupakia  tani  moja moja  unaweza kwa  siku  ukasafirisha hadi tani  20 kwa awamu  bila  kulipa ushuru”

Alisema  kuwa   suala la  kulipa  kodi ni  jukumu la kila  mmoja  ila  hapendi  kusikia  wafanyabiashara   wakinyanyasika  katika  ulipaji wa  kodi  .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE