April 29, 2018

RAIS DKT MAGUFULI ASEMA NI ZAMU YA IRINGA KUENDELEZWA KIUTALII

Rais  Dkt  John Magufuli na  viongozi mbali  mbali  wakikata  utepe  kufugua barabara ya Migori-Fufu  iliyojengwa  kwa mkopo  toka  benk ya  Afrika  na Japani   katika uziduzi uliofanyika  kijiji  cha Ndolela  wilaya ya  Iringa
Waziri  wa Ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi na mbunge wa Ismani  katikati mwenye  miwani akiwa na  spika Job Ndugai na  viongozi wengine
MNEC  Iringa Salima Asas  akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa  Dodoma  kushoto na katibu wa CCM mkoa wa Iringa
Waziri  Lukuvi  akiongozana na spika  wa bunge Job Ndugai
Spika wa  bunge JOb Ndugai  akisalimiana na  viongozi wa  dini
Waziri  Lukuvi  akiwa na  viongozi mbali mbali wa chama tawala
Askafu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Blaston Gavile  akisalimia
Mkuu wa   mkoa wa Iringa Amina Masenza  akiwa na viongozi  mbali mbali jukwaaa  kuu
Mke  wa Rais  mama  Janet Magufuli  akisalimia wananchi
Rais Dkt  Magufuli  na  viongozi  wengine  wakiwasili jukwaaa kuu
Waziri  Lukuvi  akitoa  salam kwa  wananchi
Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi  akiwasilisha vchangamoto za  jimboni kwake mbele ya  rais
Mbunge wa  Kilolo Venance Mwamoto  akiomba  barabara ya Ipogolo -Kilolo  ikijengwa ipewe  jina la  Mfugale 
Mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati  akiomba  Rais  kusaidia   Hospitali ya  Frelimo mashine
Mbunge Kabati  akitoa  salam za  wana Iringa mjini
Rais Dkt  Magufuli  akifungua barabara 
Rais  Dkt Magufuli na  viongozi wengine  wakishirikiana kufungua  barabara
Rais Dkt Magufuli  akimpongeza kwa  kumpa mkono  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza
Mkurugenzi wa  kiwanda cha Iory  Iringa akiwa amejumuika na  wananchi kumsikiliza Rais Dkt Magufuli
kada wa CCM Arif Abri na  viongozi  wengine
Wana CCM  Iringa mji  walivyoupamba mji wa Iringa
......................................................................................................................................


RAIS  Dkt.John Magufuli amesema  zamu  sasa  ni  zamu ya  mkoa  wa  Iringa kujengewa  miundo  mbinu mizuri ya  kama  ilivyokasikazini ili hifadhi ya  Taifa  ya  Ruaha  iweze  kupata watalii  wengi kama  zilivyo hifadhi za Kaskazini.

Hifadhi  ya  Ruaha  ni  hifadhi  yenye  wanyama  wote na  wengi kuliko  hifadhi  nyingine  ila hifadhi  hii  imekosa  kuwa na  watalii  wengi  kutokana na  kukosekana kwa  miundo  mbinu mizuri  ila  sasa tumejipanga  kujenga  uwanja  wa   ndege wa Nduli kwa  kiwango cha lami ili  ndege  kubwa  ziweze  kutoa .

Alisema  kuwa  kwa kujenga   uwanja   huo na  kujenga  barabara ya  kwango cha  lami  kwenda  kutoka  Iringa mjini kwenda  hifadhi ya  Ruaha   kutaongeza  watalii  zaidi .

Rais Dkt  Magufuli  aliyasema  hayo leo  wakati  akiwahutubia wananchi wa Iringa katika kijiji cha Ndolela kata ya Kihorogota Wilaya ya Iringa wakati akifungua barabara ya kiwango cha lami ya  Iringa,Migori Fufu yenye urefu wa kilometa 189.

Alisema  kuwa kukamilika kwa  barabara   hiyo iliyojengwa kwa ufadhiri  Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya Japan kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu itawezesha   ukuaji wa  uchumi  zaidi  kwani barabara   hiyo  kutoka Afrika  ya  Kusini  na Cairo  ilikuwa haijakamilika  upande wa Tanzania  pekee.

Hivyo  alisema  kukamilika kwa  barabara  hiyo pamoja na  kukuza  uchumi   pia ni  moja ya  fursa  kwa mkoa  wa Iringa kuendelea  kupokea  watalii  zaidi .


"Barabara hii ilikuwa na changamoto kubwa,wasafiri walikuwa wanasafiri kwa masaa mengi kufika Dodoma ama mikoa ya jirani lakini kwa sasa tunatumia masaa mawili na kidogo,hivyo tunatakiwa kuitunza ili iwanufaishe  wananchi  na  kuongeza kilimo “

Alisema  kuwa  ili nchi iendelee inahitaji chakula cha kutosha kwani  ni vigumu kujenga uchumi bila chakula,hivyo ninawapongeza kwa juhudu kubwa mnazozifanya katika kilimo na ninawaomba muendelee kulima kwa nguvu zote ili kuendana na soko lililopo hasa katika Mkoa wa Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.

" Ndugu  zangu  wana Iringa mmepewa  barabara,hivyo mnatakiwa tuchangamkie fursa kwa kujishughulisha na biashara,kufuga na kulima mazoa tofauti yanayostahimili ukame lakini barabara hii inapaswa kutuzwa nitasikitika  sana  kuona  alama  za  barabarani  zikitolewa na  wananchi  ambao ndio  watumiaji wa  barabara   hii  kwa  sabubu hata  deni la  mikopo  bado hatujamaliza  kulilipa  sisi   tumechangia  asilimia  12  pamoja na  kulipa  fidia” alisema
Rais  Dkt Magufuli  alisema  kuwa deni  walilokopa wakoloni  Waingereza  kwa  ajili ya kujenga  barabara ya  Uhuru  jijini  Dar es Salaam  deni lake  limemalizika mwaka  juzi amelipa Jakaya Kikwete .

Kuwa  madeni  ambayo  serikali inayalipa   sasa ni madeni  ambayo  yalikopwa na  serikali  za awamu  zote  na  yawezekana  deni langu  ninalokopa  sasa  likalipwa  wakati mimi  sipo  duniani.

Alisema  kuwa deni  linalokopwa  sasa  linaweza  kulipwa hata  miaka  50  na  kuwa  kwa  sasa  serikali yake  imekuwa  ikilipa kila mwezi  kiasi cha  Shilingi bilioni 650 kwa  ajili ya  kulipa  madeni  iliyokopa .

Ila  inaweza  kukutan mtu  anasimama  bungeni  tena  anatoka  huku  huku  Iringa akipita  katika  barabara  hii alafu  anahoji  mbona   serikali inakusanya  pesa  nyingi  zinakwenda   wapi jambo ambalo ni la kushangaza kabisa.


Rais aliwataka  watanzania  kutambua  kuwa uchumi wa  nchi  unazidi  kukuwa  ukilinganisha na  nchi  nyingine za Afrika na  hadi  sasa uchumi  umekuwa  kwa  asilimia  7 na bado  unaendelea  kukuwa na wanaotaka kujua kuwa  uchumi  wetu  umekuwa  kiashiria  moja  wapo ni nchi  kukopesheka .
  


"Serikali ninayoiongoza ina lengo kubwa la kuwasaidia wananchi ambao ni masikini tunahakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zilizopo nchini bila kubughudhiwa.

Kuhusu elimu bila malipo Rais Dkt Magufuli alisema kumekuwa na mwamko kwa wazazi kuwaandikisha watoto waliofikia umri wa kuanza shuleni,pamoja na kuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi waliofikia umri wa kuanza masomo.

"Serikali ya awamu ya Tano tumeamua kuwatumikia wananchi masikini kwa kuongeza bajeti katika wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Afya ili kuboresha Huduma kwa wananchi kwa kupata matibabu bora"

Amezitaka Halmashauri kuweka mikakati ya kuwapunguzia Wananchi ushuru katika Mazoa ili waweze kunufaika na Kilimo na hivyo kujikwamua kiuchumi.

 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano Makame Mbarawa alisema kuwa kukamilika kwa barabara hii kutarahidisha usafiri na usafirishaji  katika mikoa ya Iringa na Dodoma pamoja na mikoa jirani.

Alisema Barabara hii ya Iringa_Migori_Fufu ni sehemu ya  barabara ya Iringa_Dodoma yenye  kilometa 260.

Awali  akisoma taarifa  ya Mradi wa ujenzi wa barabara,mtendaji Mkuu wa TANROADS mhadisi Joseph Nyamhanga alisema kuwa kiasi cha Bil.207.4 zimegharimu ujenzi huo,ambapo Tz.imechangia 12.8 %,Benki ya  Maendeleo ya Afrika 65.9% na Serikali ya Japan imechangia 21.3%.

Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika   Dejene Demessie akitoa  salam kutoka Benki hiyo alisema kuwa Benki inaipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wake Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi yake kwa wakati.

"Hii inaleta Matumaini makubwa kwa wananchi na wale wanaojitoa kusaidia ili waendelee kusaidia"

Demessie alisema Benki ya Maendeleo ya  Afrika  inaipongeza Serikali ya awamu ya Tano  kwa hatua  ya kukuza uchumi wa Nchi.

"Tunaamini barabara hii itaweza kuboresha maisha ya wananchi  kiuchumi kwa kufanya biashara hivyo kujiingizia kipato  Benki inatambua  vipaumbele vilivyowekwa kuhakikisha  Maendeleo  ya uchumi yanaongezeka" Alisema 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE