April 25, 2018

POLISI WAKAMATA WANACHUO RUCU NA MWALIMU WA SEKONDARI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO

Image result for Mange  KImambi, RPC  IringaJESHI  la  polisi  mkoa  wa Iringa  linawashikilia  wawili   wa  chuo  cha  Ruaha  Iringa na  mwalimu  wa shule ya  sekondari ya  Francis mkoani  kwa  kuhamasisha maandamano yaliyopigwa  marufuku  na  jeshi la  polisi maandamano .

Kamanda  wa polisi  wa  mkoa wa  Iringa  Juma Bwire  ameueleza mtandao wa matukiodaimaBlog a  kuwa  tukio  la kukamatwa kwa  wanafunzi hao na mwalimu limetokea  April 23  mwaka huu majira ya saa tatu  asubuhi .

Kamanda  Bwire aliwataja   waliokamatwa  kuwa ni  mwalimu Erick Nyamle  (39)  mwalimu wa shule ya  sekondari Francis , Marsha  Ally (34)   na  Cheyo Oscar (24) ambao  wote ni wanafunzi wa chuo  cha Rucu  Iringa  kitivo cha  sheria mwaka wa  tatu  na  wakazi wa Mjimem,a mjini Iringa  nje  kidogo na  chuo  hicho .

Alisema  watuhumiwa hao  wamekamatwa  kwa kuhamasisha  kwenye  mitandao ya  kijamii hasa kundi la  Whatssap   la Baed 3 Last Semister chuo kutaka  watu washiriki maandamano hayo  kuwa watuhumiwa hao  watafikishwa mahakamani na  kuonya  kuwa  mkoa  wa Iringa hakuna maandamano  hayo na atakayejaribu  kuandamana  kukiona .

"  Ndugu wanahabari  naendelea  kutoa  wito  kwa  watu  mbali mbali  kutojihusisha kwa namna yeyote  ile  katika  kusambaza  taarifa  za kuchochea  maandamano ambayo hayana  kibali  atakayekaidi  tutamshughulikia kwa  mujibu wa sheria  lakini   kuna  watu  ambao wameendelea kupuuza  tutawashurutisha kutii agizo hili "

Wakati huo  huo alisema  jeshi la polisi  mkoa wa Iringa  limewakamata wahamiaji  haramu wanne   kutoka  nchi mbali mbali  ikiwemo  Ephiopia  na  Somaria   ambao  walikamatwa  katika  eneo la  Kitwiru  juzi.

Aliwataja  waliokamatwa  kuwa ni Rabiu Auwel (27), Joseph Eboduni (18) Tradasa  Heshimu (20)  wote  raia wa  Ephiopia  na raia  wawili  wa  Somaria  akiwemo HIano  Khadil (25)Dahed Juma (27) ambao  walikuwa  wakivushwa na bodaboda  kizuizi cha Ndiuka  kwenda  kwenye gari  walilokuwa  wakilitumia kusafiria  kwenda Malawi .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE