April 25, 2018

MPENZI WA ZAMANI WA ADBUL NONDO ,USHAHIDI WAKE PASUA KICHWA AFUNIKWA KUFICHWA...

Nondo kushoto akiwa mahakamani 
Mawakili wa Nondo 
Hivi ndivyo mpenzi wa Nondo alivyoondolewa kwa kufichwa mahakamani aliingia kwa kificho atolewa kwa kificho avaa suti nyeusi na kufunikwa kitambaa cheupe sura yake

Image result for Mange  KImambi, RPC  IringaUSHAHIDI wa  kesi inayomkabili   mwanafunzi Abdul Nondo  umeendelea  kutolewa kwa  upande wa jamhuri kupeleka    mashahidi  wengine wawili  kati ya wa nne  akiwemo aliyekuwa mpenzi wa zamani wa wa Nondo  ,Veronica Slvesta  Fredy (22) mkazi wa Igunga mkoani Tabora kutoa ushahidi wake. .

Shahidi  huyo ambae  alifikishwa mahakamani mbele ya  hakimu wa mahakamani ya hakimu mkazi  mkoa  wa Iringa John Mpitanjia   akiwa  amefichwa na jeshi la  polisi na  kumuingiza   mahamani hapo muda wa  kutoa ushahidi na  baada ya  kumaliza walimtoa nje ya mahakama hiyo na  kumtaka  ajifiche usoni na kuondoka naye na gari lenye Tretedi  na polisi hao . 

Mbele  ya hakimu  wa mahakamani  hiyo  John  Mpitanjia   jana shahidi huyo  ambae  aliieleza mahakama kuwa alipata  kusoma  pamoja na na Abdul Nondo  shule  ya Igunga  sekondari .

Kuwa  yeye  na  Nondo  walikuwa  ni marafiki wakiwa  shule na  pia Nondo alikuwa ni kiongozi wake   shuleni hapo  na baada ya  hapo  alikuwa nae na mahusiano ya kimapenzi kabla ya  kuachana muda  mrefu .

Katika  mahojiano yake na  wakili wa jamhuri  Alex Mwita na Shahidi huyo  mahakamani hapo  aliweza  kueleza hayo   kuwa  elimu yake ni  kidato cha  sita na  sasa anajishughulisha na kazi ya Ususi wa  Nywele  kijijini kwao Igunga .

Vero aliiambia  mahakama  hiyo  kuwa alimfahamu  Nondo   toka Agosti  mwaka 2014  na kuwa mazingira ya kufahamiana  yalikuwa  ya shuleni  kama kiongozi  wake na  kuwa mahusiano yao ya mapenzi yalianza  mwaka 2015 hadi mwaka 2017 mwanzoni na baada ya  hapo  walikuwa na mahusiano ya kawaida .

Hata   hivyo  alisema  njia  ambazo   walikuwa wakizitumia kuwasiliana na  simu pamoja na mitandao ya kijamii hasa  Whatsap  na kuwa anachokumbuka  machi 7 mwaka  2018  majira ya saa 9 usiku  Nondo  alimpigia  simu .

“ulikuwa ni usiku wa pekee  nikiwa nasumbuliwa na mafua nilipigiwa  simu na Nondo  na akaniuliza  uko  wapi nikamjibu nipo nyumbani  Igunga na akaniuliza  unaishi na nani  nikamweleza kuwa naishi pekee yangu akaniomba  kuwa anaomba  aje kwangu ana matatizo nikamtatalia kuwa sitaki”alikata  simu 

Aisema  baada ya  kukata  simu  aliendelea  kulala na majira ya saa 10 usiku simu  yake  iliita na kutazama  aliona namba ya   Nondo safari  hii  alikuwa  akiomba  nimpe namba ya  rafiki yake  Masumbuko  nikamweleza sina baada ya  hapo  alikata simu .

Akijibu  swali  la wakili  upande wa utetezi ,Shahidi  huyo  alisema  anatambua kuwa  wapo  watiu wanaoigiza sauti mbali mbali ili alimtambua Nondo kwa  kupitia  sauti yake namba  yake na kuomba namba ya  rafiki yake Masumbuko  pia  alisema kwa  wakati  akiongea nae  alikuwa ni mtu anayeongea  haraka haraka  namba  iliyotumika  kunipigia ambayo ni tigo inayoishia 25”

Shahidi  huyo  akiendelea  kujibu  maswali ya  wakili wa jamhuri alisema  kuwa alitumia  muda wa dakika  3  mara ya kwanza  kuongea na Nondo  usiku huo na mara ya pili  alitumia dakika kama  4  hivi .

Hata   hivyo  mawakili  upande  wa  utetezi mawakili Jebra  kuwa  kwa mtu anayesafiri  kutoka Dar es salaam  kwenda Igunga Tabora  ni lazima  kufika mkoani Iringa ,pia  aliwezaje  kuitambua  sauti ya Nondo kwa njia ya  simu  wakati  sauti   inaweza kuigizwa   kwa mfano msanii  Steve Nyerere  amekuwa akiingiza sauti nyingi analitambua  hilo  na  kuhoji kuwa alipoachana na Nondo kama mpenzi wake  uliumia ama
Akijibu  maswali ya  wakili  huyo   shahidi huyo  alisema  kuwa ni  kweli  mtu  anyekwenda  Tabora  si  lazima  apite Iringa  na  kuwa anakubaliana kuwa  wapo  wanaoweza  kuingiza  sauti  za watu kama  anavyofanya msanii Nyerere kuhusua kuumia ama kutoumia baada ya  kuachana na Nondo alisema  hakuumia  .
Wakili Jebra  alihoji  kama  bado anampenda  Nondo alikataa kuendelea  kumpenda na kumhoji swali  jingine  kuwa iwapo  hampendi  kwa   hiyo  yupo hapo mahakamani  kumtolea  ushahidi mtu asiyempenda .
Shahidi  huyo  alisema  anampenda kama binadamu mwingine  ma sio mpenzi  na kuwa mbali  ya tarehe  hiyo  pia   aliwasiliana  na Nondo January mosi  2018.

Hata hivyo  Veronica ambae ni shahidi wa tatu  katika kesi hiyo  alisema  amepata  kuishi  mjini Iringa eneo la  Kihesa mtaa wa  Semtema  akiwa anaishi katika nyumba yam zee Chusi  na wakati  huo  alikuwa  akisoma  chuo  cha  Tumaini japo  alisema katika kuishi kwake Iringa hakufahamu  Samora 

Kwa upande wake shahidi wa nne katika kesi hiyo  askari  Abdul  karim
kutoka kitengo ha makosa ya kimtandao  makao makuu Dar es Salaam  alieleza
  mahakama kuwa alipokea vielelezo kutoka kwa koplo John ikiwemo
komputa mpakato pamoja na simu ya mkononi.

Shahidi  huyo  alisema  baada ya kupokea vifaa hivyo alivihifadhi katika
kabati lake na baadae kuja kuvifanyia uchunguzi na alichokibaini
ndicho alichokiwasiisha mbele ya mahakama na kuiomba mahakama iweze
kuchukua vielelezo hivyo ili viwe kama ushahidi .

Hata hivyo upande wa utetezi kupitia wakili Jebra Kambone aliomba
mahakama hiyo kutokupokea kilelezo hicho kwa kuwa kuna mapungufu mengi
hivyo katika kutenda haki aliomba  usitumike huku akitolea mfano
wa kesi mbili zilitotumika kukataa kielelezo kama hicho.

Hata hivyo upande wa jamuhuri kupitia wakili wake Abel  Mwandalamo aliomba
mahakama iweze kuzipitia vizuri kesi hizo kabla hawajaweza kujibu hoja
ziliotolewa na upande wa utetetezi hivyo kuomba masa mawili ili waweze
kupitia  nyema.

Hata hivyo Hakimu John Mpitanjia aliitaka jamuhuri iwe na muda mzuri
wa kupitia vema kesi hizo ili kujiridhisha na kuahirisha kesi hiyo
hadi April 27 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE